0

Manchester United wametoa kipigo cha mbwa mwizi dhidi ya Mabingwa Watetezi wa Premier League Leicester City kwa kwafunga mabao 4-1, mchezo uliofanyika kunako Uwanja wa Old Trafford.

Katika mchezo huo ambao nahodha wa United Wayne Rooney alianzia benchi, Man United walipata bao la kwanza dakika ya 22 kupitia kwa Chris Smalling kuunganisha mpira wa kona uliopigwa na Daley Blind.
United waliongeza bao la pili kupitia kwa Juan Mata dakika ya 37 baada ya kugongeana pasi kwa uzuri na Lingard kuwahadaa mabeki wa Leicester.
Bao la tatu la United lilifungwa na Marcus Rashford dakika ya 40 baada ya kuunganisha pasi nzuri ya Juan Mata.
United walifunga bao lao la mwisho dakika ya 42 kupitia kwa Pogba kufuatia kona nzuri iliyochongwa na Daley Blind.
Leicester City walipata bao pekee la kufutia machozi dakika ya 60 kupitia kwa juhudi binafsi za Demarai Gray.
Nahodha wa United Wayne Rooney aliingia dakika ya 83 kuchukua nafasi ya Marcus Rashford.

Post a Comment

 
Top