0

Baraza la Wazee wa Chadema limesema  kuna  njama za kukifuta chama hicho zinazopangwa kupitia Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi.

Pia, baraza hilo ambalo
limekemea vikali njama hizo na limedai kuwa, Jaji Mutungi anafanya hivyo ili kutimiza matakwa ya watawala kwa kutumia mwavuli wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania.
Katibu Mkuu wa baraza hilo, Roderick Lutembeka amesema  taarifa kuhusu njama hizo zinathibitishwa na mtiririko wa matukio ya hivi karibuni kupitia Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa.
“Taarifa zimeonyesha kuwa njama hizo zinalenga kukihujumu Chadema kwa kuandaa mitego haramu ya kisiasa ili yatolewe mapendekezo ya kukifuta katika orodha ya vyama vya siasa,” alisema Lutembeka.
Hata hivyo, Lutembeka amesema Chadema haitegemei jambo hilo kutokea kwa sababu inafanya shughuli zake kwa kufuata misingi ya sheria na Katiba.
Lutembeka amesema miongoni mwa matukio hayo ni  kuahirishwa kwa baadhi ya vikao vilivyopangwa kufanyika kati ya Jaji Mutungi na Baraza la Vyama vya Siasa.
Miongoni mambo ambayo yamepangwa kujadiliwa kwenye mkutano huo, ni changamoto za mfumo wa demokrasia ya vyama vingi hususan zuio la shughuli za vyama vya siasa.
Source Mwana Halisi


Post a Comment

 
Top