Mkuu wa wilaya Paul Makonda amshikisha adabu Saidi kubenea ambaye
ni mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya chadema hii ni baada ya kumfungulia mashika
katika mahakam ya kisuto jijini Dar Es salaam Kwenye mahakama hiyo, Makonda amefungua madai
matatu dhidi ya Kubenea ambayo ni lugha ya matusi, kuitwa mpumbavu, mjinga
pamoja na cheo cha kupewa.
Kubenea ameweka mawakili sita
katika kesi yake ambao ni Peter Kibatara, Rugemereza Nshara, Nyaronyo Kicheere,
Frederick Kihwelo, Teremia Ntobesya pamoja na Omary Msemwa.
Hata hivyo, Kubenea yupo nje
kwa dhamana, waliomdhamini ni Mbunge wa Viti Maalumu, Anatropia Theonest na
Mbunge wa Kinondoni, Maulidi Mtulia ambapo kila mmoja aliweka dhamana ya Sh.
300,000.
Kesi hiyo imefunguliwa ikiwa
ni siku moja baada ya Makonda kuagiza askari wa Jeshi la Polisi kumkamata
mbunge huyo kwa madai ya kushindwa kutii agizo lake kama Mkuu wa Wilaya.
Tukio la kukamatwa Kubeneo
lilitekelezwa jana jijini Dar es Salaam, baada ya viongozi hao kukutana katika
mgogoro wa wafanyakazi wa Kiwanda cha nguo cha Tooku Tanzania.
Kwenye mgogoro huo, Kubenea
alikuwa wa kwanza kufika ili kukutana na wafanyakazi hao na kuangalia namna ya
kutatua mgogoro wa wafanyakzi na viongozi wa kiwanda hicho.
Katika mgomo huo Kubenea,
alisikiliza kero za wafanyakazi ambao walikuwa wakivutana na menejimenti ya
kiwanda hicho na baada ya makubaliano yaliyohusisha pande mbili, walikubali
kuendelea na kazi.
Hata hivyo, wakati mbunge huyo
pamoja na viongozi wa kiwanda hicho wakiwa katikati ya mazungumzo, Makonda
aliwasili katika eneo hilo la kiwanda kilichopo ndani ya Mamkala ya Uwekezaji
EPZ, Mabibo External.
Baada ya kufika, Makonda
hakutaka kuhoji kuhusu kilichoendelea kwenye mgomo huo wa wafanyakazi na kutaka
kuanza upya kusikiliza malalamiko ya wafanyakazi licha ya Kubenea kuupatia
ufumbuzi kwa mazungumzo yaliyohusisha pande zote.
Kutokana na hatua hiyo, Kubenea
hakupinga hatua hiyo ingawa Makonda alipomaliza kuzungumza na wafanyakazi wa
kiwanda hicho, alifunga mkutano bila kuruhusu hoja yoyote kutoka kwa mbunge
huyo.
Hali hiyo ilimfanya Kubenea
kuhoji sababu ya kutopewa nafasi ya kuzungumza wakati ndiye alikuwa wa kwanza
kufika katika eneo la tukio saa nne asubuhi na kulimaliza suala hilo.
Pamoja na hali hiyo Makonda,
alipinga hoja ya Kubenea kuzungumza na wafanyakazi hao na kusema kwamba tayari
amekwisha kufunga mkutano, hivyo haruhusiwi mtu mwingine kuzungumza kwa kuwa
ndiye alikuwa mzungumzaji wa mwisho na tayari alikuwa amefunga.
Hatua hiyo ilizua mabishano
makali baina ya Kubenea na Makonda kwa kila mmoja kusimamia kile anachokiamini.
Wakati hayo yakiendelea,
Kubenea aliendelea kuwasihi wafanyakazi hao watulie, lakini Makonda akasisitiza
hatozungumza hali iliyosababisha polisi waliokuwapo katika eneo hilo na baadhi
ya viongozi wa kiwanda kuingilia kati kusuluhisha mzozo huo.
“Huwezi kufunga mkutano
nisiongee na wafanyakazi ambao ni wapiga kura wangu, nimekuja hapa tangu
asubuhi nimepambana hadi tukafikia hapa na niliwaahidi nikitoka kwenye kikao
cha utawala nitawapa mrejesho (yaliyojiri).
“Inakuwaje wewe umekuja sasa
hivi unazungumza na kufunga mkutano kwa ubabe?,” alihoji Kubenea huku Makonda
akiendelea kusimamia msimamo wake kwamba tayari amefunga mkutano.
“…mimi hawa wamenipigia kura,
wewe umepata kura ngapi, huwezi kunifanya lolote wewe,” alisema Kubenea. Baada
ya mabishano hayo, Makonda aliamuru Kubenea akamatwe pamoja na kuamuru
mwandishi wa Kituo cha Televisheni cha Star TV kunyang’anywa kamera yake.
Polisi walimtaka Kubenea
kupanda kwenye gari lao la polisi (Defender) lakini kukatokea mabishano makali,
kwani Kubenea alipinga kupanda gari lao umuazi waliokukubali na hatimaye askari
wawili wenye silaha na mmoja ambaye hakuwa na silaha waliingia kwenye gari la
mbunge huyo hadi Kituo cha Polisi cha Magomeni.
Post a Comment