Mkazi wa mjini Moshi, Kyefa Joachim Makundi (33), jana alipandishwa kizimbani akikabiliwa na mashitaka ya kumtukana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete.
Mbali na shitaka hilo, mshitakiwa huyo alisomewa shitaka lingine la kumtukana Ridhiwan Kikwete ambaye ni mtoto wa Rais Kikwete ambaye pia ni Mbunge wa Chalinze anayemaliza muda wake.
Mshitakiwa huyo alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya mkoa Kilimanjaro, Joachim Tiganga na kusomewa mashitaka hayo na wakili wa Serikali Kanda ya Moshi, Agatha Pima.
Wakili Pima alidai mahakamani kuwa Oktoba 17 mwaka huu katika baa ya Harambee iliyopo katikati ya mji wa Moshi, mshitakiwa alitumia lugha ya matusi dhidi ya Rais Kikwete na mwanae Ridhiwan.
Ingawa matusi hayo hayakuandikwa kwenye hati ya mashitaka, lakini wakili Pima alidai kitendo hicho ni kinyume cha kifungu 89(1) (a) cha kanuni ya adhabu kama kilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002.
Chini ya kifungu hicho, mtu yeyote anayetumia lugha ya matusi, kuudhi, au kudhalilisha dhidi ya mtu mwingine katika hali ambayo inaweza kusababisha uvunjifu wa amani anatenda kosa la jinai.
Adhabu inayotolewa kwa mtu anayepatikana na hatia katika kosa hilo ni kifungo cha miezi sita jela.
Hata hivyo, mshitakiwa alikana shitaka hilo ambapo mahakama ilisema dhamana ilikuwa wazi ikiwa mshitakiwa atakuwa na wadhamini wawili watakaosaini hati ya dhamana ya Sh1.5 milioni kila mmoja.
Related Posts
VIONGOZI WA DINI WA WASHAMBULIA CHADEMA
Viongozi wa Dini nchini, wamesema Rais JOHN MAGUFULI Hajakataa kuzungumza wala kuwapuuza viongozi[...]
Sep 24, 2016KWA USHUJAA HUU CHADEMA WANATAKIWA KUIGWA
September 19, 2016 Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA jimbo la Temeke kimemfukuza uanachama[...]
Sep 24, 2016LIPUMBA APEWA WENYEKITI CUF
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amesema kuwa Prof. Ibrahim Lipumba bado[...]
Sep 24, 2016CUF WAJIBU BAADA YA LIPUMBA KUTANGAZWA KUWA MWENYEKITI
Baada ya kupokea Ushauri huo, The Civic United Front (CUF – Chama Cha Wananchi) kinapenda kueleza[...]
Sep 24, 2016BODI YA HABARI WA MWACHIA UONGOZI RAISI MAGUFURI
Bodi ya Uhuru Media Group inayosimamia vyombo vya habari vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambavy[...]
Sep 24, 2016NCHI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO VITA YA WENYEWE KWA WENYEWE IMEZUKA KANANGA
Ghasia za siku mbili katika mji wa Jamhuri ya kidemorasi ya Congo zimesababisha vifo vya watu 10.[...]
Sep 24, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.