Mwanza zamu yao kuisoma namba baada ya dar sasa ni
zamu ya mwanza ayo ya mesemw na Mkuu wa Idara ya Mipango Miji, Hosiana
Kusiga
wakati akizungumza na waandishi wa habari, kuwa wameanza kutambua maeneo
yaliovamiwa, viwanja vya wazi, makaburi, masoko, shule na maeneo kwa ajili ya
matumizi ya umma.
Kusiga amesema hadi sasa wameshatambua maeneo 32 yaliyovamiwa
ambayo ni makaburi, masoko, shule, viwanja vya wazi, maeneo ya umma kama
viwanja vya mpira wa miguu.
Aliyataja maeneo ambayo yamevamiwa na watakayoanza nayo
kuyabomoa kuwa ni Nyegezi, Igoma, Nyakato, Mabatini, Mto Mirongo, Mkolani,
Kishiri, Luchelele (eneo la mradi), Bugando, Bugarika (viwanja vya mpira) na
shule ya sekondari Nyakurunduma.
Hata hivyo Kusiga amesema bado wanaendelea na kazi ya utambuzi
katika maeneo yanayosababisha mafuriko na milima hatarishi kama Mabatini na
Butimba ambayo wakati wa mvua husababisha mawe kuanguka na kudai kwamba ni
lazima watu waondoke.
Aidha amesema kuwa baada ya kubaini maeneo yote watatoa taarifa
kwa watu watakaokumbwa na zoezi hilo, ili waondoke wenyewe kama ni nyumba yake
aweze kuivunja katika utaratibu utakaomsaidia kupata baadhi ya vifaa
alivyotumia kwenye ujenzi kabla ya kuvunjiwa na Serikali.
Pia aliwataka wananchi kufikiria wataenda wapi kwani baada ya
kutambua maeneo yote wataingia katika vikao vya kamati ya mipango miji ili
kuwaelimisha madiwani nao wafahamu jinsi zoezi hilo litakavyo tekelezwa kwa
waliovamia maeneo ya wazi na kando mwa mito.
“Wahusika watapewa taarifa ya kuondoka maeneo hayo, nilazima
watu wafuate sheria kwani kujenga mjini bila ya kibali ni kosa, zoezi
hili totalisimamia kwa kufuata sheria,” amesema Kusiga.
Amesema wale wanaojenga bila mpangilio ni wale wanaouziwa
vipande vya ardhi, wanaamua kujenga bila ya kufuata utaratibu na kwamba ni
muhimu mtu wanapouziwa wafuate taratibu zitakazoweza kuruhusu ujenzi eneo hilo.
Post a Comment