Elizabeth Asenga (40), mkazi wa jijini Dar es Salaam amepandishwa kortini leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kuandika maneno ya kumkashifu
Rais John Magufuli kupitia mtandao wa kijamii wa What’s App
“Rais kilaza kama huyu wetu, angalia anampa Lissu umashaghuli… fala lile, kwanza picha yake ukiweka ofisini ni nuksi tupu na ukiamka asubuhi ukakutana na picha yake, siku yako inakuwa ina mkosi mwanzo mwisho.”
Hata hivyo, mshitakiwa Elizabeth, amekana mashtaka hayo huku wakili wa serikali akidai kuwa, upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.
Mtuhumiwa amepewa dhamana yenye masharti yanayohitaji wadhamini wawili huku kila mmoja akitakiwa kusaini hati ya shilingi 3 millioni.
Kesi hiyo imeahirishwa na inatarajia kutajwa tena mnamo tarehe 22 Septemba, mwaka huu.
Post a Comment