0
Naibu wa rais nchini Afrika Kusini alichukua fursa bungeni wakati ambapo rais wa taifa hilo Jacob Zuma alikuw
a amesafiri nje ya nchi kuwakilisha maswala ya serikali ikiwemo kondomu isiyo na kelele na yenye ladha ya machungwa kwa wabunge.

Cyril Ramaphosa alielezea kwamba mipira hiyo ya kondomu ilitengezwa kufuatia malalamishi kwamba kondomu za serikali zilikuwa zina harufu mbaya na kelele.

Tangazo hilo la Ramaphosa lilizua hasira na tabasamu kutoka wanachama wa ANC na kelele kutoka kwa upinzani wa chama cha EFF huku baadhi ya wanachama wake wakisema ''mpatie Zuma hizo''.

Matamshi hayo ya wanachama wa EFF yanatoka miaka 10 iliopita wakati bwana Zuma alipokiri kwamba katika kesi yake ya ubakaji ,alifanya mapenzi bila kutumia mipira ya kondomu na mwanamke aliyekuwa na virusi vya HIV.

Aliondolewa mashtaka hayo lakini kukiri kwake kulizua mshangao mkubwa nchini humo ambapo takriban watu milion saba wana virusi.

Source bbc Swahili

Post a Comment

 
Top