0

HAMIDU Hassan Bobali, Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni Wizara ya Maji ameitaka serikali itoe tathmini ya mradi wa kuvipatia maji vijiji 10 uliotekelezwa mwaka wa fedha wa 2015/2016, anaandika Wolfram Mwalongo.


Bobali amesema mradi huo ulitekelezwa pasipo kufanyika kwa upembuzi yakinifu kwenye maeneo yaliyo paswa kuchimbwa kwa visima hivyo.

Aidha amesema, visima vingi vilijengwa na tasisi za Dini ya Kiislamu na Kikristo na fedha hizo zikiingia mfukoni mwa watendaji wachache huku halmashauri zikidai kutekeleza mradi huo.

Hata hivyo katika kitabu cha mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2016/17 kuhusu miradi ya Maji Vijijini inaonesha kuwa, imejengwa miradi mipya ya maji 975 katika vijiji 1,206 kwenye vituo 24,129 katika Halmashauri 148.

Kambi ya Upinzani Rasmi Bungeni imeitaka serikali takwimu zikaeleza kwa uwazi kwa kila Halmashauri, kata gani, kijiji gani kati ya hivyo vijiji 1,206 na vituo 24,129 vipo katika kitongoji kipi, kwa mtiririko huo ni dhahiri hata maswali kwa Serikali yatapungua au udanganyifu unaofanyika utapungua kama sio kumalizika kabisa.

Post a Comment

 
Top