Bariadi.
Watu tisa wamefikishwa mahakamani wakituhumiwa kutungua helikopta iliyokuwa
ikifanya doria kwenye Pori la Akiba la Maswa wilayani Meatu, Simiyu na na
kumuua rubani wake.
Mbali na
kutung
ua chopa na kumuua rubani wake, Rogers Gower, raia wa Uingereza, watu hao
pia wameshtakiwa kwa kukutwa na nyara za Serikali, kuuza na kumiliki silaha
kinyume cha sheria.
Washtakiwa
hao walifikishwa mbele ya Mahakama ya Mkoa wa Simiyu jana wakiwa chini ya
ulinzi mkali wa polisi, huku umati wa wananchi wakifurika na kusababisha
hekaheka mahakamani hapo.
Yamiko
Mlekano, ambaye ni wakili mwandamizi wa Serikali, alidai kuwa washtakiwa wote
kwa pamoja wanakabiliwa na kesi tatu; uhujumu uchumi, mauaji na umiliki wa
silaha bila ya kibali.
Katika
kesi namba mbili ya mauaji, Wakili Yamiko alidai kuwa Shija Mjika (38), Njile
Gunga (28), Dotto Pangali (42) na Moses Mandagu walitungua helikopta hiyo
Januari 29 kwenye Hifadhi ya Mwiba iliyoko Kijiji cha Makao wilayani Meatu na
kumuua rubani Gower.
Mlekano
alidai kuwa katika kesi ya uhujumu, mshtakiwa namba moja Iddy Mashaka (49)
anadaiwa kujihusisha na kuratibu tukio la uhujumu uchumi kinyume na sheria.
Mbele ya
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi, John Nkwabi, wakili huyo alida kuwa mshtakiwa
alitenda kosa hilo Januari 6 na Februari Mosi wilayani Meatu kwa kumshauri
mshtakiwa namba mbili, Shija Mjika (38) kuua wanyama wasioruhusiwa.
Katika
shtaka la pili, watu saba; Njile Gunga (28), Dotto Pangali (42), Moses Mandagu
(48), Dotto Huya (45), Mwigulu Kanga (40), Mapolu Njige (50) na Mange Barumu
(47) pia wanashtakiwa kwa kuhujumu uchumi.
Aliieleza
mahakama kuwa kati ya Januari 21 na 29 katika wilayani Meatu, washtakiwa
walipanga na kuratibu tukio la kuwinda wanyama aina ya tembo bila ya kibali cha
Serikali.
Wakili
Mlekano alidai kuwa shtaka la tatu la uwindaji wanyama wasioruhusiwa
linawakabili mshtakiwa wa pili hadi tisa na wanadaiwa kutenda Januari 26 na 29
kwenye Hifadhi ya Mwiba Kijiji cha Makao wilayani Meatu wa kumuua tembo mwenye
thamani ya Sh32,891,100 bila ya kibali.
Katika
shtaka la nne, mshtakiwa namba mbili na tisa wanatuhumiwa kumiliki nyara za
Serikali kinyume na sheria.
Washtakiwa
wanadaiwa kutenda kosa hilo Januari 29 na Februari Mosi wilayani Meatu ambako
walikamatwa na meno ya tembo yenye uzito wa kilo 31 na thamani ya Sh32,891,100.
Katika
shtaka namba tano, Mashaka na Mjika wanashtakiwa kwa kuuzaji nyara za Serikali
kinyume na sheria na kwamba walitenda kosa hilo kati ya Januari 6 na Februari
Mosi wilayani Meatu.
Hakimu
Nkwabi alisema washtakiwa hawatakiwi kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo
kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo na aliahirisha hadi Februari 24
zitakapotajwa tena.
Katika
kesi ya tatu ambayo ni kukutwa na silaha kinyume cha sheria iliyosomwa mbele ya
Hakimu Mfawidhi wa Wilaya, Mary Mrio, washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka
matano.
Washtakiwa
hao ni Buluma, Mjika, Pangani, Ngunga, Mandagu, Huya na Kanga ambao
baadhi yao walikiri kumiliki silaha na risasi kinyume cha sheria akiwamo
Njile anayedaiwa kutungua helikopta hiyo.
Washtakiwa
hao walikiri mashtaka mawili ambayo ni kukutwa na bunduki aina ya Riffle
303, wakati Ngunga na Mandagu walikiri shtaka la tatu, nne na tano la
kukutwa na silaha na risasi bila ya kibali.
Hata
hivyo, Hakimu Mrio alishindwa kutoa hukumu kwa washtakiwa waliokiri kosa
kutokana na kutokuwapo kwa vielelezo mahakamani hapo, hivyo kesi hiyo
iliahirishwa hadi
SOURCE MWANANCHI
Post a Comment