Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesimamisha bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa Nyumba (NHC) kuacha kufanya ujenzi mpya wakuacha kuanzisha miradi mipya ya ujenzi hadi kati kuna miradi haijakamilika lukuvi ameongea hayo alipokuwa akizungumza na bodi jijini Dar es Salaam alisema
“Nadhani miradi iliyopo mnaijua na tarehe za kukamilika ujenzi wake wote tunafahamu, hivyo nitoe agizo kuanzia leo hakuna kuanza kwa mradi mpya wowote mpaka imalizwe iliyokwishaanza,” alisema.
Lukuvi pia aliiagiza bodi hiyo kutopandisha kodi za nyumba zake bila ridhaa yake huku akisisitiza gharama zipangwe kwa kuzingatia uwezo wa wananchi.
“Hamuwezi kusema nyumba ya gharama nafuu wakati ina vyumba viwili na inauzwa kwa Sh52 milioni, hainiingii akilini na wala Mtanzania wa kawaida hawezi kuona unafuu wowote hapo,” alisema Lukuvi.
Post a Comment