0

Katika hali isiyo kuwa ya kawaida Chama cha Demokrasia na Maendeleo mkoani Shinyanga leo kimedai kwamba Jeshi la Polisi mkoani humo limefanya maandamano ya Chadema bila kujijua.

Kwa mujibu wa baadhi ya viongozi wa chama hicho walidai kupokea taarifa kutoka kwa uongozi wa juu wa chama hicho ukiwataka kufanya maandamano leo nchi nzima  ya kupinga ushindi wa Dkt. John Pombe Magufuli kwa madai kuwa demokrasia imebakwa katika mchakato mzima wa uchaguzi  mkuu uliofanyika tarehe 25 oktoba 2015.

Katibu wa Chadema wilaya ya Shinyanga mjini George Kitalama amesema kwamba chama hicho kimefanikiwa kufanya maandamano kupitia  jeshi la polisi lililozunguka mji mzima kuwasaka wanachama wa chadema na kuambulia patupu.

“Tulipanga kufanya maandamano leo Novemba 03,2015 mji mzima wa Shinyanga lakini polisi ndiyo wamejitokeza kufanya maandamano wakiwa na magari yao kila mtaa.”Alisema Kitalama.

Kufuatia taarifa  ya Chadema kutaka  kufanya maandamano katika maeneo mbalimbali nchini Askari wa Jeshi la Polisi wamekuwa  katika misururu ya magari yakiwemo ya maji ya kuwasha wakizunguka kuwasaka waandamanaji kutoka chama hicho ambao hawakufanikiwa kufanya maandamano hayo.

Jijini Dares salaam Askari Polisi wakiwa kwenye punda na wengine wa doria wameonekana katika maeneo mbalimbali ikiwemo maeneo nyeti na yenye ofisi nyingi za Serikali ikiwemo Posta.

Post a Comment

 
Top