JAJI Mkuu na Mwanasheria Mkuu
Mstaafu, Mark Boman amesema kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja
Zanzibar, Maalim Seif Hamad akubali uchaguzi urudiwe Zanzibar kwani kama
alishinda atashinda tena kutokana na waliompigia katika uchaguzi ulifutwa
watampIgia kura tena
.
Boman ameyasema hayo leo jijini
Dar eS Salaam , wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa Maalim
kujitangazia kuwa ameshinda ni suala ambalo halikufuata utaratibu hivyo
kutokana na mazingira hayo uchaguzi ufanyike ili kupata Rais wa Serikali ya
Zanzibar.
“Kurudia uchaguzi Zanzibar ni
jambo lisilo epukika lakini wakae na kuangalia dosari zilizojitokeza na kufuta
uchaguzi lazima lishughukiwe kisheria bila kufanya hivyo kunaweza kuleta
matatizo”amesema Jaji Mstaafu, Boman.
Amesema kuwa uchaguzi uliofanyika Zanzibar
walitakiwa kukaa na kuona wapi walikosea katika kuondoa changamoto hizo ambapo
ilikuwa ngumu kutokana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salum
Jecha na wajumbe walishindwa kuafikiana.
Hata hivyo Boman ametaka suala la
katiba lazima lishughulikiwe kuacha kwake ni aibu ya nchi kutokana na mabilioni
ya fedha yametumika katika mchakato huo.
Amesema kuwa migogoro inayotokea
ya ardhi na wafugaji pamoja wakulima inatokana na kutokuwa na katiba ambayo
ndio ingekuwa suluhu ya utatuzi wa migogoro hiyo.
Post a Comment