Leo dodoma wamekwama nakusababisha watu kupata mseto wa
ghafla kiongozi aliyezuia safari hiyo,
Suzo Kazimoto, amesema uongozi wa TRL umemalizika kuzuia kuendelea kwa safari
ya abiria hao kutokana kuelezwa mapema kuwa hu
ko waliko kuwa wakielekea
kumetokea ajali.
Amesema baada ya kupata taarifa ya
kuanguka treni hiyo wameona ni vema kuzuia katika kituo hicho kwa vile abiria
hao wangeweza kupata huduma zote za kijamii zinazohitajika baadala ya kuiruhusu
kwani huenda wangeenda kwamba katika eneo ambalo halina huduma hizo muhimu.
“Taarifa tulizonazo ni kwamba
mafundi wako kwenye eneo wanaendelea na kazi ya kurejesha na tumewatangazia
abiria wetu kuwa safari yao itaendelea kuanzia saa 12:00 jioni leo,” amesema
Kazimoto.
Akizungumzia malalamiko ya abiria
kwamba baadhi yao walikuwa hawana fedha za kujikimu, Kazimoto, amesema wakati
huo walikuwa wakikusanya idadi halali ya abiria wenye tiketi ili aweze kufanya
mawasiliano na Makao Makuu Dar es Salaam kwa ajili ya kupata kibali cha
kuwapatia abiria hao fedha ya kujikimu.
“Hata kama leo, ni nusu siku kwamba
benki zinafungwa mapema hilo siyo tatizo tutaangalia kilichopo ili tuweze kuwa
saidia abiria wetu,” amesema Kazimoto.
Awali baadhi ya abiria walilalamikia
uongozi wa Shirika hilo kushindwa kujenga njia mbili tangu walipokabidhiwa reli
hiyo na mkoloni kwani kama kungekuwa na njia mbili kama ilivyo katika nchi
nyingine safari yao ingeendelea bila mvutano kama huo.
mmoja wa abiria hao, Khadija Salum
ambaye alikuwa akielekea Kigoma huku akiwa na mtoto mdogo alikuwa akilia njaa baada
ya kuibiwa Sh. 70,000 ambazo zilikuwa ni kwa ajili ya kujikimu wakati wa safari
hiyo.
Pia, amesema kuwa baada ya kukwama
katika kituo hicho baadhi ya wafanya biashara walipandisha bei za bidhaa ghafla
hivyo kuwaongezea ugumu katika kumudu kununua bidhaa hizo ikiwemo maji ya
kunywa na chakula.
Post a Comment