Zaidi ya hekari 150 za Mahindi zimefyekwa na watu wanaodaiwa
kuwa ni askari wa idara ya maliasili wilayani Mbozi na kusababisha wananchi
zaidi ya 400 kuwa katika hatari ya kukumbwa na uhaba wa chakula mwaka
huu.
Wananchi wa vijiji vya Nambizo, Utambalila na Ipapa katika kata
ya Nambizo wilayani Mbozi ndio ambao wameathirika na zoezi hilo la ufekaji wa
Mahindi yao wakidaiwa kulima kwenye hifadhi ya msitu wa Isalalo, hali ambayo
imewafanya wananchi hao kuishi kwa hofu ya kukumbwa na baa la njaa.
Uongozi wa vijiji na kata ya Nambizo umelaani tukio hilo kwa
madai kuwa askari hao wamevamia kata hiyo na kufanya uharibifu wa mazao bila
kushirikisha uongozi wa serikali katika kata hiyo.
Mbunge wa jimbo la Mbozi, Pascal Haonga ametembelea eneo la
mashamba hayo na kujionea uharibifu mkubwa wa mazao na kusema kuwa yeye kama
mwakilishi wa wananchi hawezi kukaa kimya hivyo atachukua hatua ya kuwaona
viongozi wa juu serikalini kujua hatma ya wananchi hao.
Wilaya ya Mbozi ni miongozi mwa maeneo yanayozalisha Mahindi kwa
wingi na kuiuzia serikali kupitia wakala wa hifadhi ya chakula nchini kwa ajili
ya kuwasaidia watanzania katika maeneo mbalimbali nchini wanaopatwa na uhaba wa
chakula.
LAKINI KWANINI WASISUBILI WANANCHI WAVUNE NDIO WAPIGE MARUFUKU
Post a Comment