0

 Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson Masilingi akisikiliza maelezo kutoka mmoja ya walimu wa darasa la utgawaji utumiaji
wa dawa kwa mgonjwa chuoni hapo Mwl. Allen Greene (kushoto) kati ni Dr. Lucas Shallua akifuatilia kwa makini muzungumuzo hayo.

Moja ya madarasa chuoni

Mke wa Dr. Shallua, Dr. Dorothy Edward Shallua (kulia) akimuelezea Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson Masilingi kuhusiana na kampuni yake ya Mount Eagle Health Care ambayo ofisi zake pia zipo kwenye jengo la ofisi za chuo hicho.


 kutoka kushoto ni Afisa Uhamiaji wa Ubalozi Bwn. Abbas Missana, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Watanzania North Carolina, Bi. Gloria Alex, nyuma ya Mhe. Balozi ni mkewe Marystela Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson Masilingi, mke wa Shallua, Dr. Dorothy Edward Shallua na Dr. Lucas Shallua ambaye akitoa maelezo kwa Mhe. Balozi wakati akimtembeza na kumwonyesha chuo hicho.



Mazungumuzo yakiendelea, wengine katika kufuatilia mazungumuzo hayo kutoka kushoto ni ni Afisa Uhamiaji wa Ubalozi Bwn. Abbas Missana, Dr. Dorothy Edward Shallua (mke wa Dr. Lucas Shallua), Mke wa Balozi Marystela Masilingi, na mwenyeiki wa Umoja wa Watanzania North Carolina, Bi. Gloria Alex.


Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson Masilingi akifanya mazungumuzo na mmiliki wa chuo cha Mount Eagle College &University Dr. Lucas Shallua siku ya Ijumaa Septemba 3, 2016 Balozi Wilson Masilingi alipotembelea chuo hicho kilichopo Winston Salem, North Carolina



 Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson Masilingi akimsikiliza Dr. Lucas Shallua alipokua akimwonyesha moja ya darasa linalotumia kurekodia masomo ya matandaoni.


Chuo cha Mount Eagle kinatoa unafuu kwa Mtanzania anayetaka kujiunga katika masomo ya Unesi na ugawaji dawa na chuo hicho kwa kukuwezesha wewe kufanyakazi hospitanini au kwenye maduka ya dawa pia wanamsomo ya mtandaoni kwa bei nafuu. Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana na Dr. Lucas Shallua barua pepe Lshallua@mounteag.com

Post a Comment

 
Top