0


Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA Salum Maalim amelaani vikali kitendo cha serikali kutaka kutoonyeshwa
kwa matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya bunge kwa sababu ya gharama, akiongea na waandishi wa habari leo Alhamisi 28/01/2016 katika ofisi za CHADEMA makao makuu Kinondoni Dar es salaam, alilaani kitendo hicho na kusema ni kuwanyima wananchi haki yao ya msingi ya kupata habari na kwamba serikali ya awamu ya tano inataka kuendesha nchi kidikteta na kutaka kuficha maovu yake.

Kutokana na kile kilichotokea ndani ya bunge la Jamuhuri la muungano wa Tanzania siku ya Jumatatno 27 Januari 2016, na matukio mengine ambayo yameendelea kufanywa na serikali ya awamu ya tano inadhihirishasha ni vitendo vya udikteta. Serikali ilianza kwa kupiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa na wakiwa Lindi Waziri mkuu na Katibu wa, Itikadi na uenezi CCM ambaye pia ni waziri wa habari, michezo, wasanii na utamaduni Mhe. Nape Nnauye alisema, Kaimu Katibu Mkuu Salum Mwalimu akanukuu alichokisema Mhe. Nape “Waachwe walioshindwa wafanye kazi yao, hakuna mikutano ya hadhara kwa vyama vyote”.

Baadae likafuata tamko la jeshi la polisi likikazia, kauli hiyo ya serikali, baaada ya hapo, tukaoana bungeni namna ambavyo kamati za bunge zilivyoundwa, ukiangalia umuhimu na unyeti wa kamati zenyewe na shughuli za kamati hizo katika kutimiza shughuli za bunge na kuisimamia serikali, kamati zimeundwa katika namna ambayo unaona kabisa ya kwamba serikali hii haitaki changamaoto, haitaki kusimamiwa, haitaki kuonekana upande wake mwingine.

Wiki moja baadae serikali inakuja kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya bunge, achilia kwamba sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 inaeleza wazi kabisa chama cha siasa kitaendesha shughuli zake kwa mikutano ya hadhara na maandamano, lakini wao wakasema hapana, kauli ya walioshindwa waachwe wafanye kazi zao hii ina maana kwamba wengine wote hamna thamani ondekeni uwafanye wanavyotaka, wakakiuka sheria hatijulikani mamlaka hayo wameyatoa wapi?.
Kamati za bunge zilivyotenegenezwa unajua kabisa kuna mtu alipaswa kuwa pale, huyu alipaswa kuwa hapa kwa uzoefu wake au kutokana na uwezo wake lakini haikuwa hivyo, badala yake tunashuhudia vituko vya hali juu katika uundwaji wa kamati hizo, baada ya wiki tunaoana tena katiba ikivunjwa, kule wakati wanapiga marufuku mikutano walisema nchi bado ipo katika joto la uchaguzi.

Leo wanavunja katiba ya kimsingi kabisa inayowapa watu haki kupata taarifa kwa kisingizio cha gharama, wakitoa mfano wa mabunge mengine, hii ni wazi kwamba serikali ya awamu ya tano inataka kuendesha nchi kidikteta na inataka kuficha maovu yao.
Huwezi kupiga marufuku mikutano ya hadhara, mtu muovu huwa anajijua anajitafutia kinga, huwezi kuzuia bunge, hawataki watu wawasikilize nje katika mikutano, na hilo kimsingi wakati haujafika hatukuwa tayari na operesheni , opersheni za CHADEMA bado zinaandaliwa zitafanyika tu, hayupo mwenye mamlaka juu ya sheria, wengine wameuliza kwanini CHADEMA hawafanyi mikutano lakini ni kwa sababu muda bado ila tupo kwenye mikakati ya kuanza ziara kwa sababu tunaruhusiwa na katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Hatuwezi kukubali kuzuiliwa kufanya shughuli zetu kwa kauli zisizo namashiko, mikutano ipo program zinaandaliwa.

Leo wanaminya bunge, ni dalili za Udikteta, dalili za hofu , serikali imejawa na hofu, na wanajua hawana kitu ni mbwembwe tu, zisizokuwa na mashiko, leo imekuwa ni fasheni unasikia huyu kamfukuza huyu huyu kamfukuza yule, hakuna hata mmoja aliyetoka akatuambia amefanya hiki, amefanya hiki, kufukuza fukuza watu ni dalili za udikteta pia, kwa sababu udikteta maana yake ni kinyume cha utawala wa sheria kwa maana ya utawala bora, na usio zingatia misingi ya sheria na katiba, sasa tunaona jinsi sheria zinavyovunjwa, katiba inavyovunjwa, hakuna tafsiri nyingine, kwamba kama hutaki kuzinagatia sheria, kanuni na taratibu maana yake wewe ni dikteta.

Tunapinga sababu zilizotolewa na Mhe. Nape, hazina mashiko, amezungumza sababu za gharama, ni gharama zipi? Akizungumza Salum Mwalimu alisema “ eti 4.2 bilioni, sijui, labda katika utawala ule ule wa kiserikali, mimi nimekuwa mwandishi wa habari, nanimefanya kazi kwenye TV, kila nikichambua, 4.2 bilioni kwa ajili ya kurusha bunge muda ambao sio prime time? Yani kila nikipitia rates za televisheni zote sioni hiyo 4.2 bilioni inapatikanaje, Nape aje atuchambulie, asiishie kutaja figures za jumla, aje atuambie amekokotoaje hiyo 4.2 bilioni ya TBC kurusha vipindi vya bunge, bunge linakaa mara ngapi kwa mwaka? Leo tuangalie vipindi vya TBC, with very due respect, wala sina sababu ya kuwasema vibaya TBC, vipindi vinavyorushwa majira ya saa 3 mpaka saa 7 ni vipindi vya aina gani? Na sio kwa TBC tu…Televisheni zote” alisema MSalum Mwalimu.

Akiendelea kuongea Kaimu Katibu Mkuu CHADEMA Salum Mwalimu aliongeza “Mimi nimeafanya kazi kwenye TV muda wa saa 3 mpaka saa 7, utakuta muziki, utakuta marudio ya tamthilia, utakuta sijui burudani, ndio muda huo vipindi vya bunge vinaporushwa, Nape aje atuambie ni kitu gani cha msingi kinachorushwa kwenye TV yeyote hapa nchini ikiwemo TBC muda huo? Na kama ni cha msingi inakuwa ni marudio, sijaona kipindi cha msingi kwa mara ya kwanza kimerushwa saa 4 asubuhi, saa 5 asubuhi, saa 6 mchana na saa 7 mchana sijaona, kwa sababu muda ule sio prime time” aliongeza.

Mhe. Nape aliulizwa na waandishi wa habari serikali si imetenga fedha? Mhe. Nape akajibu kwamba kweli fedha zimetengwa lakini hazitoki, lakini hapo uzembe ni wa nani? Huwezi kuwahukumu wananchi kwa uzembe wa serikali, kwamba wanatennga bajeti lakini fedha hazitoki. Lakini hao hao ndio wanatamba, tumeokoa hiki, tumeokoa kile, makusanyo yameongezeka kama makusanyo yameongezeka wangeenda kupitia bajeti.

Kwa hiyo alichokizungumza Mhe. Nape hakina uhalisia na kama Mhe. Nape anataka tumuamini atukokotolee hizo gharama, hakuna televisheni inayoonyesha mambo mazito ya msingi yanayowaweka watu pamoja kuyaangalia saa 4 usiku, ndo maana hakuna televisheni inayoonyesha taarifa ya habari saa 4 usiku. Hata mtu ukijiuliza saa 4 usiku unakuwa wapi? Unafanya nini? Unajiandaa na nini? Walio wengi kama hawako njiani wamechelewa kutoka makazini, basi washafika nyumbani, washaangalia habari saa 2 na vipindi vingine hadi saa 3 kisha unakwenda kulala tayari kupambana na siku inayofuata.

Kijiji gani, wakulima gani ambao Mhe. Nape anasema watakaa wasubiri bunge? Umeme wenyewe ni wa solar, Tv zenyewe ni kushirikiana watu wanakusanyika wanaangalia, baada ya hapo TV zinazimwa watu wanakwenda kulala, hakuna mtu anayekaa mpaka saa 5 usiku kuangali tamthilia hakuna. Serikali inadanganya umma inaona watu wote wajinga.

Utafiti gani alioufanya Mhe. Nape unasema saa 4 usiku ndiyo kuna watazamaji wengi ? na ukitaka kujua muda wa usiku saa 4 sio prime time kama ilivyo asubuhi huwezi ukakuta movies au tamthilia, unakuta tamthilia kwa sababu tamthilia sio za kila mtu anatazama.Jana amefanya PRESS saa 3 usiku kwanini asingefanya saa 4, kwa kile alichokisema ilibidi PRESS yake afanye saa 4 usiku, lakini alijua saa 4 usiku sio muda watu wengi wanatazama TV.

Mhe. Nape alisema kunatafiti za mabunge mbalimbali lakini hizo nchi zina channels maalum kwa ajili ya bunge muda wote, lakini kwanini uige nchi nyingine kwa kuficha maovu yako, kwanini asituambie Uingereza kuna uhuru mkubwa wa vyombo vya habari, vyombo vya habari havifungiwi hovyo? Tuige na hilo.

Kwanini asituambie kuna nchi kama Kenya na Congo matokeo ya Urais yanaweza kupingwa mahakamani ? na wao wakaiga tukayapinga matokeo ya Urais mahakamani , kwanini wasiige kwenye nchi za wenzetu kuna uwajibikaji na utawala bora? Nchi hii ukiona jambo linaigwa nje ujue linamaslahi yao.

Lakini na sisi tutakuwa wa kuiga mpaka lini? Kwanini sisi siku moja tusiwe mfano, kwamba Tanzania bunge linaonyeshwa moja kwa moja ili wengine waige, zinakuja whatsapp, face book, twitter, instagram zote hizi zinaletwa ili kupashana habari kwa urahisi zaidi, lakini unataka urudishe watu enzi hizo, haiwezekani kabisa, mambo yamebadilika.

Vyombo vinavyoshughulika na sekta ya habari kikiwemo MOAT, MCT e.t.c kuliangalia hili ili kuhakikisha haki ya watu kupata taarifa haiguswi, watafute ni jinsi haki ya kupata habari haiguswi, bunge lionyeshwe au taifal ipate TV maalum irushe matangazo,hatuwezi kulirudisha taifa nyuma.


Sababu za gharama, watu hawatafanya kazi haipo, haiwezekani mtu aache kazi yake aangalie TV, kwa ofisi gani za serikali saa 10 jioni ndio kazi zinachanganya? Au waziondoe TV ili wenye majukumu wafanye kazi, waacche uongo, kama sababu ni fedha waseme wadau wapo, bunge halionyeshwi siku 365 na siku nzima asubuhi mpaka jioni.

Post a Comment

 
Top