Dk
Shein alimweleza Rais Dk Magufuli kuwa utatuzi wa mgogoro chini ya kamati
maalumu iliyopo chini yake, unaendelea vizur
i.
Kamati
hiyo iliyoanza kazi mapema Novemba 9, inawajumuisha pia Makamu wa Kwanza wa
Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Idd, Rais Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu Jakaya
Kikwete, marais wastaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume na Dk Salmin Amour.
Dk
Shein alisema kuwa mazungumzo aliyofanya na Rais Magufuli yalilenga kumweleza
hatma ya Zanzibar baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25.
Uchaguzi
huo uliingia doa baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha
Salim Jecha kutangaza kuufuta Oktoba 28 kutokana na kuvunjwa sheria na kanuni
za uchaguzi visiwani humo.
Mgogoro
huo uliodumu kwa takriban miezi miwili sasa unazidi kutengeneza sintofahamu
visiwani humo ambako watu wake wamekuwa watulivu kipindi chote, kuliko miaka ya
nyuma huku wakisubiri utatuzi.
“Kwa
hiyo nimekuja kumpa taarifa mheshimiwa Rais Magufuli kuhusu maendeleo ya
mazungumzo yetu ili aweze kujua kinachoendelea akiwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ambayo Zanzibar ni sehemu yake, na sisi ni jukumu letu
kumpa taarifa hiyo,” alisema Dk Shein.
Mara
baada ya kupata muafaka, Dk Shein alisema kamati yake itatoa mrejesho kwa
wananchi makubaliano hayo ambayo yamekuwa yakisubiriwa kwa muda, baada ya miezi
miwili kupita bila kupatikana ufumbuzi wa kina.
Mazungumzo
hayo ya jana yalifanyika zikiwa ni siku tano baada ya Maalim Seif kuteta na
Rais Magufuli juu ya kutafuta suluhisho la mkwamo huo wa kisiasa.
Katika
mazungumzo hayo ya Jumatatu, Rais alimwakikishia Maalim Seif kuwa Serikali
itadumisha amani na utulivu visiwani humo.
Maalim
Seif awali alikutana na Rais Jakaya Kikwete kabla ya hajamaliza muda wake
Novemba, 5 na kufanya mazungumzo ambayo yaliweka mwelekeo mzuri wa kutafuta
suluhu.
Mgogoro
wa Zanzibar umezidi kuibua mashinikizo kutoka katika jumuiya za ndani na
kimataifa kwa takriban miezi miwili sasa, wakitaka matakwa ya wananchi
yasikilizwe. Tayari madhara ya shinikizo la kumaliza mgogoro huo yameanza
kuonekana baada ya Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Changamoto za
Milenia (MCC) la Marekani kuahirisha kutoa msaa wa Dola 472 milioni za Marekani
(Sh992 bilioni) hadi hapo suluhu itakapopatikana.
Hata
hivyo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga alisema hivi karibuni kuwa kinachoendelea
Zanzibar kisiwe kigezo cha Jumuiya ya Kimataifa kudharau mafanikio ya
kidemokrasia yaliyofikiwa nchini.
Aliitaka
jumuiya hiyo kutambua utofauti wa siasa uliopo kati ya visiwani na bara na
kwamba waendelee kuvuta subira wakati ya usuluhishi inaendelea kutatua mgogoro
huo.
MIMI NAULIZA TU KUHUSU NEUTRALITY YA HIYO KAMATI!...HII KAMATI HII IMEZINGATIA UWAKILISHI BALANCED KWA UPANDE WA UPINZANI??...."Kamati hiyo iliyoanza kazi mapema Novemba 9, inawajumuisha pia Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Rais Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, marais wastaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume na Dk Salmin Amour."....WAPINZANI WAMEPEWA UWAKILISHI UNAOLINGANA HUMU??
ReplyDelete