Wanawake ni viumbe
tofauti sana (complex) wao ni walezi kwa asili, waumbaji wa vitu,
wasimamizi wazuri na wabunifu sana.
Wanaweza kwa
urahisi sana kuelezea kitu kilichopo kwenye akili zao likija suala la deal lolote
la biashara kama kununua au kuuza.
Wanaweza sana
kwenye mambo ya design na hata mawasiliano.
Ila likija suala
mwanaume hapo ndiyo kuna tofauti.
Jawabu ni kuelezana
tena kwa upole na upendo jambo lolote unahitaji mwanaume afanye.
Kuna ubaya gani
wewe kushangalia kile mume wako anapenda (hobbies)
Kumbuka unaweza
kuwa wewe hupendi kwenda naye huko yeye anapenda kwenda, lakini kuna wanawake
wanafurahi kuwa naye huko wewe umekataa kwenda na hana njia kwani ni kitu
anakipenda na ni sehemu ya maisha yake (kama hatendi dhambi).
Inawezekana jioni
kabla ya kulala mkawa na glass ya juicemnakunywa
wawili huku watoto wamelala, wewe mwanamke kwa ujasiri shusha story za
michezo mambo ya Chelsea,Manchester united, Liverpool au
hata Yanga na Simba just for fun, au hata habari za mafisadi au
hata habari za mfalme Suleiman au Daudi au business ambazo umezitafiti hapo
mwanaume atajua nina mke ndani ya nyumba.
Pia unaweza kubadilisha
akili katika kufahamu mambo.
Je, itakuwaje kama
na wewe mwanamke siku ukamwambia mume wako leo pamoja na watoto tunaenda lunch
sehemu au dinner sehemu kula, au kula kitimoto na nk pamoja na watoto wenu kwa
hela yako au bajeti yako au maamuzi yako.
Wakati huo huo
umetinga kiwalo chako cha nguvu (sexy) hadi unamkumbushia zile ezni zenu ambazo
zilifanya avutiwe na wewe hadi kukuoa.
Jaribu kufikiri
mwenyewe hivi ukiondoka asubuhi unawasiliana na mumeo mara ngapi?
Siku hizi karibu
kila mtu ana simu ya mkononi, unaweza kutuma sms, au kumpigia just to say hi
honey! Mbona wakati wachumba sms zilikuwa zinatumwa hadi vidole vikaota sugu,
leo kunani?
Jifunze kwa busara
na hekima kujua nini kinaendelea katika maisha ya mume wako na pia onesha
kwamba unamjali sana (care) na kwa njia hiyo automatically atakupenda
zaidi na ndoa yenu itakuwa imara zadi.
Related Posts
DAWA YA MWANAUME ANAYEFIKA MAPEMA KILELENI NA NAMNA YA KUCHELEWA KUFIKA KILELENI
Chanzo ni nini?Tatizo hili halina sababu za kitaalamu zilizofanyiwa utafiti zikakakubalika ila [...]
Sep 24, 2016madhara Ukikaa Muda Mrefu bila Kufanya mapenzi
Ukikaa Muda Mrefu bila Kufanya tendo la Ndoa madhara yake ni kama haya: Hasira za mara kwa mara[...]
Sep 24, 2016HADITHI :MAPITO NA RAHA ZA DUNIA SEHEMU (12-13)
SEHEMU YA 12 Mtunzi. Long live Josephat "Ilipoishia toleo lililopita vibweka vinamkumba hab[...]
Sep 10, 2016HADITHI: MAPITO NA RAHA ZA DUNIA SEHEMU [7-10]
Sehemu ya 7 Mtunzi. Long live josephat Ilipoishia toleo lililopita,......... ..." habiba a[...]
Sep 09, 2016HADITHI: MAPITO NA RAHA ZA DUNIA {1-2}
SEHEMU YA 1 "Maisha huwa magumu pale unapopenda usipo pendwa,lakini huwa magumu zaid pale un[...]
Sep 08, 2016HADITHI :MAPITO NA RAHA ZA DUNIA {3-4}
Sehemu ya 3 Mtunzi. Long live josephat Ilipoishia toleo lilopita, habiba anamdadisi [...]
Sep 08, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.