0
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry amesema hii leo atakutana na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wiki hii nchini Ujerumani kabla ya kufanya mazungumzo pamoja na kiongozi wa utawala wa ndani wa Palastina Mahamoud Abbas.Hii ni mara ya kwanza kwa waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry kuthibtisha ripoti za vyombo vya habari kuhusu mkutano wake pamoja na Netanyahu na Abbas.John Kerry hakusema lakini wapi hasa anapanga kukutana na Mahmoud Abbas.Amedokeza tu mazungumzo yatafanyika mashariki ya kati.Hata hivyo mazungumzo hayo huenda yakafanyika nchini Jordan.Akizungumza katika makao makuu ya shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni-UNESCO mjini Paris,waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani ameongeza kusema anapanga pia kuzungumza na mfalme Abdallah wa Jordan na viongozi wengineo.Matamshi ya John Kerry yametolewa katika wakati ambapo Israel na Marekani zinaanza upya mazungumzo kuhusu hatima ya msaada wa kijeshi ambao Netanyahu aliusitisha akilalamika dhidi ya makubaliano ya mradi wa nuklea wa Iran

source dw

Post a Comment

 
Top