0


‪#‎ZanzibarYaamua2015‬. Muda mfupi uliopita, mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, ameitisha mkutano wa
waandishi wa habari na kusema kuwa baada ya chama chake kukusanya fomu zote za matokeo kutoka vituoni, yeye amepata kura 200,007 dhidi ya kura 178,363 za mgombea wa CCM anayetetea nafasi yake, Dk. Ali Mohammed Shein, na kuitaka Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kutangaza matokeo halisi kama yalivyo kwenye fomu zinazotoka vituoni. Mengi zaidi, sikiliza matangazo yetu ya leo mchana.

Source
DW (Kiswahili)
Media/News/Publishing369,577 Likes
1 hr

Post a Comment

 
Top