Ama kweli nimeamini kiongozi dhaifu watumishi dhaifu leo
mawaziri watatu wakutana katika machimjio Vingunguti
mawaziri hao ni Mwigulu Nchemba (Kilimo,
Mifugo na Uvuvi), Dk Hamisi Kigwangalla (Afya), na George Simbachawene (Ofisi
ya Rais-Tamisemi) na kutoa maamuzi m
agumu kutokana na kukithiri kwa uchafu,
ubadhilifu wa makusanyo ya fedha za ushuru. Ziara hiyo ilikuwa ni dakika 45 tu
lakini walijua ushuru ni malipo ya Sh11,000 kwa ng’ombe mmoja, fedha ambazo
hulipwa mnada wa Pungu (sh6,000) na Vingunguti (Sh5,000).
Catherine Severine, ambaye ni mchuuzi aliyekuwa
zamu usiku wa Desemba 24 mwaka jana, aliwaambia mawaziri hao kuwa kumekuwepo udanganyifu
wa utoaji wa vibali kwenye mnada wa Pugu. Alidai kuwa siku hiyo walifikishwa
mbuzi 1,407 huku wenye vibali wakiwa 300 , ng’ombe 700 lakini wenye vibali
halali 492, hivyo kwa hesabu za haraka, zaidi ya Sh3.4 milioni zilipotea.
Alisema kwa ujumla wanatakiwa wakusanye kiasi cha
Sh75 milioni kwa mwezi, lakini walikuwa wanakusanya Sh18 milioni huku Sh55
milioni zikiingia mifukoni mwa wajanja.
Simbachawene alimpa siku tatu mkurugenzi wa
Manispaa ya Ilala kuwaondoa wale wote waliokaa muda mrefu katika eneo hilo na
kujimilikisha kila kitu.
“Kigwangalla naomba usitufungie, Jumanne nitataka
kupata maelezo ya waliohusika na haya mabanda. Si kweli kwamba yamegharimu
Sh100 milioni. Hadi Jumatatu umeme uwe umerudishwa kwenye hayo mabanda,
yatumike ili kupunguza mbanano,” aliagiza Simbachawene.
Mwigulu aliwataka wote waliokuwepo mnadani
Desemba 24, kufika kwa katibu mkuu wa Wizara Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Jumatatu
na kuanzia leo waanze kutafuta kazi ya kufanya kwa sababu ya kujumlisha ng’ombe
na mbuzi imewashinda.
Mwigulu alisema hayo baada ya juzi usiku kukuta
machinjio ya Vingunguti kuna vibali 300 vya mbuzi, lakini kukiwa na mbuzi zaidi
1,000 na ng’ombe zaidi ya 200 hawakuwa na vibali, kitu alichosema kinaashiria
wanafanya makusudi siyo kwamba hawajui kujumlisha.
“Kuanzia sasa vibali vyote vya wanyama
wanaotakiwa kuchinjwa hapa, vitolewe kwenye mnada wa Pugu, huku wakusanya
ushuru wa Serikali Kuu na Halmashauri watakusanya hapa katika machinjio ya
Vingunguti. Mnaolipia ushuru hakikisheni mnaondoka na risiti, lango la
kuingizia ng’ombe lijengwe mara moja hata matatu, manne tena kwa fedha
inayopatikana hapa hapa machinjioni,” alisema Mwigulu huku akishangiliwa.
Kigwangalla alisema anakubali ombi la
Simbachawene la kutaka wasifungiwe kwa muda na watavamia wakati wowote kukagua
maagizo waliyotoa kama yanafanyiwa kazi.
Alisema mambo aliyoyaona akiwa katika Kamati ya
Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa miaka miwili iliyopita ndiyo
aliyoyakuta jana , hivyo hatawavumilia wanaohusika.
Post a Comment