0

"Maisha huwa magumu pale
unapopenda usipo pendwa,lakini
huwa
magumu zaid pale unapo kataa
kukubali kua hupendwi, daa. Habiba
miye sikuwahi kudhania ningekuja
kugombania penzi, tena kwa mtu
ambaye hanijali siwezi kuzificha hisia
zangu lakini,sitaki kujidhalilisha pia,

huyu mwanaume mshenzi kani kana
mbele ya umati anadai hanitaki, yeye
na malaya wake walipanga kuniumiza
roho yangu najuta kwa nini niliuliza
swali lile la kumwambia achague kati
yangu na yule malaya anampenda
nani?, Ningejua ningeondoka bila
kuuliza na mimi kiherehere changu na
kukosa maarifa na kutokuuona ukweli
ndiko kumenifanya nibwatuke,, daaah.
Amakweli mtoto akililia wembe mpe
na
ndicho nilichokipata, leo hii kevi
wakunikataa mimi kwa kunidhalilisha
tena mbele za watu na mbele ya yule
malaya wake amakweli
nimeyaona,sinto
rudia tena upumbavu ule tena kwa
staili ile nimekoma nasema
nimekoma"....
..."mawazo yalikua mengi sana
mpaka nilikua nashindwa kuelewa nipo
wapi?, ghafla niliskia
"Habiba Habiba
Habiba,"
....... "nilishtuka kama mtu aliepigwa
shoti ya umeme alikua ni dada yangu
alikua ananishtua niliitikia kana
kwamba nilikua usingizini
"abeeee"
kisha nikafuta machozi "
........dada...."kunamjomba
wako hapa anakupa pole"
........" dada alikua
ananipa taarifa zile nilikua nipo mbali
sana kimawazo na wengi pale msibani
walikua wananionea huruma jinsi
nilivyokua nalia kwa maana nilikua
nalia
kupitiliza kumbe nilikua nalia kwa
mambo yangu mengine tofauti na
msiba
japo nilikua msibani na msiba ulikua
unanihusu,
......mjomba..... " pole sana habiba"..
....habiba....."akhasante
nashukuru".....
......"nilijikaza lakini
nikiwa nimekaukwa na sauti kwa ajili
ya
kulia nilipotoa asante nilifuta tena
chozi sasa sijui lilikua chozi la
kumlilia
bibi alie nitoka au kevi alie niacha,
ilikua
haieleweki, naomba bibi anisamehe
sana, huko
ulipo, maanaake ilikua kama laana
msiba mzima nilikua namuwaza kevi
kana kwamba yeye ndio alikua kafariki,
baada ya masaa kadhaa tulielekea
makaburini makaburi ya
mwananyamala kisiwani , siunajua
tena
waislamu tuliikamilisha safari ya bibi
kwa kumlaza kwenye nyumba yake ya
milele, ilikua inauma sana kwa kweli
alikua ni mtu wangu wakaribu sana
nilimzoea na siri zangu nyingi alikua
anazijua na kilichoniuma zaidi alikua
anamjua mpaka kevi nikikumbuka
hapo
machoz yananitoka zaidi. Daah!! huyu
kevi kanipa donda ambalo sito weza
kulisahau maishani mwangu, asubuhi
sana nilijihimu nakuanza kufanya
usafi
wageni walikua wengi sana jana hivyo
palikua pachafu sana nilifagia kudeki
na kuandaa chai, baadae kama mida
ya
saa nne niliingia bafuni kuoga kisha
nikajiandaa kidogo nikavaa baibui
langu baadae, nikamfuata mama
mkubwa nilikua nimeenda kuongea
nae
kuhisu mambo ya chuo, nilimuomba
ruksa, kuwa nataka niende chuo
kuangalia
majibu kama yametoka maana na
mimi
niliomba chuo cha kigamboni na
wamesema majibu yatatoka leo kwaio
nataka nikaangalie kama nimepita au
lah, mama kubwa alikua si mfuatiliaji
sana alinipa elfu kumi na kunisihi
nisichelewe kurudi, nilimkubalia,
alikua
anajua kuwa nimeomba chuo cha
kigamboni kile kilichopo n'gambo cha
mwalimu nyerere,na nikweli
ndicho.chuo nilichoomba, nilikua
naishi mwananyamala kwaio
nilichukua
gari za mwananyamala kivukoni,
nilikua
nakaa kwa kopa, basi baada kama ya
lisaa nikafika feri pantoni lilikua
linashusha sikukaa sana feri Geti
likafunguliwa tukaanza kuingia kwenye
pantoni, baada kama ya dakika ishirini
tukawa tunashuka kwenye pantoni,
nilimuona james alikua yupo getini
lakini geti la kutokea nilimfuata,naba
adae tukawa tunaongozana nilienda
nae umbali mrefu nikiwa kimya, sana
alijaribu kunidadisi lakini hakupata
jibu, nilimuongelesha mara moja tuu
pale nilipomuambia nataka niende
uwani mara moja, kwakweli sisi
wanawake tunatabu sana, nilikua
nimevaa baibui lakini nilipotoka uwani
kwenye baa flani nilikua mtu mwingine
nilikua nimevaa kimini cha ajabu
sana,nilikua spendi kutoka vile
nyumbani maana mama mkubwa
angeibua maswali na lawama, james
hakuongea kitu ila alikua anameza
mate tuu, nilijua kwa sababu alikua
ananiangalia kwa jicho la tamaa sana,
.....james...."umependeza"...
...."nilitabasamu sikumjibu
kitu chochote, moja kwa moja mpaka
kwenye gest ya entembe ilikua mitaa
ya
kwa dani karibu kidogo na kwa urasa
james alikua keshalipia teyari
alochofanya nikuchukua chips na
mayai
alivyo agiza na baadae tukaingia ndani
chumba namba 9 haikua kazi sana
nilisalula kila kitu nikabaki na chupi tu
baada ya muda alikuja
muhudumu wa gest alileta shuka na
sabuni,
james alivichukua kisha akafunga
mlango, niliamua niwe wakwanza
kuoga,nilienda kuoga na baadae
kidogo
jamesalinifuata, ikabidi tuoge wote
ilikua ni mara yangu ya kwanza
kufanya
vitu vile na james nilikua nimezoea
kuoga na kevi lakini hivi sasa hayupo
tena nilimkumbuka kiasi flani maana
yeye ndio alikua mwanaume wakwanza
kufanya nae mapenzi lakini baada ya
kuleta hitilafu mambo yakabadilika,
ilikua ngumu kidogo kumsahau kevi
lakini ilinibidi, james alikua teyari
yupo
hewani yaani alikua anamidadi ile
mbaya, alikua ananitaka kwa kipindi
kirefu lakini hakuweza kupata kitu,
sababu moyo wangu na roho yangu
Vyote vilikua kwa kevi,haikuchukua
muda
niliingia na james kitandani teyari kwa
ajili ya pambano ilikua mechi nzito
sana,lakini sikuwa na hisia hata
kidogo
nilikua namuwaza kevi tu, sura ya
james nikaitoa kabisa lakini
sikukatisha
tendo sikutaka james ajue kitu,
baadae
kama masaa matano nilijiandaa kwa
ajili ya kuondoka ilikua inabidi niwahi
nyumbani, baada kama ya nusu saa
nilifika nyumbani mida kama ya saa
kumi nambili jioni, wakati nakaribia
maeneo ya nyumbani kuna kitu
kilinishangaza kidogo, nilimkuta dada
yangu ananyonyana ndimi na bwana
Wake, nilitaka kuwapita lakini ilinibidi
nisimame kidogo kisha nigune kama
kuwashtua sikuwai kumuona jamaa
wake
pale nyumbani lakini alikua
ananiambiaga kua anaishi mitaa ya
mwanyamala hospitali, nilipo guna
walishtuka na kuachiana wakawa
wananiangalia niliogopa na
nilidondoka
chini sikuamini nilichokiona"....
Itaendeleaaa.......
Habiba kaona nini?
Zikifika like 20 inaendelea muda huuu
huuu

Post a Comment

 
Top