0
Wahamiaji 24 wamekufa maji baada ya boti walimokuwa, kuzama karibu na kisiwa cha Samos kilichoko
Ugiriki mkabala na Uturuki.
Watu wengine 11 waliokolewa.
Waokoaji wanaendelea kutafuta miili ya watu wengine 11.
Watoto kadhaa walikuwa miongoni mwa wahasiriwa kulingana na walinzi wa ufukweni wa Ugiriki.
Hii ni ajali ya pili katika siku mbili.
Wahamiaji wengine 7 walikufa maji karibu na kisiwa cha Kos kilichoko Ugiriki siku ya Jumatano.
Hadi kufikia leo takwimu zinaonesha kuwa takriban watu 200 wamepoteza maisha yao wakijaribu kuingia bara Ulaya mwezi huu pekee.
Hadi kufikia tulipochapisha habari hii, uraia wa wahasiriwa haukuwa umebainika.
Umoja wa Ulaya umetoa ilani kwa Ugiriki likiitaka iimarishe ulinzi wa mika yake la sivyo hatua za pamoja zitumiwe dhidi yake.
Maafisa wa uhamiaji wa Ulaya wametumwa katika eneo la Samos kujaribu kudhibiti hali na kuwaokoa watu.


SOURCE BBC

Post a Comment

 
Top