0
[5:44PM, 12/13/2015] mimaz: ✏✏DARASA📝
HURU💉


Ukweli kuhusu uzazi wa mpango



Uzazi wa mpango ni nini?
Uzazi wa mpango ni maamuzi ya hiari ya mtu au wenza juu ya ni wakati gani waanze kuzaa, watoto wangapi wazae , wapishane kwa umri gani na lini waache kuzaa.


Kwa nini uzazi wa mpango ni muhimu?
Kipindi cha Ujauzito kinaweza kikawa ni hatari kwa mama na motto hususani kinamama wakipopata ujauzito katika umri mdogo sana/mkubwa, muda mfupi baada ya kujifungua au wakizaa watoto wengi. Asilimia kumi na saba 17% ya vifo vyote vya kinamama wa kitanzania kuanzia umri wa miaka 15-49 hutokea wakati wa ujauzito, wakati wanajifungua ndani ya kipindi cha miezi miwili baada ya kujifungua au kutoka kwa mimba (TDS ) . Vilevile mtoto mmoja kati ya watoto ishirini wa kitanzania hufariki dunia kabla ya kutimiza umri mwaka moja baada ya kuzaliwa. Njia mojawapo bora ya kuzuia vifo vya kinamama na watoto vitokanavyo na uzazi ni kuzuia mimba zisizopangwa/zisizotarajiwa na njia nzuri ya kujikinga na hili ni kutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango.

Nini hali halisi ya uzazi wa mpango Tanzania?
Ingawa kuna ongezeko la watu wanaotumia njia za kisasa za uzazi wa mpango lakini pia kuna ongezeko la watoto 5.4 wanaozaliwa kwa kila mwanamke mmoja. Utafiti unaonyesha wanawake wengi huzaa mapema ambapo asilimia ishirini na nane 28% huzaa katika umri wa miaka 18, asilimia hamsini na tano 55% umri wa miaka 20 na asilimia themanini na nane 88% umri wa miaka 25.
Tafiti hii inaonyesha kuna umuhimu wa kutoa elimu juu ya uzazi wa mpango kwa vijana, kwa watu ambao hawajaoa au kuolewa. Vilevile kuna ulazima wa kuwalenga pia wenza (wanaume).
Pia asilimia sabini 70% ya wanawake walioolewa wanatamani kuchelewa kupata watoto au kupanga idadi ya watoto watakaowazaa lakini ni asilimia ishirini na saba 27% ya wanawake hao hutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango. Ambapo asilimia
tano 5% hutumia njia za muda mrefu na njia za kudumu za uzazi wa mpango.

Uzazi wa mpango una faida gani?
Pamoja na kumuwezesha mama na mtoto kuwa na afya njema, uzazi wa mpango una faida nyingi kwa wanawake, wanaume, watoto, familia na jamii kwa ujumla:
• Unamsaidia mama kurudi katika hali yake ya zamani ambayo ilisumbuliwa na hali ya ujauzito, uchungu na kujifungua, mama atakuwa mwenye nguvu, afya nzuri na mchangamfu. Na pia atakuwa na muda mzuri wa kurudisha afya yake kabla ya kupata ujauzito mwingine.

• Unamuwezesha kuhudumia familia yake vizuri na kuwa na maisha bora. Utakuwa na muda, fedha na mahitaji muhimu kwa familia yako kama chakula, mavazi, elimu, mapenzi na huduma zote muhimu.
• Mama anapata muda wa kutosha wakujishughulisha na mambo mengine ya kiuchumi na kimaendeleo kwa ajili ya familia na jamii kwa ujumla.
[5:44PM, 12/13/2015] mimaz: • Mama na baba wanapata muda mzuri wa kujishughulisha zaidi na mambo na mahitaji yao binafsi.
• Unasaidia kukuza uchumi na maendeleo ya nchi.

Nani anapaswa kutumia uzazi wa mpango?
Yoyote mwenye umri wa kuzaa au anatarajia kufikia umri huo anapaswa kufikiria kuhusu uzazi wa mpango. Uzazi wa mpango ni muhimu kwa:
• Wanawake na wanaume
• Watu walioa na kuolewa au ambao hawajaoa wala kuolewa
• Watu wenye watoto au bado hawajapata watoto.



Ni wakati gani mtu atumie uzazi wa mpango?
Umri sahihi wa kuanza kutumia uzazi wa mpango ni kuanzia miaka ishirini (20) na thelathini na tano(35). Ujauzito ni hatari kwa mama na mtoto endapo mama
atajifungua chini ya umri wa miaka ishirini (20) au zaidi ya miaka thelathini na tano (35) vilevile ni hatari kwa mama atakaejifungua zaidi ya watoto wane au
hasipowapishanisha watoto. Wenza wanatakiwa kusubiri angalau miaka miwili kabla ya kupata mtoto mwingine pia wafikirie kutumia njia za kisasa za uzaziwa mpango wakati wote ambao hawajapanga kupata mtoto.


Njia za uzazi wa mpango ni zipi?
Kuna njia nyingi za uzazi wa mpango ambazo zinaweza kutumiwa na mtu au wenza waweze kusubiri, kuchelewesha, au kupunguza idadi ya watoto watakaowazaa. Zipo njia za mda mfupi, mda mrefu na za kudumu.

• Njia za muda mfupi:
Hizi ni njia za kisasa za uzazi wa mpango ambazo unaweza kuzibadilisha. Unaweza kupata ujauzito pindi utakapoacha kuzitumia. Njia hizi ni nzuri kwa mama
anayetaka kupata ujauzito baada ya miaka miwili baada ya kujifungua.
Nazo ni: -
Njia ya vichecheo
Njia hizi zina vichocheo ni sawa na vichocheo vya kawaida vilivyomo kwenye mwili wa mwanamke.

Njia ya vidonge
Vidonge hivi hutumiwa na wanawake kila siku.

Njia ya sindano
Mama huchoma sindano kila baada ya miezi mitatu (3). Njia ya dharura ya vidonge vya uzazi wa mpango Humezwa na mama ili kuzuwia kupata mimba kwa mama
aliyetenda ngono bila kutumia kinga yeyote. Hivi vinaweza kuzuwia mimba hadi siku tano baada ya kujamiana.

Njia za Kizuizi
Kondom za kike na kiume. Ni muhimu kutumia ipasavyo kila unapofanya ngono. Hii ni njia ya pekee ambayo pia inazuia maambukizi ya VVU na magonjwa ya zinaa.
[5:44PM, 12/13/2015] mimaz: Njia za asili
Kukosa hedhi kwa kunyonyesha mfululizo Hii ni njia ya asili ambayo inatokea kwa mwanamke anayenyonyesha na ni ya kuaminika zaidi wakati mama huyo bado hajaanza kuona siku zake za hedhi na ili hayo yote yatokee ni lazima mama awe anamnyonyesha mwanae mara kwa mara usiku na mchana na Mtoto awe na umri chini ya miezi sita (6).

Elimu ya kujua siku za hatari uzazi
Hii inawezekana ikiwa mama anaufahamu mzunguko wake mzima wa siku zake za hedhi na kujua ni zipi siku za hatari za kushika mimba. Yeye na mwenza wanatakiwa kuacha kabisa kufanya ngono siku hizo za hatari.

Kukojoa nje
Hii inafanywa na mwanamume wakati wa tendo la ndoa ambapo humwaga shahawa zake nje ya uke.

• Njia za muda mrefu:
Hizi ni njia ambazo pia zinaweza kurudiwa. Unaweza kupata ujauzito mara utakapoacha kuzitumia. Hizi ni nzuri ikiwa unataka kusubiri zaidi ya miaka miwili kabla ya kupata mtoto mwingine.
Njia ya vipandikizi
Hiki ni kijiti cha plastik anachowekewa mwanamke chini ya ngozi kwenye mkono wake kinaweza kuwa kimoja au viwili. Hivi huzuia mwanamke asipate ujauzito kwa muda kati ya miaka 3 hadi 5 kutegemea na aina ya vipandikizi alivyotumia.
Njia ya kitanzi
Ni kifaa kidogo chenye shaba na plastiki ambacho huwekwa kwenye mji wa mimba. Hichi hukuzuia usipate mimba mpaka miaka kumi na mbili (12), unaweza kukitoa wakati wowote utakapoamua au kuhitajia kupata mtoto.

• Njia ya kudumu:
Hizi ni njia huwezi kuzirudia na ukitumia huwezi kupata mtoto tena. Na hutumiwa na watu ambao hawataki kupata mtoto tena. Nazo ni: -
Kufunga kizazi kwa mwanaume
Njia hii inahusisha upasuaji mdogo ambapo mirija ya uzazi ya mwanaume ukatwa au kufungwa hivyo kuzuia yai kusafiri na kukutana na shahawa. Mwanaume anaendelea kuwa na hamu ya kujamiiana na kutoa mbegu lakini mbegu zake hazitaweza kutunga mimba

Kufunga kizazi kwa mwanamke
Njia hii inahusisha upasuaji mdogo inafanyika kwa kuziba au kukata mirija ya kizazi kuzuia yai kukutana na mbegu. Mwanaumke ataendelea kuwa na hamu ya kujamiiana na kuona siku zake za hedhi.

Utafahamu vipi kuwa njia gani ya uzazi wa mpango ni sahihi kwako?
Inategemea na mtu mwenyewe au wenza kuamua njia gani ni sahihi kwao. Tembelea kituo cha afya kilicho karibu nawe uonane na wahudumu wa afya wataweza kukufahamisha njia sahihi kwako. Pia unaweza kutuma
ujumbe mfupi M4RH kwenda 15014 BURE kwa maelezo zaidi.


Ni nini Madhara ya njia za uzazi wa mpango?
Njia za kisasa za uzazi wa mpango hazina madhara na zinafanya kazi vizuri zikitumiwa kwa ufasaha. Yafuatazo ni madhara madogo madogo ya njia za uzazi wa mpango ambayo ni ya kawaida na hayana madhara. Pia sio dalili ya maradhi. Mama wengine wanaweza kuona: -
• Mabadiliko ya siku za hedhi, Kutokwa na damu nyingi wakati wa siku za hedhi au damu kidogo au kukosa kabisa
• Maumivu ya kichwa
• Matiti kujaa
• Mabadiliko ya uzito
• Kizunguzungu
Madhara mengi yanapungua au kuisha ndani ya miezi michache baada ya kuanza kutumia njia za uzazi wa mpango. Ni wanawake wachache hupata matatizo baada ya kutumia njia za uzazi wa mpango. Ukipata matatizo yoyote nenda kituo cha Afya kilicho karibu nawe.

Vipi njia za uzazi wa mpango unaathiri uwezo wa
kupata mtoto
Njia za kisasa za uzazi wa mpango hazimfanyi mtu kuwa tasa. Njia kama kondom, vidonge, kitanzi na vipandikizi unapoviacha tu mwanamke anaweza kupata ujauzito. Inawezekana mwanamke kuchukua miezi michache kupata ujauzito kwa yule aliyetumia sindano. Hii ni hali ya kawaida na mwanamke hana haja ya kuwa na
wasiwasi.
Kuna njia mbili za kudumu za kufunga kizazi kwa mwanamke na kufunga kizazi kwa mwanaume ambazo hawataweza kupata mtoto tena. Hizi ni kwa wale ambao wameamua kutopata mtoto tena katika maisha yao. Ni vizuri ifahamike kuwa uzazi unapungua kadiri mwanamke anapoongezeka umri. Unaweza kwenda kwenye kituo cha afya kilichopo karibu nawe wakati wowote ikiwa una tatizo lolote, maswali au ikiwa unataka kubadilisha njia za kisasa za uzazi wa mpango.
[5:49PM, 12/13/2015] mimaz: HABARILEO

Makampuni 15 yaliyokwepa kodi baada ya kutorosha makontena yao, yamejisalimisha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), lakini yameshindwa kulipa kodi ndani ya siku saba za msamaha wa Rais John Magufuli.

Kodi inayodaiwa kwa kampuni hizo ni Sh bilioni 3.75, hivyo watachukuliwa hatua za kisheria kwa kukwepa kulipa kodi, ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.

Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, Dk Philip Mpango alisema hayo jana wakati akielezea makusanyo ya kodi ya makontena yaliyoondolewa katika bandari kavu ya Azam, kinyume cha sheria pamoja na kumalizika kwa siku saba alizotoa Rais Magufuli kwa wafanyabiashara hao kulipa kodi waliyokwepa, bila kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria.

Dk Mpango alisema siku hizo saba zimefikia kikomo juzi, hivyo hatua kali za kisheria kwa wafanyabiashara ambao hawakulipa kodi katika kipindi hicho zinafuata hivyo wasubiri cha moto.

“Tumewasihi waje kulipa kwani huruma ya Rais sasa imeisha… tulifanya uhakiki na kuthibitisha kuwa kampuni hizo zipo. Wamekuja kulalamika lakini hakika hakuna atakayesamehewa kulipa na sasa tunafuata mkondo wa sheria ili kuwafikisha mahakamani,” alisisitiza.

Wadaiwa Alitaja kampuni hizo kuwa ni Ahmed Saleh Tawred anayedaiwa Sh milioni 59.23; Cla Tokyo Limited Sh milioni 77.52; Farida Abdullah Salem Sh milioni 75.33 na Juma Kassem Abdul Sh milioni 190.18.

Wengine ni Libas Fashion Sh milioni 52.94; Rushy Wheel Tyre Center Co Ltd, Sh bilioni 1.8; Said Ahmad Hamdan Sh milioni 68.36; Said Ahmed Said Sh milioni 68.73 na Salum Continental Co Ltd Sh milioni 151.17. Pia yumo Salum Link Tyres Sh milioni 343.44; Simbo Yonah Kimaro, Sh milioni 69.22; Snow Leopard Building Material Co Ltd Sh milioni 93.97; Swaleh Mohamed Swaleh Sh milioni 34.68; Tybat Trading Co Limited, Sh milioni 598.69 na Nasir Saleh Mazrui Sh milioni 70.10.

Alisema mpaka kufikia jana TRA walikuwa wamekusanya Sh bilioni 10,643.004,948.46 kutoka kwa kampuni 28 ambapo kampuni 13 zimelipa kodi yote iliyokadiriwa, ambayo ni Sh 4,167,130,173.89 na Sh 2,303,637,554.57 kutoka kampuni 15 zilizolipa sehemu ya kodi iliyokadiriwa.

Dk Mpango alisema Sh bilioni 4.17 zimelipwa na kampuni ya Azam ICD, ikiwa ni dhamana ya kodi iliyokwepwa, hivyo atatakiwa kumaliza kulipa kodi yote inayodaiwa kwa mujibu wa nafasi yake kama mwenye dhamana.

Alisema wakati utekelezaji huo ukiendelea, ili kurahisisha ukusanyaji wa kodi hiyo ya makontena yaliyoondolewa bandarini kinyume cha sheria na taratibu za forodha, TRA imefungua akaunti maalumu katika Benki Kuu yenye namba 9921169785 inayoitwa Commissioner for Customs and Excise – Container Account.

Kwa mujibu wa Dk Mpango, mpaka sasa watumishi 36 wa TRA wanaotuhumiwa kushiriki katika upotevu wa kodi kutokana na makontena hayo kuondoshwa bandarini.

Watumishi wachongewa Aidha, alisema TRA imepata taarifa zisizopungua 15 kutoka kwa wananchi kuhusu mali za kifisadi na mwenendo mbaya wa baadhi ya watumishi na walipakodi wanaokwepa kodi. Aliwashukuru wananchi waliotoa taarifa na kuwaomba wengine wajitokeze kutoa taarifa zaidi na mamlaka hiyo inawahakikishia kuwa itawalinda.

Dk Mpango alisema wanaendelea kutekeleza maagizo ya Rais katika ukusanyaji wa mapato, ikiwa ni pamoja na kupiga picha makontena yote badala ya sampuli ya kontena ilivyo sasa na wanafanya utaratibu wa kupata mashine za kupiga picha za nyongeza.
[5:49PM, 12/13/2015] mimaz: HABARILEO

Wakati wapinzani wakipinga uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, waziri huyo amewasihi wananchi kumvumilia kidogo, ili baada ya muda mfupi atoe mpango wa maendeleo ya wizara hiyo, ambao pamoja na mambo mengine, utaelezea bei ya nishati hiyo itakavyoshuka.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo jana Ikulu jijini Dar es Salaam, Profesa Muhongo alisema mbali na mkakati wa kushusha bei ya umeme, kasi ya kusambaza umeme vijijini kupitia miradi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), itarejea palepale.

“Nimepokea uteuzi huo, kinachofuata ni kuwatumikia wananchi, niwaombe tu wanivumilie kidogo nitawapa mpango wangu wa maendeleo wa muda mfupi na mrefu, lakini nisisitize tu nishati sio siasa, ni suala la utaalamu, liachwe lifanywe kitaalamu,” alisema Profesa Muhongo.

Akizungumzia bei ya umeme na upatikanaji wake, Profesa Muhongo alisema kupunguza bei hiyo ni ajenda muhimu itakayozingatiwa na kusema ili umeme uwe wa uhakika, ni lazima kuwe na mipango ya kuwa na nishati hiyo ya uhakika ifikapo mwaka 2025.

“Umeme wa uhakika utapatikana na matarajio yetu ni Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 ambapo tunatarajia uzalishaji wa nishati hiyo ufike Megawati 10,000 hadi 15,000,” alisema Profesa Muhongo.

Alisisitiza kwamba wizara yake haitategemea chanzo kimoja cha nishati bali wataangalia vyanzo vingine ikiwemo nishati jadidifu, upepo, gesi, makaa ya mawe, maji huku akisema vyanzo hivyo vikitumika kuzalisha nishati, ni wazi bei ya umeme itashuka na kushusha gharama nyingine za maisha na za uwekezaji.

Aliongeza katika kuendeleza sekta ya nishati suala la uwekezaji ni muhimu hivyo wizara yake inakaribisha wawekezaji wenye sifa, watakaowekeza kwenye sekta hiyo ili kuja na matokeo bora zaidi, wananchi wanufaike na rasilimali za nchi yao.

Pamoja na nia yake hiyo kwa wananchi, Profesa Muhongo anakabiliwa na pingamizi kutoka kwa wanasiasa wa vyama vya upinzani, akiwemo Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) na aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.

Lissu na Profesa Lipumba, wamekaririwa wakikosoa uteuzi wa Profesa Muhongo kwa madai kuwa wizara aliyopewa kuiongoza, ilikumbwa na kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow wakati wa uongozi wake, ikasababisha ajiuzulu.

Hata hivyo, Profesa Lipumba na Lissu katika kukosoa huko, hawakutaka kutumia kumbukumbu zilizo wazi kuwa uchunguzi dhidi ya Profesa Muhongo, ulibaini kuwa hakukiuka maadili yoyote katika sakata la utoaji wa karibu Sh bilioni 300 zilizokuwa katika akaunti ya Tegeta Escrow, iliyokuwa Benki Kuu (BoT).

Matokeo ya uchunguzi huo yalitangazwa Mei mwaka huu na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, ambapo alisema Tume ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, ndiyo ilifanya uchunguzi kama Profesa Muhongo alistahili kwenda kwenye Baraza la Maadili kujibu mashitaka, lakini hawakuona tatizo lake na kufunga shauri lake.

Balozi Sefue aliweka wazi kuwa Profesa Muhongo alijiuzulu kwa sababu za kisiasa, lakini kimaadili hakuhusika kwa namna yoyote, kutokana na uchunguzi wa Sekretarieti ndiyo sababu hakufikishwa katika Baraza la Maadili.
[5:49PM, 12/13/2015] mimaz: HABARILEO

Wananchi katika majimbo ya Arusha Mjini na Handeni Mjini mkoani Tanga, watafanya uchaguzi wa wabunge wao leo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva, jijini Dar es Salaam.

Pia alisema wananchi wa Kata ya Mvomero mkoani Morogoro, nao watamchagua diwani leo. Wananchi wa majimbo hayo mawili na kata hiyo, hawakupiga kura katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Siku hiyo, uchaguzi uliahirishwa katika majimbo saba nchini, ikiwemo Arusha Mjini na Handeni Mjini, kata ya Mvomero na nyinginezo 34 nchini.

Tangu wakati huo hadi sasa, uchaguzi umeshafanyika katika baadhi ya majimbo na kata nchini.

Lubuva aliwaomba wananchi waliojiandikisha kama wapigakura katika majimbo na kata husika, kujitokeza leo kwenye vituo walikojiandikisha ili kupiga kura na kuwachagua na viongozi wanaowataka.

“Kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, nawapongeza wananchi wote katika majimbo na kata zinazofanya uchaguzi kutokana na utulivu waliouonesha katika kipindi chote cha kusubiri siku ya kupiga kura kuchagua wabunge aumadiwani wao,” alisema Jaji Lubuva.

Alisisitiza kwamba taratibu zilizotumika katika uchaguzi mkuu tarehe 25 Oktoba mwaka huu, ndizo hizo hizo zitakazotumika.

“Vituo vitafunguliwa saa 1:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 jioni. Iwapo wakati wa kufunga kituo watakuwepo wapiga kura katika mstari, ambao wamefika kabla ya wakati wa kufunga kituo na hawajapiga kura, hao wataruhusiwa kupiga kura. Mtu yeyote hataruhusiwa kujiunga katika mstari wa wapigakura baada ya saa kumi jioni”, alisema Jaji Lubuva.
[5:49PM, 12/13/2015] mimaz: HABARILEO

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amesema atafanya kazi kwa kasi ya Rais Magufuli katika kukabiliana na changamoto zilizopo katika wizara hiyo.

Amesema changamoto ziko nyingi kuanzia chini mpaka juu, katika Mahakama, magereza na kwingineko, hivyo aliomba apewe muda kuangalia hali ikoje ili abadilishe mifumo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

Akizungumzia suala la Katiba Mpya, alisema Rais alieleza vizuri kuwa litafanyiwa kazi, kwani halikuishia pabaya hivyo muda ukifika litakamilika.

Alisema watafanya kazi kubwa ili mfumo wa sheria usiwe pingamizi, bali uendeleze kasi aliyoanza nayo Rais Magufuli.

Nape Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye alisema atatengeneza utaratibu katika wizara hiyo, ili kuondoa utamaduni wa mtu mmoja kufanya mambo mengi peke yake na kuahidi kuwa msikivu na kutengeneza sheria, ili kila mmoja atimize wajibu.

Akizungumzia changamoto katika michezo, Nape alisema tatizo katika michezo ni usimamizi wa sheria na kutokuwa na nidhamu kwa kila mtu kufanya anavyotaka. Alisema zamani wanamichezo walikuwa wakifanikiwa kutokana na nidhamu, hivyo watasaidiana na wadau mbalimbali kurudisha nidhamu.

Manyanya na elimu ya juu Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Stella Manyanya, alisema kinachosubiriwa ni kasi ya kuleta mabadiliko kwa muda muafaka na jambo la msingi ni kazi na kila mtu ahakikishe anatimiza wajibu wake.

Alisema changomoto katika wizara hiyo ni nyingi, ikiwemo suala la mikopo ya elimu ya juu na kusisitiza kwamba wanafunzi wote wenye sifa ya kupata mikopo, wanapaswa kupewa kwa kuwa huo ni mkopo ambao wataurudisha.

Manyanya alisema wizara hiyo haitamvumilia mwalimu yeyote mzembe, atakayetumia muda wake vibaya kwa kutotimiza wajibu, kwa kuwa hatua zitakazochukuliwa ni kumfukuza kazi na sio kuhamishwa kituo cha kazi.

Mhagama, Kairuki Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama, alimshukuru Rais kutambua mchango wake katika Serikali iliyopita na kilichobaki ni kutimiza wajibu wao katika wadhifa huo.

“Rais katambua mchango wangu, nashukuru na sasa ni kuhakikisha nakwenda na kasi yake, ili tumsaidie kutimiza ndoto za wananchi na hasa kuondokana na tatizo la ajira,” alisema Mhagama.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki alisema anawiwa deni kubwa kuhakikisha anakwenda na kasi ya utendaji kazi ya Rais Magufuli.
[5:49PM, 12/13/2015] mimaz: MWANANCHI

Shirika la Umeme (TANESCO) wilayani Mwanga limepata hasara ya zaidi ya Sh151.2 milioni kwa kipindi cha miezi miwili kutokana na uharibifu wa miundombinu ya nishati hiyo.

Meneja wa Tanesco wa wilaya, Reinhild Malinjanga alisema jana kuwa hasara hiyo imetokana na matukio kumi na moja ya wizi yaliyotokea kati ya Novemba na Desemba.

Alisema mita 2,645 zimeibwa na kusababisha shirika hilo kupata hasara na kushindwa kutoa huduma bora kwa wateja. Mkuu wa wilaya, Shahib Ndemanga alisema hatawavumilia wala kuwafumbia macho watu watakaogundulika kujihusisha na wizi wa nyaya na nguzo za umeme.

Ndemanga alisema kwa kipindi alichofika wilayani hapo matukio hayo yamekuwa yakiongezeka ukilinganisha na miaka ya nyuma.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Fulgence Ngonyani alisema wanashikilia watu 28 wanaotuhumiwa kuhusika na wizi wa nyaya za umeme aina shaba wilayani Mwanga.

Kamanda Ngonyani alisema Desemba 8 walikamata mita 200 za nyaya za umeme zenye thamani ya Sh10.6 milioni na Desemba 9 walikamata mita 300 zenye thamani ya Sh 17.2 milioni.

MWANANCHI

Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza imeelezwa kukithiri kwa ukatili wa kijinsia, huku idadi kubwa ya watu wanaofanyiwa vitendo hivyo ni wanawake na watoto.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCu), Justin Bamanyisa alisema hayo jana wakati akitoa tathimini ya awali ya utafiti wa vitendo vya ukatili wilaya hapa.

Alisema utafiti huo unaonyesha kuwa asilimia 33 ya wanawake walio katika uhusiano wanafanyiwa vitendo hivyo.

“Nimefanya utafiti hasa vijijini na kubaini kwamba wanawake wanafanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia, lakini asilimia 21 ndiyo wanatoa taarifa katika vyombo vya dola, huku vitendo hivyo vikiwa vinatokea mara kwa mara,” alisema Bamanyisa.

Alisema kati ya watu waliowahojiwa wakati wa kufanya utafiti huo, asilimia 50 walisema wanaona ipo haja ya kuwasaidia waathirika wa vitendo vya ukatili wa kijinsia, huku asilimia 49 wakisema hakuna haja ya kuwasaidia watu hao.

“Kwa kweli hali ni mbaya, Misungwi kumekuwa na vitendo vya kikatili vingi ambavyo wanafanyiwa wanawake na watoto, tunaomba kila mmoja ajue ukatili ni dhambi,” alisema Bamanyisa.

Mratibu wa Afya wilayani hapa, Mery Joseph alisema wamekuwa wakipokea wasichana wa chini ya miaka 18 wakiwa na ujauzito. “Wanawake wenye zaidi ya miaka 20 ndiyo wanapaswa kuolewa, lakini sisi hapa tumekuwa tukipata changamoto ya kupata wasichana wa chini ya miaka 18 wakiwa na ujauzito,” alisema Joseph.

Katibu Tawala wa wilayani hapa, Elius Nyaka alisema vitendo hivyo havikubaliki na kwamba watalifuatilia suala hilo kuhakikisha wanatokomeza vitendo vya ukatili.

Mkurugenzi wa Shirika la kutetea haki za Wanawake (Kivulini), Yasin Ally alisema takwimu hizo zinatisha, kitaifa zinaonyesha utakili wa kijinsia Mwanza unafanyika kwa asilimia 43. “Hii hali inatisha, ipo haja ya kufunga mkanda na kupambana na vitendo vya ukatili.
[5:49PM, 12/13/2015] mimaz: MWANANCHI

Dalili za kufanyika kwa uchaguzi wa Rais wa Zanzibar na wawakilishi zinaonekana kuwa finyu kutokana na kutokuwapo maelekezo yoyote ya kuitaka Tume ya Uchaguzi (ZEC) kuanza kuuandaa.

Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salum Jecha alitangaza kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi huo Oktoba 28, akisema kulikuwapo na ukiukwaji mkubwa wa sheria na taratibu za uchaguzi na kuahidi kuwa ungeitishwa uchaguzi mpya ndani ya siku 90.

Zikiwa zimepita siku 44 tangu atangaze uamuzi huo, hakuna maelekezo yoyote kuhusu maandalizi ya uchaguzi huo kutoka ZEC, huku kukiwa hakuna taarifa rasmi za maendeleo ya vikao vinavyodaiwa kufanywa baina ya uongozi wa CCM na CUF, vyama vyenye upinzani mkali visiwani Zanzibar.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa ZEC, Salum Kassim Ali aliiambia Mwananchi jana kuwa hawajapata maagizo yoyote ya kutakiwa kuanza maandalizi ya uchaguzi.

Ingawa hakuwa tayati kuzungumzia suala hilo kwa kina, Kassim Ali alisema wakati akijibu maswali ya gazeti hili kuwa hakuna kinachoendelea hadi sasa.

“Wewe unauliza kununua pampasi wakati hujui mtoto atazaliwa lini? Badala ya kuuliza uchaguzi upo au haupo unauliza vitu vingine?” alihoji Kassim Ali alipoulizwa na gazeti hili uchaguzi wa marudio utafanyika lini”. alihoji.

Maalim Seif Sharrif Hamad alitangaza kuwa ameshinda uchaguzi huo na kuitaka ZEC imtangaze mshindi. Kitendo hicho pamoja na vurugu ambazo Jecha alidai zilifanyika ndani ya ZEC na wakati wa kuandikisha wapigakura, ndvyo vilivyomfanya atangaze kufuta uchaguzi, uamuzi ambao unapingwa na CUF inayodai kuwa mwenyekiti huyo hana mamlaka ya kufuta uchaguzi na kwamba alichukua uamuzi huo bila ya kushirikisha wajumbe wenzake.

Kuhusu taarifa kwamba Jecha amekuwa haonekani ofisini, mkurugenzi huyo wa uchaguzi wa ZEC alisema taarifa hizo si za kweli na kwamba kama kuna taarifa zimeenea kuhusu jambo hilo, ziandikwe hivyo hivyo. “Aliyekuambia hayupo ofisini ni nani? Andika hayo hayo ya mitaani,” alisema.

Akizungumzia suala hilo la tarehe ya uchaguzi wa marudio, ofisa uhusiano wa ZEC, Idrissa Jecha alisema kuwa Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar haizungumzii uchaguzi wa marudio bali tarehe ya kupiga kura baada ya wagombea kuteuliwa na Tume.

Post a Comment

 
Top