SHIRIKA
la Viwango Tanzania (TBS) limedhibitisha ile kauli kwamba akutukane akuchagulii
tusi ni baada ya Marekani kutupa bid
hha feki ambazo ni msaada ambapo imepelekea
Tbs kuziteketeza kwa moto misaada hiyo ilitolewa Wilaya ya Tarime bidhaa izo
azifai hata kidogo kwa matumizi ya binadamu, bidhaa zenyewe ni kama nepi ambazo
zimkwisha muda wake wa matumizi
Akizungumza
baada ya bidhaa hizo kuteketezwa katika dampo la Pugu Kinyamwezi nje kidogo ya
Jiji la Dar es Salaam, Msemaji wa TBS, Roida Andusamile amesema bidhaa zote
zina thamani ya Sh 20 milioni.
Kwa mujibu wa Andusamile, wakati bidhaa zilizoingizwa kwa ajili
ya Halmashauri ya Tarime zililetwa zitolewe msaada kwa wahitaji kwenye eneo
hilo, na nepi ziliingizwa nchini kwa ajili ya kuuzwa.
Ameitaja kampuni iliyoingiza nepi hizo kutoka China kuwa ni
Chaoming & Xlambin Chen, iliyolenga kuzisambaza katika soko la ndani na kwa
faida.
Andusamile amesema, “kwa kawaida bidhaa mbalimbali zinapoingizwa
nchini kutoka nje kwa ajili ya biashara, kupitia katika mipaka yetu, bandari na
viwanja vyetu vya ndege hukaguliwa na maofisa wa udhibiti ubora kutoka TBS, ili
kujiridhisha endapo zinafaa kwa matumizi au la.”
Amesema baada ya kukagua mizigo hiyo katika Bandari ya Dar es
Salaam na kupima sampuli kwenye maabara husika za shirika hilo, ulibainika
upungufu kadhaa, ikiwemo kwisha kwa muda wa matumizi.
Ofisa Udhibiti Ubora wa TBS, Salome Emmanuel ameeleza kuwa,
mbali ya muda wa matumizi ya nepi hizo, vipimo vya sampuli za bidhaa hiyo
vilionesha kuwa hazifai kutumiwa kwa kuvalishwa watoto kutokana na kuwa na
madhara kwa afya zao.
Bidhaa za msaada ambazo watu wa Marekani wanaelezwa kuchanga ili
kusaidia wahitaji Tarime, ambazo hata hivyo ziliteketezwa ni losheni za watoto,
sabuni za maji kwa ajili ya kunawa mikono, dawa za meno aina ya Colgatte na
Crest.
Nyingine ni dawa za kusukutua mdomo ili usinuke, sabuni za
kuoshea nywele pamoja na sabuni za maji za kuogea.
Imeelezwa kuwa bidhaa hizo zilibainika mwishoni mwa mwaka jana,
na kwamba zilizoingizwa kibiashara ziliteketezwa kwa gharama za kampuni
iliyoagiza huku za msaada zikiteketezwa na TBS.
Post a Comment