Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amewalipa baadhi ya wakandalasi w
anao hidai serikali na
kuwarudisha kazini wote waliosimamishwa huo unaonekana kama ni udhaifu
mkubwa Prof. Mbarawa alisema tayari Serikali
imeshalipa makandarasi mbalimbali nchini shilingi bilioni 400 na itaendelea
kufanya hivyo ili kumaliza madeni yao kwa haraka.
“Hakikisheni mnarejea kazini na kuwapa
mikataba ya ajira wafanyakazi wenu katika kipindi cha wiki mbili kuanzia sasa
ili ujenzi wa barabara na madaraja ukamilike kwa mujibu wa mkataba na hivyo
kuondoa usumbufu kwa watumiaji wa barabara hii”, alisema Prof Mbarawa.
Profesa Mbarawa amemhakikishia mkandarasi
China Civil Engineering Construction Corporation anayejenga barabara ya
Magole-Turiani kuwa tayari serikali imeshamlipa zaidi ya kiasi cha dola za
kimarekani zaidi ya laki 735 na Shilingi za kitanzania zaidi ya Milioni 795
hivyo ni wakati wa kukamilisha ujenzi huo hususan sehemu za madaraja kabla ya
mvua za masika kuaanza.
Akizungumza katika ukaguzi huo Mbunge wa
Mvomero Mhe. Sadick Murad ameiomba Serikali kumalizia daraja la Diwale lenye
urefu wa mita 75 ili liweze kupitika.
Katika hatua nyingine Waziri Prof. Mbarawa
alikagua karakana ya ujenzi wa vichwa vya treni mjini Morogoro na kumtaka
mkandarasi anayekarabati vichwa hivyo kufanya kazi hiyo kwa haraka na kutoa
kazi nyingine kwa watanzania ili kuwajengea uwezo wa kazi hizo.
Amewataka wafanyakazi wa Shirika la Reli
Tanzania (TRL) Kufanya kazi kwa ubunifu, uadilifu na uwazi ili kufufua hadhi ya
Shirika hilo ambalo ni muhimu kwa uchumi wa nchi hii.
Alisema takribani asilimia 96 ya mizigo
inayoshushwa katika Bandari ya Dar es salaam husafirishwa kwa njia ya barabara
hivyo ni jukumu la TRL kuhakikisha inapata mizigo ya kutosha ya kusafirisha ili
kupunguza mizigo hiyo kusafirishwa na barabara lakini kufufua uchumi wa TRL na
taifa kwa ujumla.
“Fanyeni kazi kwa bidii, uwazi na kwa
kushirikiana ili kujenga Shirika la Reli la kisasa lenye uwezo wa kujitegemea
acheni vitendo vya hujuma na migomo vinavyoweza kudhoofisha shirika hili”, alisisitiza
Prof. Mbarawa.
Naye Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano
Eng. Edwin Ngonyani alikemea vitendo vya wizi wa mafuta na kuhujumu Reli
vinavyofanywa na watumishi wasio waaminifu na kuwataka kuwa wazalendo kwa nchi
yao ili kuchochea kasi ya maendeleo.
Profesa Mbarawa alikuwa kwenye ziara ya
kukagua utendaji wa taasisi zilizo chini ya Wizara Ujenzi,Uchukuzi na
Mawasiliano ambapo alipata fursa ya kukagua ujenzi wa mizani ya kisasa ya
Mikese na kituo cha mtandao wa mawasiliano ya simu vijijini ya Halotel
unaosambazwa katika taasisi za Serikali ikiwemo Hospitali, Polisi, Mahakama na
Shule hapa nchini.
Post a Comment