0
SEHEMU YA 12

Mtunzi. Long live Josephat

"Ilipoishia toleo lililopita vibweka vinamkumba habiba usiku ule usiku unakua mrefu kwake anaamua kumsaidia mdada aliyeumia huku akiwa anavuja damu baadae anamuuliza kilichomsibu yule dada, d
ada anashindwa kujibu kwa kubanwa na kwikwi lakini anabaki analitaja jina la frenk, habiba anajiuliza maswali mengi kua frenk ndio nani na kamfanya nini yule dada , habiba anabak njia panda,   songa nayooo".....

" Alitaka kuniambia kitu lakini alikua kashikwa sana na kwikwi, sikumpata vizuri nilikaa kimya ,kumfuatilia kwa makini nijue ni nani huyo frenk, lakini nilicho ambulia ni lawama kwa frenk na vilio, niliamua kuhitimisha mjadala ule kisha nikamkaribisha kitandani kwangu, ulikua usiku unaoelekea kua hasubuhi, nisingeweza kumuacha aondoke kwa hali ile, alikua anajiskia vibaya sana alikua anataka kuniliza mpaka mimi, nilijisogeza pembezoni mwa kitanda kisha nikamkaribisha aje kulala, maskini dada wawatu alikua kabadilika mpaka sura mishipa imemtoka kwa ajili yakulia, punde tu alisogea akajilaza, alikua ana mafua yaliyosababishwa na kulia lakini nilimvumilia, nilikua naomba pakuche maana vitimbi nilivyokutana navyo kwa siku ile vilikua vingi jamani mpaka nikawa najiuliza hapakuchi tuuu, maana hali yapale ilikua inachangamoto sana, kwa upeo wangu mdogo niliamini kukutana na vitimbi vile pale ni ushahidi tosha kua mwanzo mgumu lakini nitazoea kadri siku zinavyokwenda, nililala chali   namimi kuupata usingizi ni kazi kweli, nilikua namkumbuka batuli, Baba , Kevi nilimchukia kwa kunipitisha kwenye kipindi kigumu na kunikondesha kwa mawazo nilimtukana kila,nilipo kumbuka jina lake,   muda si muda niliskia watu wanaongea na kelele zilikua juu safari hii, milio ya mibuluzo ya viatu ikienda huku nakule, niliamka kutoka kwenye kausingizi ka mda mfupi,  kumbe ilikua hasubuhi imefika, kwahiyo mishe mishe zilikua zimetawala watu walikua wanaenda kuoga nawengine wanajiandaa kutoka, niligeuka upande wa yule binti ila sikumuona pale kwangu wala chumbani nilimuangalia kemi kama yupo   kemi alikuwa yupo macho teyari anachezea simu yake nilimuuliza kama kamuona yule dada nilie lala nae alinijibu hapana nayeye ndio anaamka mda ule,   basi nilijiandaa nikachukua kitaulo changu nikaenda kuoga, watu sio wengi bado, mabafu hayajai wala hamna anaemsubiri mtu atoke eidha bafuni au chooni ili apate naafasi yakuingia yeye, basi muda mchache nikawa nimemaliza,  mambo yakujipamba nakusubiria wageni wapya na kuwaangalia wakina kaka na warembo waliotuzidi, masomo yalikua bado hayajaanza kwa hiyo siku zote zile zilikua za usajili  masomo yalitarajiwa kuanza mpaka wiki iishe ndio kwanza tulikua tupo kwenye juma nne kwaio mpaka ifike jumatatu bado sana, basi taratibu nikawa nimevaa kamkoba kangu na kiwalo flani ivi cha pink ambacho nilienda kukiopoa mlimani city , sikutaka kuonekana kama habiba wa mwananyamala , nywele nilikua nimekarabati kwa wigi langu lenye blonde hair baba asingeweza kujua kitu hijabu ilistiri siri zangu, basi taratibu nikawa naelekea, Administration (utawala) watu wengi sana walikua pale yaani ni wengi sana kila mtu alikua kwenye mishe mishe za kujaza form nakusubiri maelekezo aende wapi arudi wapi, watu walikua wapo bize sana nili enjoy ubize wao, nilikaa kidogo pale utawala kama na mimi nina kitu nataka nikifanye kumbe waapi!!! nauza sura tuu, ila kwakweli kuna watu wameumbwa watu wazuri jamani makaka ( mahand some wakutosha , daa yaani basi tuu, nilijisemea moyoni kweli hiki chuo, baadae nikaamua kuondoka nikaenda mpaka kule karibia na getini tulipotokea jana , watu walikua bado wana miminika, sura nyingi lakini hamna hata ninaye mjua, baada ya kama hatua kadhaa ilikuja gari flani hivi aina ya range rover ilipaki karibu yangu nilisogea kidogo kioo tinted( cheusi tupu) kilishushwa sura ambayo ilikua imeshika stering ilinishangaza kidogo alikua ni mtoto wakike mdogo yaani saiz yangu manukato yalikua yananukia kama jini, ndani alikua yupo mwenyewe tuu, baada ya muda alinitoa kwenye kukodoa kisha akanisalimia, kistaarabu tuu,"
......"mambooo"...
......habiba....."poa"....

......."samahani dada naomba niulize eti Admini strationi ni wapi sijui,?"...
.....habiba...." pale mbele kuna kigeti we ukifika kunja kona yakulia utapaona pana ghorofa ukiingia tu,"...
..." akhasante dada"...
......habiba....." poa"..

....." hiki kidada kinajiskia yaani kinaonekana kina dharau sana na mimi nimekosea sana kukijibu ninge kiambia mimi sio mlinzi na wala sipajui huko anapotaka kwenda, kina ringa kwa gari ya baba atafute gari yake kama kweli ye mwanamke, kamalaya sana kanaonekana tuu, sasa mtu kama yulee anaweza kusoma kwelii,   nilimponda yule sister duu aliyeondoka na gari muda mfupi tuu baada ya kuniuliza kama napajua utawala, niliachana nae nikaendelea kutalii, baada ya muda nikamuona james kwa mbali kidogo nilichenga asinione , sikutaka usumbufu nilikua nataka nitalii mwenyewe, nilizunguka mitaa ya mule ndani migahawa yote niliitembelea , uzuri wa kile chuo kuna fukwe nzuri tuu nilitembelea zote,nikawa naanza safari ya kurudi jua lilikua limeanza kuchoma, nili jivuta taratibu kurudi ndani, nilipo kua nakaribia kufika karibu na getini teyari kuingia ndani ya Hostel, nilimuona yule binti aliyelewa jana usiku akiwa anazozana na yule binti aliyekua kaja jana usiku akiwa analia na akiwa anavuja damu, sikujua wanazozana nini ila ilinibidi niende kusikiliza wanagombania nini,  kufika pale watu wakawa teyari wamewaamulia nikakosa uhondo, nikaamua kumfuata yule nilie msaidia jana usiku aliyekua kwenye hali mbaya nilihisi anaweza kunikumbuka kwa sababu alikua hajalewa kama yule mwingine, hali ilikua mbaya kwake kumbe alikua ni mtu wa jazba sana alikua anawakaripia walio mshika na alikua anatoa matusi ya hapa na pale, ila sikujali nilimvaa vile vile na matusi yake, nilianza na kumpa salamu,"...

....habiba..." dada mamboo"...
......mshari..." poaa"..
........" mmmh!! Yule dada anajibu kwa shari kweli yaani utafikiri mimi ndie nilie gombana nae  wakati nia yangu nikutaka kujua tu anatatizo gani"...
....habiba...." vipi unanikumbuka dada"...
.....mshari...."  eeh. Sasa mimi nikukumbuke wewe nani mpaka nikukumbuke we sema shida yako swala la mimi kukukumbuka la nini, sikukumbuki haya sema shida yako"....

....."mpaka pale nikaona kweli huyu dada mjinga hana akili kabisa kumbe jana nilifanya makosa kumsaidia daa kweli tenda wema uende zako usingoje shukrani sasa nimeamini chamsingi nimwambie samahani nime kufananisha alafu niendelee na mishe mishe zangu niachane naye huyu mbulula, nilikua namsema kimoyo moyo yule mdada alikua wamakamu yangu pia,kwa majibu yale aliyonipa nikaamua kuachana naye"
......habiba......" samahani dada nimekufananisha sio wewe nilikua nadhani ni mtu flani samahani sana dada"...
...."niliamua kumkataa kwa stahili ile sikuendelea nae nikaamua kwenda zangu , huku. nikijilaumu kujipendekeza na kumsaidia , wakati nawaza yote hayo nikaamua niongoze mpaka kizota hostel nikalale maana jana sikulala vizuri kabisaa, huyoo taratibu nikawa nimefika hostel  kuingia ndani nikakutana na mizigo kibao kwenye kitanda cha pembeni yangu nilikua najua kua kuna mtu anaingia mule ndani, sikujua ni nani edha ni monika au ester maana mimi nakemi teyari tupo ndani sasa hao walio baki sijui nani ni nani, baada ya muda kidogo aliingia kemi alikua amevalia mwenyewe sijui alikua katoka wapi, story zikaanza".....

.......kemirembe...." hivi habiba unamfahamu frenk?",
.....habiba...." hapana kwani vipi?"....
.....kemirembe...." mmmh! maana kila chumba nachoingia anazungumziwa yeye, sijui yukoje nina hamu ya kumuona kweli huyo frenk"....
.....habiba....." unaweza kukuta ka mtu kenyewe ka kawaida tuu sema watu wanakuza mambo siunajua sisi  wanawake tena kwa kukuza kitu"...
.....kemirembe......" ila kweli maana tupo nawashamba kibao humu wengine hawajawai kuona watanashati ila mtu kama mimi mabrother men nawajua wakawaida nawajua yaani hunidanganyi,".....
.....tulicheka nakemi baada ya kemi kutoa sentensi ile,kabla hatujamaliza kicheko chetu mlango ulifunguliwa ghafla , sasa huyo aliefungua mlango ndio aliye nichosha , yaani sikuamini si yule sister duu aliyekua anaendesha gari aina ya reng sijui alikua anatafuta nini?"...
....sister duu....."mambozenuu"...
......kemi...."safi za kwako"..
....sister duu..." poa tu, samahani jamani nimeambiwa hii itakua rum yangu sijui nyie ni member wenzangu?"
...." kaliuliza kale kasister duu, sikukajibu niliacha kemi aongee nako, si unajua sikumpenda toka kule mwanzo tulipokutana"...
...kemi...." yea sisi ni member mimi naitwa kemirembe wanapenda kuniita kemi na huyu hapa anaitwa Habiba, sijui wewe unaitwa nani mwenzetu?"...
....sister duu..." oooh kumbe unaitwa Habiba, mimi naitwa Monica nashukuru kuwafahamu Kemi na Habiba,"........

......." kale kasister duu eti kumbe unaitwa habiba sasa sijui yeye alitaka niitwe nani, maana anaonekana hajalipenda jina langu sasa mjina wake mbona hata hauvutii eti Monica, niliwaza kwa muda maneno hayo, sijui kwanini namchukui Monica kwasababu kisa hata sikijui",
....Kemi...." basi karibu mwana member utalala pembeni ya habiba au juu utachagua wewe,"..
......" kemi aliendelea kumjali yule sister duu sikujali hata kidogo, basi kale kasister duu kakatoa pochi lake kakaanza kupanga vitu kalivua shati lake kaka baki na vesti moja nyeusi , nyuma ya mgongo alikua anatatuu iliyokua imekaa juu kidogo ya bega nyuma lakini, ilikua imeandikwa  FRENK <3  ilikua imekaa vizuri ila nilijua fika huyu mdada ni muhuni tuu, baada ya muda kalitoa simu zake kwenye mkoba wakati huo naongea nakemi lakini nampiga jicho la wizi yule sister duu anavyopanga nakutoa vitu vyake, wivu ulinishika alipotoa mikufu na simu zake simu nzuri alafu za bei hiyo mikufu ndio usiseme nyie acheni tuu kale kasister duu kiboko inaelekea kwao ni wakishua sana baada ya muda alitoa mipete ya thamani kisha, akaviweka vizuri, akatoa shuka lake na baadae akaanza kukarabati kitanda chake aliamua kulala juu, alipanda juu kwenye deka ya pili, kuacha hii yetu mimi na kemi, basi alikua kakiremba kweli kitanda chake kama yupo hotelini vile wivu ulinishika sana kwakweli na yeye alikua mzuri kweli  kisura ila sikupenda"....


Vip kuhusu sister duu wataiva na habiba


Sehemu ya 13



" ilipoishia toleo lililopita"

" monica anapata chumba ambacho yupo habiba, habiba anakua haamini lakini anaamua kumkaribisha monica ambaye anaonekana ni mrembo na ni tajiri, monika anaaza maandalizi yakuandaa sehemu yake, wakati huo ni muda mchache tuu umepita habiba ametoka kuonana na wanawake ambao walikua wamelala usiku chumbani kwao, wakiwa wanagombana mmoja anamkana habiba ,habiba anaamua kuachana naye songa nayoooo"...

" Basi nikiwa namtolea macho sana yule Monica alimaliza kupanga vitu vyake , kwa kweli yule mdada kabarikiwa haikua rahisi sana kuto kumuonea wivu monica,  kwa jinsi alivyo na vitu alivyonavyo, ilikua imetimia jioni tukawa tunajiandaa mimi na kemi kwenda kutembea  pamoja na kutafuta chakula pia, si unajua maisha ya kichuo chuo tulikua hatupendelei kula ndani hii ni pamoja na watu kutaka kuyajua mazingira ya kigamboni , basi wakati tupo kwenye harakati za kujiandaa , Monica aliingilia nakutoa wazo"..

....Monica...." samahani jamani lakini nilikua napendekeza au naomba tukale sehemu nzuri ili tupate kubadilishana mawazo na kuongea mawili matatu kama member wa chumba kimoja"..

....." yani hapo ndipo nilipokua napataka huyu dada sijui hajielewi sasa anataka twende tukale wapi na sidhani kama anapatambua vizuri huku kigamboni kwasababu mimi na kemi wangu tulipanga twende tukatembee sehemu mmoja ivi inaitwa kwa Dani na baadae tununue vyakula, sasa sijui sister duu anataka nini,? Nilijisemea moyoni huku nikijiandaa kumjibu,"
....habiba....." kwahiyo monica ulikua unapendekeza twende tukale wapi au tukakae wapi tuongee"..

.....Minica...." Moven pick, nahisi pale ndio sehemu special kwetu sisi, tunaweza kukaa na kuongea mambo yetu bila bugza yoyote ile, au mnaonaje"..

......" alipo itaja moven pick akawa ameingia kwenye kumi na nane zangu yaani kweli huyu dada alikua anahamu kuona naongea shombo, nilijipanga kwa kumshambulia, kwasababu nilikua nina wivu nae na pia nilikua namchukia ikabidi nimpe vipande vyake"...

.......Habiba...." samahani lakini kama nitakuudhi,  hivi kwa akili tuu yakawaida pale moven pick chakula kina gharimu pesa yangu ya Mwezi mzima ya hapa chuo yaani poket money, na ukijumlisha usafiri, wa kwenda na kurudi hivi kweli hilo unadhani ni wazo zuri sijui nyinyi wenzangu kwetu wengine pesa ngumu"..

...."nilizidisha vitu vingine kwa mfano pesa ya chakula pale moven pick sijui hata ni shilingi ngapi? ila nilihofu itakua juu ila kwa kutaka kumuonyesha Monica kua wazo lake ni pumba ilibidi niongee vile kama mtu mwenye uhakika na ninaye fahamu bei za mahoteli makubwa, kuhusu usafiri wa kwenda na kurudi ilikua haizidi hata elfu mbili  si hapo posta tuu, hata ivyo sikuuliza kama tuna changa au lahh!! Mimi nilichokua nataka ni kumkera tuu monica baada ya kumaliza kumpa vipande vyake nikawa nasubiri nione atachukulia vipi majibu yangu kwa jazba au kawaida"...

......Monica......" hahahahahahh,!  Nimekuelewa habiba lakini nataka nikutoe hofu ni kweli moven pick pako juu ukilinganisha na sehemu tulizo zizoea lakini napenda niwataarifu kua trip hii nitagaramia mimi kuanzia vinywaji usafiri mpaka chakula, naomba msihofu member naomba leo iwe siku special tuu, yaani naomba tuifanye iwe siku maalum kwa kwenda sehemu maalum kula kuongea na kubadilishana mawazo,"....
......" Monica alikua anajiamini sana hilo pia lilinifanya nitamani kuwa yeye na nizidi kumuonea wivu, kemi hakua mbali sana aliamua kuingilia kati mjadala ule"..
.....kemirembe....." lakini Monica kwanini tusiende sehemu yakawaida tuu tuka kaa tuka ongea na tukafurahi kuliko kwenda mbali kote huko alafu garama kubwa au we unaonaje?"...

......"nilikua nasubiri jibu la Monica nione litakuaje eidha atabadili msimamo wake au lah"...

......Monica....." guyz mbona ni kitu kidogo tu jamani mi naomba tufanye leo siku special kwetu kwa ajili yakukutana na kubadili mawazo pamoja na ushauri wa hapa na pale , kitu gani bwana kikubwa pumzi pesa makaratasi au mnasemaje ila sita walazimisha kama hamtataka kwenda  naeshimu mawazo yenu"

......" mmmmmh!!! Mwenzangu mambo yakuchezea shilingi chooni nani anataka mi mwenyewe sijawahi kwenda kula huko moven pick leo imetokea bahati sitaki kuilazia damu kabisaaa , lazma niubadili mchezo asije akagairi huyu mpumbavu ,hata ivyo hatutumii pesa zetu si yeye ndio atapata hasara , ngoja nimuingie kistahili, nilijikuta nikitamani kwenda lakini naona aibu jinsi ya kukubali, sikuwaza sana hata ivyo niliamua kuumaliza mjadala ule,"

......habiba....." basi sawa kama umeamua hivyo sisi tupo teyari, ngoja tujiandae kidogo si unajua sehemu kubwa zile"....
....." kemi alikua ananikubali sana baada ya mimi kukubali nayeye akaamua kukubali, basi maandalizi yakaanza mishe mishe za nguo vioo na maurembo mengine yakawa yanaendelea, sio siri Monica kajaaliwa kaumbika dada wawatu na anajua kuvaa, alivaa nguo flani ivi kimini cha bei  sana kwa kuangalia tu kilivyo na ubora wake si chini ya laki moja, maana kilikua kina naksh ya chui na maurembo yakuvutia kwa kweli nilimpa saluti ya kimya kimya, kitu ambacho monica kilifanya nimuonee wivu ni jinsi alivyo, kwanza ana shepu yaani anakiuno cha cha kushikika namba nane yenyewe hana tumbo akivaa kimini kiuno na tako lake unaviona jinsi vilivyo jipanga ,anamguu huyu dada ana sura nzuri yaani alikua kapedelewa kwakweli, mimi na kemi tulikua tunajiremba lakini macho kodo kwake jinsi alivyo tufunika, kemi kama kawaida yake anakila kitu cha kumfanya mwanaume wa sasa ampende au adate kama wanavyosema waswahili, kemi hawezi kumpita mwanaume wa sasa aliye rijali na asiye na matatizo ya kiafya bila kugeuza shingo , nilikua naskia miluzi tuu nikitembea na kemi, basi ndio hivyo bwana kasura kake mwenyewe kakuvutia basi wala hana hata habari mimi nilikua wakawaida tuu sijui nijizungumziaje, paja langu la wastani kiuno changu sura yangu na makalio kidogo yalikua yamejaa jaaa, mule ndani alikua anaongoza kemi anafuata bibie Monica na Mimi wa mwisho ila kwa ubora wakila kitu Monica alikua anaongoza, basi niliibua kimini changu kilichoshika umbo langu vizuri nikatoa na kamkoba kangu, siku ile niliamua kuvunja kabati kwasababu sehemu tunayoenda ni yenye hadhi sana, nilipanga nivae vile kwenye sherehe ya kuwakaribisha mwaka wakwanza ila ilibidi tuu ni vunje kabati kwa mtoko ule wa movenpick, baada yakila mtu kumaliza , yakaanza mambo ya marashi, bwana weee yule Monica kama jini anavyonukia yalikua yametawala marashi yake yeye tuu, mpaka yetu yakaonekana hayanukii, mmmh!! Basi pilika zakujiremba zikawa zimeisha mambo yamtoko yakawa yameanza , basi taratibu tukawa tunaondoka zetu mlango tulifunga tukatoka na funguo zetu, hali ilikua tofauti kwangu maana , nikimuangalia monica kuanzia tembea yake viatu vyake miguu yake nilikua najiona kama sijavaa vile, ila ningefanyaje na pale mimi ndio nilikua nimevunja kabati, na hapo bila zile milioni mbili sijui ningevaa nini leo, tulipotoka getini nikajua pengine Monica ataiita bajaji au tax lakini haikua hivyo tuliongoza mpaka kwenye parking za watu wakawaida , mwana dada alitoa funguo ya gari aliminya alam gari ikalia kisha tukaelekea garini , haoo mabinti tukazama ndani ya gari nilikaa mbele na dereva ambaye ni Monica kemi alikaa nyuma haikuchukua mda tukawa getini yani nilikua namuangalia monika si mmalizi anavyo endesha gari na jinsi alivyo, kiyoyozi mpaka mwisho na vioo ni tinted giza tupu, basi mziki taratiibu, punde tu tukawa tumefika fery pantoni lilikua lipo  liliruhusu magari hao tukawa tumeingia, hivi hata kama ni wewe mtu wa makamu yako sister duu anamiliki gari na kwa jinsi alivyo huwezi kumuonea wivu kweli au kumchukia kwakua yeye anacho na wewe huna, basi mimi mwenzenu ndio nilichokua najiskia nikimuona Monica, punde tu tukawa tumefika n'gambo, haikuchukua hata dakika tatu tukawa tumefika Moven pick, si unajua posta na moven pick ni pua na mdomo, basi bila kupoteza muda tukashuka kwenye gari , mtu wa parking alikuja na kwenda kuipark  gari, tuliongozwa moja kwa moja mpaka mezani yaani kama vile monica alikua keshaweka Oda pale hotelini nilihisi hatutopata nafasi maana palitengwa vizuri nikama tulikua tunangojwa sisi mandhari ya pale ni nzuri sana inavutia kwakweli watu wengi wanaonekana wamekuja kibiashara na wengi ni watu wazima hamna kelele wala fujo, basi ilikua ni burudani tuu, ghafla muhudumu akaja na menu, akatukabidhi tukawa tunachagua , mavyakula mengine hayaeleweki lakini niliagiza chips kuku kama ilivyo andikwa  na kiswahili pia kipo kwenye menu kwaio haikutuwia. Vigumu sana kutambua ni vyakula gani vimeorodheshwa kwenye lile daftari, wenzangu nao.  waliagiza kama mimi, kinywaji kiliagizwa na Monica aliagiza mvinyo wa sant anna, sijui alikua anawaza nini maana sikua nakunywa pombe kabisa nilihitaji maji tu yakilimanjaro, kemi pia aliagiza kama mimi, baada yakumaliza zikaanza story huku Monica akiwa anamuita muhudumu , muhudumu alikuja kumsikiliza alimuagiza aje na glass mbili ili awekee mvinyo, basi punde tuu glasi zikaja , baadae akaanza kumimina mvinyo ule kwenye zile glass, akampa moja kemi na nyingine akanipa mimi, nilisita kidogo ila sikutaka nionekane mtoto wa mama mbele ya monica niliianza taratibu sana ile glass, hali kadhalika na kemi pia , mara story zikaanza kukolea likatoka wazo kua kwanini tusiende club, hapo nikatoa macho kidogo"....

......Minica...." aaah jamani kwanini tusiende clabu hapo maisha club ni karibu tuu, tena usafiri tunao jamani , au unasemaje habiba maana chuo bado masomo hayajaanza bora tujiachie mapema ili yakianza  twende nayo sambamba "

......." mmh!! Yule Monica ni mtu wa starehe sana yaani anahimiza twende tena clabu , na hapa sasa kanipa mzuka ngoja niende tuu bwana nikapunguze mawazo hata ivyo chuoni kunatisha tisha ngoja tukaenjoy, bwana, maisha ndio haya , niliamua kukubali unafikiri ningefanyaje na mambo yenyewe ndio kama vile mvinyo ndo unapanda mwanamke najikuta naropoka tuu".....

......habiba......"  sawa jamani ila tusichelewe, kurudi jamani simnajua tena"....
....." nilitoa wazo tuu lakini sidhani kama lilikua ni la muhimu kwa wakati ule tulichofanya ni kuinuka na kuondoka zetu bill alikua analipa Monica, haoo tukawa tunaenda zetu clab, safari hii ilikua ni mwendo wa story na kucheka tuu si unajua tena kilevi kilichangia kwakweli  sikuwa napafahamu Maisha clab lakini nilikua napaskia tu sikuile ndio nilipajua nje pale karibu na coco beach mataa yalikua yanawaka sana monica alishuka garini na sisi tukashuka nae, baada ya muda tulienda kukaa baa ndani ya ukuta wa maisha clab kabla hatujaingia clab kwenyewe ziliagizwa bia kama kawaida nimo nikawa nakunywa kilimanjaro nitafanyaje na mimi ndio na jaribu sitaki kuonekana mtoto wa mama yaani mpaka mrembo monica anizidi hii itakua aibu, wakati tunasubiri kuingia clab, monica alinituma nikamchukulie simu yake,  ile naenda kwenye gari matapishi yakanibana nikawa nakimbia kwenda kutapika nikapishana na kaka mmoja alitaka kunizuia lakini nilimkwepa kwakua matapishi yalikua yanaanza kuja nilienda mpaka kwenye gari la monica kisha nikatapika pembeni ya gari, baadae yule mtu alikuja na kunifuata mpaka pale nilipo, nilikua najifuta futa tuu si unajua tena ,  yule jamaa alini sihi nitafute supu usiku ule au nyama choma ili niondoe maswahibu yale nilimuelewa lakini sikujua kwanini ananishauri mimi, kabla sijamaliza kutafakari yule jamaa akawa ameondoka naye akawa ameingie mule clab, sikushangaa sana nilifungua gari kisha nikaichukua simu ya monica, wakati nampelekea simu monica ,simu ikaanza kuita  ilikua ni simu yake inaita  kutoka kwa frenk kama ilivyokua inasomeka, sikupokea ila niliamua kumpelekea mpaka pale alipo, haikuchukua muda sana ikaita tena , akaipokea akaanza kuongea, mimi nakemi tunacheka tuu yaani pombe zimetukolea , Monica aliongea na simu kisha akaomba atoke kidogo aliaga kua kuna mtu anaenda kuonana naye, baada ya kutoka nilimuona yule jamaa aliyenipa ushauri wa kunywa supu alikua anamsubiri monica baada ya moica kukutana naye ,waliongea kidogo kisha nikaona Monica katoa mkoba wake akamkabidhi yule jamaa, baadaye monica alikuja mpaka mezani kwetu akatuaga kua anaenda wash room, kujisaidia nakwamba tuagize chochote , huyooo monika alienda zake yule jamaa aliekua anaongea naye pia hakuonekana maeneo yale, baada ya muda kidogo nikamuona monica anarudi na mkoba wake, sikuelewa kirahisi ni kwanini amuachie mkoba yule jamaa kisha arudi na mkoba ule ule wakati alimpa yule kaka, au monica ni Malaya na ndio kazi yake, kaenda kupatana bei na yule jamaa, mpaka hapo sasa nikawa makini na monica kunakitu nilihisi hakipo sawa kuhusu yeye"


Fuatilia monica ana nini na kitu gani hakipo sawa kwavmonica


Post a Comment

 
Top