MBUNGE wa Nzega Mjini kwa tiketi
ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hussein Mohammed Bashe amejitokeza hadharani
na ku
mtaka Waziri wa Zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Bernard Membe kuacha kulipotosha taifa kutokana kauli zake juu ya utendaji wa
Rais John Magufuli.
Hivi karibuni, Membe alikosoa hatua
mbalimbali zilizochukuliwa na Rais Magufuli. Pia, alipinga hatua ya kutangaza
kurudiwa kwa uchaguzi wa Zanzibar.
==>Kupitia ukurasa wake wa facebook,
Bashe ameandika;
Membe Amuache Ndg Magufuli Afanye kazi.
Membe amekua waziri for ten yrs ametimiza
wajibu wake amuache Ndg Magufuli atimize wajibu wake. Aliomba Urais Hajateuliwa
asubiri 2020 or 2025 ili akipita aanzishe uvasko dagama tena.
Hoja kuwa serekali haijapungua ama kubwa au
ndogo ama hoja kuwa Safari za nje nimuhimu na Rais amekosea kufuta ama
kupunguza ni hoja ya mwanasiasa muflisi .
Membe amekua sehemu ya mfumo dhaifu
ulotufikisha hapa kama Taifa,amefaidika na safari za nje yeye binafsi bila
manufaa kwa nchi,.
Membe akumbuke kila Rais ana Vission yake
.Magufuli anaamini matatizo ya Taifa letu yatamalizwa na sisi wenyewe kwa
kudhibiti matumizi ya hovyo na yasiyoyalazima na si kwa safari za Ulaya nakuendeleza
Tabia ya Kuwa Omba omba.
Ni muhimu membe afahamu Magufuli ana style
yake ,tutampima kwa matokeo as of now hatujaona athari za safari.Membe kama
yeye binafsi anatakiwa aseme kufutwa safari kulimuathiri yeye binafsi kwa
kukosa nafasi ya Ukatibu mkuu wa Commonwealth thats why leo anakosoa.
Tunafaham maamuzi mengi ya Magufuli kwa sasa
hayatafurahisha wengi walofaidika na Miradi kama NIDA Pesa za
Gadafi, walofaidika na Matumizi Mabaya ya Madaraka katika Awamu ya
nne, Majipu mengi yanayosubiri Kutumbuliwa ama yaliyotumbuliwa yatafanya
jitihada kukosoa muelekeo wa Serekali ya awamu ya Tano.
Hoja ya kutokua na mabalozi magufuli hana
siku 100 yeye amekua waziri wa mambo ya nje for 8 yrs hakuona umuhimu wakati
huo? Kuwa na balozi kwenye nchi ni jambo Mtambuka na hasa linatazamwa zaidi
kiuchumi na kisiasa .
Amekua mmoja wa mawaziri walioua foreign
relation yetu wakati wake kumekua na malalamiko mengi juu ya mis use of funds
katika wizara yake, kipindi chake Bernad Membe safari za nje walisafirishwa
ma girlfirend kwa kutumia Pesa za Umma.
Nimuhimu membe aheshimu Vission ya Magufuli
na style yake inafahamika ameathirika directly or Indirect na mchakato wa
Majipu na kufunga safari za nje.
Binafsi kama mbunge naunga mkono style ya
Magufuli ya uongozi. Aliwahi kusema Sankara " You cannot carry
fundamental change without a certain amount of Madness"
Mabadiliko anayofanya sasa Ndg Magufuli
yanahitaji Roho Ngumu, wendawazimu kidogo, Kuungwa mkono na wananchi wa kawaida
kwani walofaidika na udhaifu wa awali watajitahidi kutaka kuzuia mabadiliko yoyote
ambayo yanamfaidisha aliekuwa akinyonywa hapo awali
Tutasikia watu wa aina ya Membe wengi kwakua
style ya Magufuli inaathiri mfumo wao wakuwanyonya wengi na wachache kufaidika.
Wassalaam.
Post a Comment