Baada ya kukosa nafasi ndani ya CCM sasa ameanza kuwasha moto ndani ya UKAWA anasema magufuli atasoma number alichokisema lowassa
Waziri
mkuu wa Zamani Edward Lowassa amewaahidi wafuasi wa chama cha
Demokrasia na Maendeleo Chadema pamoja na wale wa umoja wa katiba ya
wananchi (UKAWA) ushindi wa kishindo katika uchaguzi mku
u utakaofanyika oktoba 25 mwaka 2015.
Mwanasheria mkuu wa Chadema Tundu Lissu alisema kwamba ili mgombea ameweze kuwania urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania
ni lazima awe mwanachama wa chama chochote cha Siasa nchini Tanzania,
hivyo Lowassa ni mwanachama halali wa Chadema pia amechaguliwa na vikao
mbalimbali vya kamati kuu ya chama hicho iliyoketi hadi usiku wa manane.
u utakaofanyika oktoba 25 mwaka 2015.
Lowassa
alisema hayo jana mara baada ya kukabidhiwa fomu ya kugombea urais kwa
tiketi ya chama cha Demkorasia na Maendeleo ambayo itampa ridhaa ya
kugombea urais kupitia umoja wa Katiba ya wananchi ukawa unaundwa na
vyama vinne vya siasa nchini Tanzania ambavyo ni Chadema, NCCR-Mageuzi,
Cuf na NLD.
Aidha,
Lowassa aliyekabidhiwa fomu na Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na
Maendeleo Chadema Freeman Mbowe katika ofisi za Chadema makao makuu
yaliyopo Kinondoni jijini Dar es salaam jana,alichangiwa kiasi kadhaa
cha pesa kitakachomsaidia katika yake ya matumaini iliyofufukia Ukawa.
Katika hafla hiyo Lowassa aliongozana na Mkewe pamoja na wana familia
na ndugu wengine mbalimbali.
Uamuzi
wa Lowassa kugombea Urais ulipokelewa kwa shangwe na umati wa wananchi
uliohudhuria hafla hiyo makao makuu ya Chadema kinondoni jijini Dar es
salaam.
Mwanasiasa
huyo Mkongwe atapambana na Mgombea kutoka chama cha Mapinduzi Dk.John
Magufuli katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu utakaokuwa wa aina
yake mwaka huu wa 2015.
Post a Comment