Su Bin anaaminika kuwa
kwenye kundi
la watu ambao wamekuwa wakiiba habari kuhusu ndege za kivita,
ndege za kubeba mizigo na silaha.
Wizara ya haki ya
Marekani imesema kupitia taarifa kwamba Bw Su alilenga kufaidi kifedha.
Bw Su, mwenye umri wa
miaka 50, alikamatwa akifanya kazi nchini Canada mwaka 2014.
Alidaiwa kuwa na
kampuni ya Kichina ya teknolojia ya uchukuzi wa ndege iliyokuwa na afisi Canada
na alikamatwa akijaribu kupata uraia wa Canada.
Alikiri kufanya kazi na
watu wawili kutoka Uchina kati ya Oktoba 2008 na Machi 2014 kudukua mifumo ya
kompyuta ya Marekani, ikiwemo kampuni ya Boeing inayotumiwa na jeshi la
Marekani kuunda ndege zake.
Sasa anakabiliwa na
kifungo cha miaka mitano jela na faini ya $250,000 (£170,000).
SOURCE BBC
Post a Comment