0
Kenya imetia saini makubaliano na kampuni ya Volkswagen ya Afrika Kusini ili kutengeza magari hayo katika taifa hilo la Afrika Mashariki ,kulingana na taarifa ya serikali.
Volkswagen imeing
ia katika mkataba huo kwa kutumia kampuni ya kutengeza magari nchini Kenya KVM mjini Thika kuunganisha sehemu za magari hayo ikianza na gari lake maarufu la Volkswagen Vivo.
Thika ni mji wa viwanda ,uliopo kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa Kenya Nairobi,na serikali ya Kenya inamiliki hisa katika kampuni hiyo.
Gari la kwanza la Volkswagen Vivo linatarajiwa kuunganishw akatika kiwanda hicho kufikia mwezi Disemba.
Kampuni hiyo ya ujerumani ilikuwa ikifanaya operesheni zake Kenya katika miaka ya 60 hadi mawaka 1977 ,ikiunganisha Mabasi ya Volkswagen,mabasi madogo na matatu ya kombi iliokuwa maarufu sana wakati huo.

SOURCE BBC SWAHILI

Post a Comment

 
Top