Lukuvi atimiza ahadi ya Rais John Magufuli ya
kumaliza mgogoro wa ardhi baina ya
wananchi wa Kapunga na mwekezaji wa Kapunga Rice Project Limited na sasa hekta 1,780.
wananchi wa Kapunga na mwekezaji wa Kapunga Rice Project Limited na sasa hekta 1,780.
Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alitangaza jana katika mkutano wa
hadhara ambao licha ya mvua kubwa, wananchi walimsikiliza kwa makini na
kushangilia baada ya kupokea taarifa hiyo. Kijiji cha Kapunga kina wananchi
4,500.
Lukuvi alisema hatua hiyo
ni zawadi ya kwanza ya Rais kwa wananchi Tanzania kwa kutatua mgogoro wa siku
nyingi.
“Rais amedhamiria
kuwasaidia wananchi, hivyo naomba (Mkuu wa Mkoa), uandae orodha ya watu wote
wanaomiliki mashamba yasiyoendelezwa ingawa wanapata mikopo kupitia hati za
mashamba hayo ili kazi ya Serikali kuwapatia maeneo ya kulima na wananchi wa
kawaida iweze kufanikiwa,” alisema.
Lukuvi alikwenda kwenye
kijiji hicho kutangaza jambo ambalo aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, Profesa
Anna Tibaijuka alilishindwa Januari 7, 2013.
Meneja wa Mradi Kapunga
Rice Project, Sumil Tayic alisema viongozi wake wameafiki uamuzi wa Rais bila
kinyongo na sasa wataimarisha ushirikiano mzuri na wananchi.
Mwakilishi wa wananchi,
Sekela Sandube aliishukuru Serikali hususan Rais Magufuli na Waziri Lukuvi kwa
kumaliza mgogoro ambao uliwashinda wengi kwa sababu za roho mbaya.
Mwenyekiti wa Kijiji cha
Kapunga, Brighton Mwinuka alisema hatua ya Rais Magufuli kuwapatia eneo hilo
kutakifanya kijiji kiwe na mipango ya maendeleo.
Kabla ya kwenda wilayani
Mbarali jana, Lukuvi alikutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya
kuanzia saa 2.24 hadi saa 3.57 kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Habari kutoka kwenye
kikao hicho zilisema waziri aliwaeleza kinagaubaga kuhusu msimamo wa Serikali
ya Awamu ya Tano katika kutatua kero za wananchi na kwamba lazima viongozi wote
wabadilike kiutendaji.
Alipoulizwa kilichozungumzwa
Waziri Lukuvi alisema yalizungumzwa mambo mengi ya kiutendaji na baadhi
angeyatoa Kapunga.
Mgogoro wa Kapunga
Mwaka 1995, wanakijiji
walitoa hekta 5,500 za ardhi kwa Kampuni ya Taifa ya Kilimo (Nafco), huku eneo
la hekta 1,870 likiwa la wakulima wa kawaida.
Lakini katika mazingira
ya kutatanisha, Serikali ilichukua hati moja iliyojumuisha hekta 5,500 na
nyingine 1,870 bila kuwajulisha wananchi, hivyo mwekezaji aliponunua eneo la
Nafco alikabidhiwa hati ya eneo lote.
Serikali ilibaini kwamba
Nafco ilisajili na kupata hati moja kwa eneo lote likiwamo la kijiji lakini kwa
miaka yote imeshindwa kutoa uamuzi.
Mwaka 2013, mwekezaji
huyo alidaiwa kumwaga sumu kwenye mashamba ya mpunga yaliyokuwa na mgogoro na
Serikali ilimtuma Profesa Tibaijuka kuulimaliza.
Alifika akiwa na msimamo
wa kutaka kumshauri Rais wa Awamu ya Nne afute hati ya eneo linalozidi ambalo
ni hekta 1,870, lakini baada ya kupata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji,
Justin Vermaak alisema anawashangaa wananchi kudai kwa nguvu eneo ambalo ni la
mwekezaji kisheria.
“Baada ya kuzunguka nimeona
mwekezaji hana matatizo, chanzo cha mgogoro ni Serikali, hivyo itaendelea
kuzungumza na mwekezaji na wananchi ili kumaliza mgogoro,”
Post a Comment