0
Madiwani wa vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni wamemtetea Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Mhandisi Mussa Natty 7aliyesimamishwa kazi.
Mhandisi Natty alisimamishwa kazi kwa tuhuma za kushindwa kusiamia vyema mkataba wa ubinafsishaji wa ufukwe wa Coco Beach kwa diwani wa Mbagala Yusuf Manj pamoja na kutowasimamia ipasavyo watumishi wake na kupelekea ujenzi wa baadhi ya barabara za manispaa hiyo chini ya kiwango.
Katika utetezi wao, madiwani hao wameeleza kuwa Mhandisi Natty amewajibishwa kisiasa zaidi kwa kuwa wakati wa uingiaji wa mkataba wa Coco Beach yeye alikuwa bado hajawa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo.
Katika tamko lao, madiwani hao wameitaka serikali ya awamu ya tano kushughulikia mgogoro huo na kuangalia hatua za kisiasa zilizochukuliwa. Pia, waliahidi kuwa endapo watafanikiwa kushika manispaa hiyo watahakikisha maeneo yote ya umma yanakuwa katika hali salama na yanaufaidisha umma.
Mbali na tamko la madiwani hao, Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akiwa na diwani wa  kata ya Ubungo, Boniphace Jacob (Chadema), walionesha mikataba iliyoingiwa kati ya Manispaa ya Kinondoni na Yusuf Manji ambayo inaonesha kuwa wakati huo Natty hakuw Mkurugenzi wa manispaa hiyo. Walidai kuwa sababu zilizotumika ni za kisiasa kwakuwa mkugenzi huyo alitenda haki na kupelekea majimbo ya uchaguzi kuchukuliwa na Chadema.
“Kama kuna ufisadi umetokea hatutamtetea mtu na kama kuna mtu tunaona anaonewa hatutakaa kimya na hili la Natty tunamwomba Rais John Magufuli aunde tume ambayo haitawahusisha Tamisemi na wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Post a Comment

 
Top