Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir kwa
mara ya kwanza amewaomba radhi raia wa nchi hiyo kutokana na mateso
na dhiki
ambayo wamepitia wakati wa mzozo wa kisiasa uliodumu miaka miwili.
Bw Kiir amesema kuomba msamaha ndiyo hatua ya kwanza katika
kufanikisha maridhiano nchini humo.
Amechukua hatua hiyo wakati wa kufungua rasmi mkutano mkuu wa
chama tawala cha SPLM.
Kutoelewana katika mkutano sawa mwaka 2013 kulitangulia jariibo
la mapinduzi ya serikali nchini humo na mapigano yaliyodumu miezi mingi.
Mkataba wa Amani ulitiwa saini mwezi Agosti mwaka jana mjini
Addis Ababa, ingawa Rais Kiir alitia saini mkataba huo shingo upande.
Jana, pande zilizohusika katika mzozo huo ziliafikiana kuhusu
kugawana nyadhifa za uwaziri katika baraza la mawaziri la serikali ya umoja.
“Hebu niwaambie, wenzangu, kwamba mimi, kama Mkristo, imenibidi
kujitafakari jambo ambalo ni hatua kuu kwetu sote kama taifa moja na kufikia
uwiano na umoja,” alisema Bw Kiir.
source BBC
Post a Comment