kunashinikizo kubwa la watu
Shinikizo
dhidi ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, la kumtaka akihame
Chama Cha Mapinduzi (CCM) linazidi kuongezeka na katika timu yake ya
ndani ni watu wawili tu wanaonekana kumtaka abakie ndani ya chama hicho.
Habari
za ndani ya vikao vya kujadili hatua za kuchukuliwa na Lowassa baada ya
jina lake kukatwa kwenye mchakato wa kugombea urais kupitia CCM,
zinasema kuwa wandani wake wanaamini kuwa hana atakachopata kama
ataendelea kubaki kwenye chama hicho tawala.
"Kaka
sikiliza, inavyoelekea shinikizo dhidi ya Lowassa ni kubwa sana. Watu
wake wa ndani wanataka aondoke CCM. Wanaona kama amedhalilishwa mno," kilisema chanzo chetu ndani ya vikao hivyo.
Chanzo
hicho kilichoomba kutokutajwa jina kwa sasa, kilisema kuwa watu wake wa
ndani wanaamini Lowassa akiendelea kubaki CCM atakuwa amewavunja moyo
wale wote waliompigania, hasa vijana waliojaa matumaini ya kumuona
akiongoza taifa hili.
Wandani
wa Lowassa wanaamini kuwa kama akiamua kujiunga na chama chenye nguvu
cha upinzani anaweza kutimiza ndoto yake ya kuwatumikia Watanzania kama
rais wa awamu ya tano.
Chanzo
chetu kinasema kuwa Lowassa mwenyewe amekwisha kuamua kufanya uamuzi
mgumu, ila kuna msuguano juu ya namna ya kuondoka CCM.
Taarifa
zaidi zinasema kuwa watu wawili katika timu ya ndani ya Lowassa ndio
wanaelekea kuwa na mawazo tofauti. Hawa ni Rostam Aziz, mwanasiasa na
mfanyabiashara mashuhuri nchini na mtu mwingine anayetofautiana na
mkakati huu mpya wa kung'oka CCM ni mkewe, Mama Regina Lowassa.
Chanzo
chetu kinasema kuwa wawili hao wanaamini mapigo ambayo Lowassa
amekumbana nayo ni mengi na yanatosha, kwa maana hiyo ingefaa tu
apumzike.
"Sijui
ni kwa nini RA (Rostam Aziz) anakuwa skeptical (shaka). Si unakumbuka
ndiye aliyesema amechoshwa na siasa uchwara... sasa sijui kwa nini
anapunguza makali," chanzo kilisema.
Hata
hivyo, vyanzo vyetu vinaongeza kuwa pamoja na upinzani huo Lowassa
anadaiwa kuwa amekwisha kuamua na kinachosubiriwa sasa ni muda tu wa
kutamka anakokwenda.
Wakati
hali ikiwa hivyo ndani ya kambi ya Lowassa, kuna taarifa za kuaminika
kuwa kumekuwa na mashauriano baina ya watu wake na viongozi waandamizi
wa kambi ya upinzani juu ya mwelekeo wake wa kisiasa.
Mwandani
mwingine katika kambi ya Lowassa alisema kimsingi yeye (Lowassa)
amekwisha kuamua, anachofanya ni kuona kwamba watu wake wa karibu
hawadhuriki na uamuzi wake huo.
Chanzo
hicho kilisema kuwa wenye msimamo mkali katika kambi ya Lowassa
wanaamini utabiri wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kuwa upinzani utatoka
ndani ya CCM utatimia mwaka huu.
"Mnakumbuka ya Mrema (Augustino) alipoondoka CCM siasa za Tanzania zilibadilika mpaka leo? Sasa safari hii ni zaidi," alisema.
Takriban wiki mbili sasa, Lowassa amekuwa na jambo kubwa moyoni analitaka kuwaambia Watanzania.
Mara
ya kwanza alikuwa afanye mkutano na waandishi wa habari Julai 13 mwaka
huu mjini Dodoma majira ya asubuhi, lakini mkutano huo ukahamishiwa Dar
es Salaam ambako pia ukaahirishwa kwa muda usiojulikana.
Tangu wakati huo kumekuwa na tetesi kuwa alikuwa atangaze kujiondoa CCM.
Lowassa
ni miongoni mwa makada 38 waliojitosa kuwania kuteuliwa kuwa wagombea
wa nafasi ya urais wa CCM katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25,
mwaka huu.
Hata
hivyo, jina lake halikuwamo katika orodha ya makada watano
waliopitishwa kwenye vikao vya juu vya chama hicho ambavyo mwishowe
vilimteua John Pombe Magufuli kuwa mgombea urais atakayekabiliana na
wagombea wa upinzani katika uchaguzi mkuu huo.
Post a Comment