Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) imesema imeongeza muda wa usajili wa Pikipiki
ha
di februari Mosi mwaka 2016.
Hayo
yamesemwa leo na Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Alphayo Kidata alipokuwa
akizungumza na waandishi wa Habari katika kikao chake cha kutoa taarifa kwa
umma juu ya ukusanyaji wa kodi. Kaimu Kamishna Mkuu amesema wameamua kuongeza
muda wa zoezi hilo ili kuwapa nafasi wale ambao bado hawajasajili.
“ Natoa
wito kwa wamiliki wa pikipiki kusajili vyombo vyao mapema ili wasipatwe
na adha itakayojitokeza baada ya muda uliotolewa kumalizika ” Alisema Kaimu
Kamishna Kidata.
Ameongeza
kuwa zoezi hilo lilikumbwa na changamoto kadhaa zilizowalazimu kuongeza muda
mara mbili, ambazo ni umbali wa vituo vya usajili na makazi ya wamiliki wa
pikipiki hasa mikoani,pamoja na upotevu wa nyaraka za kununulia pikipiki.
Aidha
Kaimu Kamishna Alphayo Kidata ameomba wananchi kushirikiana na
Mamlaka ili kutimiza azimio la Serikali ya Awamu ya Tano ya kulijenga
taifa kwa kufanya kazi na hasa kulipa kodi stahiki zinazoleta mapato
yanayowezesha maendeleo katika taifa letu.
Zoezi la
usajili wa pikipiki lilianzishwa kwa lengo la kurahisisha ukusanyaji wa mapato
kutoka katika vyombo hivyo na lilipangwa kukamilika tangu Desemba 31, 2015
lakini ikaonekana wengi hawakusajili pikipiki zao hivyo basi Mamlaka imetoa
mwezi mmoja mpaka Februari Mosi 2016
Source mwananchi
Post a Comment