George
Simbachawene ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, ameagiza kuitwa
ofisini kwake kwa viongozi wa Manispaa ya Dodoma, Idara ya Elimu, ili wakatoe
maelezo
ya kwa nini wanachangisha michango.
Simbachawene
alitoa agizo hilo jana baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika ofisi hizo
na kukuta viongozi hao hawapo. Alitaka kujua kwa nini Shule ya Msingi Makulu
inaendelea kukusanya michango kutoka kwa wazazi.
Awali,
Waziri huyo alizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake aliokuwa
akiwafafanulia kuhusu fedha za elimu bure, lakini alikatisha mazungumzo hayo
baada ya swali la mwandishi aliyeuliza ni kwanini shule ya Makulu inaendelea
kuwachangisha michango wazazi.
Aliondoka
ofisini hapo akiongozana na baadhi ya maofisa wa wizara na kuelekea katika
shule hiyo kwa lengo la kwenda kuthibitisha alichoulizwa.
Alipofika,
alielezwa kuwa wamepatiwa kibali na ofisi ya Elimu, Manispaa ya Dodoma.
“Hili
halikubaliki hata kidogo, sisi tumetoa waraka Namba 6, 2015 kuzuia michango
halafu maofisa wa manispaa wanatoa maagizo mengine, twendeni kwao,” alisema
Simbachawene baada ya Mwalimu Mkuu, Janeth Justine kumuonyesha barua ya
kutakiwa achangishe.
Akitoa ufafanuzi
kuhusu fedha zilizopelekwa katika shuleni mbalimbali nchini, alikiri kuwa ni
kiasi kidogo, lakini alisisitiza kitumike kama ilivyoelekezwa.
Hata
hivyo, Mwalimu wa Justine alithibitisha wazazi kuagizwa wachangie huduma za
maji, umeme na mlinzi.
Kaimu
Katibu Mkuu Tamisemi, Benard Makali, aliagiza uongozi wa Manispaa ya Dodoma
kufika leo ofisini kwa waziri wakiwa na majibu ya kwanini wamepuuza maagizo
yaliyotolewa na Serikali.
source Mwananchi
Post a Comment