0
Sehemu ya 7

Mtunzi. Long live josephat

Ilipoishia toleo lililopita,.........
..." habiba anaanguka nusura azirai  baada yakutajiwa majibu ya vipimo vya ukimwi alivyopima,  hali inabadilika baada yakugundua kua sio vipimo vyake na kwamba si kweli kua ameathirika, anarurahi baada yakujua hivyo lakini hofu inamjia tena baada ya baba yake kumtaka akapime tena siku inayofuata, habiba anakubaliana nae na kuamua kuondoka, kwenda chumbani,  punde simu inaita  simu ya  kulee kwa kijana yule wa magomeni, alie msev kwa jina la roho mbaya.   Songa nayooooo"

Habiba.....   " daaa huyu mpuuzi nae anataka nini sasa".......
" sikua na jinsi niliamua kuipokea ile simu,"

......Habiba....." hallow" ...........roho mbaya......" hallow , we mwanamke, sikiliza kwa makini  kesho nataka uje umevaa vizuri  namaanisha vizuri yaani  uvutie, kuna kazi nataka  kukupa utaijua ukifika huku magomeni, natena naomba usichelewe kwasababu  wafanyakazi wachelewaji huwa wananiudhi sana sipendi hilo litokee kwako saa mbili asubuhi nakuhitaji hapa ofisini kwangu"...
........." simu ilikatwa ghafla, yule jamaa mwenye roho mbaya kwakweli simuelewi kabisa, na anadai nivae niwe navutia, anataka nijiuze au anadangulo anataka anipelekeee!!, huyu jamaa mbona anataka kunizeesha sasa, kwa jinsi maisha yangu yanavyoenda sidhani kama mwaka huu nitaumaliza,"   .
......." nilijisemea moyoni na kujiuliza maswali hayo, hakika wakati niliokua nao ni mgumu, hebu fikiria asubuhi niende kupima kisha niwahi kule kwa yule mpuuzi magomeni, mimi sio mchawi bwana siwezi kuwa sehemu mbili tofauti, kwa wakati mmoja,, atasubiri sana ntaenda kwa muda wangu ngoja kesho nikapime niondoe haya mawazo, kwakweli nilikua napitia kipindi kigumu sana mtoto wa miaka ishirini na mbili, si rahisi kuhimili vikwazo hivi,  kesho mungu alisaidia ikafika, mapema nikaamka nakujiandaa, baba hali kadhalika,alikua amejiandaa,  akanipakiza kwenye gari yake ikaanza. Safari yakwenda kupima ukimwi,  daa jamani najuta yaani ni bora ningeyajua jana tuu majibu yangu maana  naona presha inaanza upya,  aaah. Sio mbaya kufanya maamuzi haya, leo ndio leo naenda kujua hatma ya maisha yangu,  wakati nikiwa kwenye lindi hilo la mawazo nashtukia tumefika hospitali ya aghakan,  mzee kuna mtu anajuana nae pale ni Doctor pale aghakan,  basi alizunguza nae kisha,  akanitambulisha kwa yule Doctor kuwa mimi ni. Mwanae wapili,  tulikua wawili mimi na batuli, mzee alikua kazaa majike tuu,  mimi sikua na mengi sana nilikua nawaza mambo yangu mimi ukijumlisha na vipimo,  doctor,  mwanjara, alinisalimia kisha mzee akaniongoza teyari kwa ajili ya kwenda kupima, kuna kativii huwa wanaonyesha pale na. Viti vinakua vingi kidogo kwa ajili ya wale wanao subiri kupima, nilikaa pale kama foleni, watu walikua wengi kiasi kama watu kumi hivi,  kitu nilicho jifunza pale ni kwamba mtu haongei au hacheki ,wala hawezi kukuuliza na hamna anayeomba nafasi yake au zamu yake ifike ili aende kupimwa kama ilivyo kwenye magonjwa mengine,  palikua kimya sana, baadhi walikua ni wapenzi ambao nafikiri walikua wanakuja kuhakiki kama kweli waposalama au, lah, wengine ni watu wa umri kama wangu tuu,  kitu ambacho kilinifanya nitabasamu ni kuona kipindi cha kwenye Televishen, kilikua nikipindi cha ze comedy,  yaani mpaka marudio yanaisha hamna alie cheka, hamna wala alie ongelea chochote ,ni kama vile tulikua tunaangalia picha yakutisha,  baada ya kuisha ze comedy yakawekwa matangazo ya ukimwi na umuhimu wa kupima ukimwi,  kwa mimi nilikua sina hofu sana nilikua naishi kama mtu anaye ijua afya yake, muda unaenda sana jamani ilikua inakaribia zamu yangu, nilijiandaa huku tumbo na haja vikinibana, nilijikaza tuu kisabuni,  watu wengine wanatoka wamenuna na wengine wanacheka basi, hamna anaye elewa siri zao, bali wao na daktari, ghafla baba alinishtua kua zamu yangu imefika, na inabidi niende, nilinyanyuka  nakuanza kuelekea kwenye chumba cha daktari.....  daktari..", karibu sana naitwa dokta fredy, ni mtaalamu wa magonjwa ya zinaa napia ni mtoa ushauri nasaha kwa walio athirika na wasio hathirika, napenda kukuambia kua, umefanya uamuzi sahihi kuja kupima ili ujue afya yako, kuja kwako kupima kutakusaidia, kujua kama unamaambukizi, au lah napia itakusaidia kujilinda endapo utakua na maambukizi kwa kutumia dawa ambazo zitakusaidia kuongeza siku zakuishi na zitapunguza athari za vijidudu vya ukimwi,,  sasa basi tuongee, kama mtu na rafiki yake nitakuuliza maswali na naomba unijibu kwa usahihi maswali nitakayokuuliza kwa ufasaha"

......" hilo lilikuwa trela tuu picha kamili ilikua, ndio inaanza nikajikaza mtoto wakike, nikaitikia kwa kichwa tuu kwamba nitajibu kila kitu kwa ukweli na ufasaha"

...daktari..." unaitwa nani".....habiBa...." habiba"
....daktari..." unaishi wapi" ......habiba...." mwananyamala" ....daktari...." umeshawai kufanya mapenzi bila condom"......habiba...."  ndio".....

...Dakari..." mara ngapi umefanya mapenzi bila kinga".......habiba...."mara nyingi tuu zaidi ya mara kumi"...
....daktari..." umeshawai kufanya mapenzi na mtu usiye mjua , safarini, na bila condom"...
...habiba...."hapana".....daktari...." kwanini umekuja kupima" ....habiba..." nataka niijue afya yangu"....
....daktari..." ukijijua unaukimwi utafanya nini,"
...habiba...." nitaishi kwa matumini nitawashauri wenzangu na nitatumia dozi ili kuepuka maambukizo zaidi,"..
..daktari....." na ukijijua huna ukimwi, utafanyaje,"..
...Habiba...." nitajiweka mbali na ngono zembe na sito rudia kufanya mapenzi bila condom"...
....daktari..."nani kakuambia uje kupima"...
...habiba...." ni mimi mwenyewe nimeamua uamuzi wakuja kupima ili niijue afya yangu,".....

....daktari..." hongera kwa uamuzi wako na naomba uwe na moyo huo na uwashawishi na wengine pia wawe na moyo huo, basi habiba tutaanza vipimo na nakuahidi ni rahisi kuchukua vipimo na majibu hayatachukua muda sana"

....." zoezi lilianza lakupima ukimwi walichukua damu kubwa kwenye kigimbi cha mkono wangu, baada ya mda mchache vipimo. Vilikamilika nikaanza kusubiri majibu hayakuchukua mda pia, dakika chache tuu kiutaalam zaidi,  doctor alikuja na karatasi, iliyoonyesha majibu yangu na kuanza kunitajia, huo ndio ulikua wakati mgumu saana,nilijikaza kisha nikajiweka teyari kupokea majibu yangu japo nilihisi nayajua"....

....Dokta..." habiba teyari vipimo vimekamilika, na haya ndio majibu yako naomba niyaseme mbele yako, kumbuka kua tupo pamoja na usije kufanya kitu cha ajabu kama ukifanikiwa au usipo fanikiwa, naomba upokee majibu haya, "
...."enheeee, mtoto wakike naumbuka mkojo huoooo,"
.....dokta....." NIMEPIMA VIRUSI VYA UKIMWI,, nimegundua kua huna kwakua hakukua na kirusi chochote cha ukimwi kitu kilichopelekea kuwa NEGATIVE,  na naomba nikujulishe kua huna maambukizo ya virusi vya ukimwi, yaani uko salama kabisa huna tatizo lolote"......
....." hata kabla hajamaliza niliruka juu mtoto wawatu full kunengua hadi vigelegele, atafanyaje daktari wawatu zaidi yakucheka na kuniomba nitulie lakini haikuwezekana zaidi ya kusubiri nitulie kwa amri yangu mwenyewe, baada ya dakika tano nikatulia nikawa namsikiliza kwa makini,"
....dokta...." hongera sana habiba kwa kutokua na ukimwi na kwa kuchukua jukumu lakuja kupima, naomba nikushauri uilinde afya yako na kuwa makini na vishawishi, napiai naomba baada ya miezi mitatu uje kupima tena ili uwe na uhakika zaidi, ni hayo tuu habiba, haya hapa ni majibu yako na, pole sana kwa wasi wasi,na hofu uliyokua nayo, wakati wamazungumzo,"...
....dokta alinitania kidogo sikusita kucheka yaani ile ndio ilikua siku yangu yafuraha, tangu aliponiacha kevi, daa niko safi niko poa daaa acha tuu, ngoja niende kumuelezea baba yaliyojiri,  nilitoka nje nikiwa mwenye furaha sanaa yani kupita kiasi, nilimfuata baba pale wanaposubiria wagonjwa nakumkumbatia, baba alijua kua nipo salama kwa ile furaha alioniona nayo na kwakweli nilikua nafuraha sana, haikuwa vigumu mtu kujua kua nimepima na nimeonekana sina virusi, raha tupu ilinitawala, nilimkabidhi baba ile karatasi ili ahakikishe mwenyewe, baada yakuona kua nipo safi alifurahi zaidi, natukaanza kwenda zetu, nili waaga watu wote mule hospitalini wakati sikumsalimia mtu wakati naingia,  wakati tunatoka nje niliongea na baba kwamba kuna mtu nataka nikamsalimie ni raiki yangu mage, baba hakuninyima ruksa alinisihi tu, kua nisichelewe kwa ajili ya sherehe itakayofanyika pale nyumbani,  kusema kweli lengo lilikua sio kwenda kwa Mage kwanza sina rafiki anaeitwa mage ile ilikua zuga tuu nilikua naenda kulee, magomeni kwa jitu lile lenye roho mbaya, nilipanga niende kumwambia kua umalaya sifanyi na kama anazisambaza  picha zangu za utupu mitandaoni azisambaze tuu, sina shida nazo. Nilipanda gari mapema nikawa niefika pale magomeni hapakua nafoleni saaana, ilikua ni jumamosi, ilikua ni mida ya saa nne kasoro, nilifika pale ofisini kwake ,nilikuta katoka kidogo, nikakaa kama dakika mbiki hivi, nilipoamua kumpigia simu, niliskia sauti yake nyuma yangu,,"

.....Roho mbaya....." kweli wewe mtanzania tumeahidiana vip na unafika saa ngapi,haya mama chukua huu mzigo upeleke karia koo kwenye duka la patel nitakuelekeza pindi tuu utakapokua maeneo ya mnazi mmoja, ukifika mnazi mmoja utanipigia simu na nitakupa maelekezo yote, jitahidi ukifanikisha, adhabu yako itakua imeisha kabisa,"...
....habiba...." kwaio nikipeleka nikimaliza picha zangu unanirudishia na kila mtu anafanya yake? Na hamna tena kujuana,?....
....Roho mbaya....."ndio haswaa habiba, maliza zoezi hili kisha uwe huru, naahidi hutoniona tena na wala hutosikia sauti yangu,"

....." hiii huyu jamaaa bwege nini mbona kazi ndogo sana, ahhh namshukuru mungu leo siku nzuri sana kwangu,,nilijisemea kimoyo moyo"
...roho mbaya..." basi habiba chukua huu zigo na uupeleke kariakoo, vipi nilikuambia uvae vizuri, mbona baibui tena, na nilikuambia uvutie, nakuona unabaibui, vipi tena"?
.....habiba...." we usihofu bwana ndani ninakila kitu, nilimvulia baibui nakubaki na kimini cha bluu, alinikubali mwenyewe, basi alinipa mkoba fulani waki sister duu hivi, ambao ndani anadai kua ndio kuna mzigo, niliubeba ule mzigo, nikapanda dala dala mpaka karia koo, teyari kwa ajili ya kuupeleka mzigo, nilikua sina wasiwasi kabisa,  ilinichukua kama dakika kumi natano kufika mnazi mmoja si unajua sio mbali wala nini kutokea pale magomeni, hatimaye huyoo, nikatoa simu ili kupata maelekezo, alinielekeza kua ni duka la tatu kutoka mwanzo wa maduka ya spair za magari, niliangaza hatimaye nikalioa ,alinielekeza kua nionane na mzee patel, alisema ni muhindi ivi, nilifika kweli nikamkuta mzee patel, pale dukani sikuongea mengi nilitaja namba, yule jamaa wa magomeni aliniambia nitaje namba ambazo ni moja moja, ili mzee pateli aweze kunitambua, nakweli nilizitaja, zile namba nikampa kile kimkoba, na yeye akanipa kamkoba, kingine kama kile nilichompa mimi, rangi ile ile,  niliuchukua ule mkoba teyari kwa ajili ya kurudi na kumpelekea yule jamaa magomeni, sikujua ni nini kimo ndani ya mkoba nilichowaza nikubeba mkoba na kuondokana na maisha yale yakuishi kiuoga,  nilifika haraka pale magomeni nilimkuta yule jamaa, kama kawaida yake pale dukani sijui anauza nini maana hata wateja hamna, aah atajijua bwana, nilimpa mkoba wake"

......habiba...." haya mimi naomba memory card na hizo lap top, kama ulivyo niahidi,  mzigo wako huo apo nafikiri itakua vizuri kama kila mtu hatobadili msimamo wake"

.....roho mbaya....." sawa habiba nimekuelewa lap top hizi hapa na memory card hii hapa, na sina copy nyingine zaidi ya hiyo, na naomba uamini maneno yangu siwezi badili msimamo wangu, akhasante sana, na huu ndio mgao wako alinipa kibahasha cha kaki , nilikibeba nikakiweka kwenye mkoba, nikabeba nazile lap top, zikawa zangu tena, na hivi nilikua sina lap top we acha tuu, huyooo mwanamke kama siamini vile jinsi siku ilivyoenda vizuri, nilifika nyumbani nikakuta kuna ndugu baadhi, na kuna kamziki kidogo, ilikua ni sherehe aliyoniambia baba, nilizidi kufurahi, nilirudi chumbani kubadili nguo, nikatoka na nguo zangu nyingine za heshima tuu ukiachana na baibui, basi tulisherekea na baadae wageni waliaga kuondoka , tukawasindikiza, tukabaki wenyewe, tulikunywa shampeni, na waine kidogo, lakini, ilikua ni raha sana mimi ,batuli, baba ,namama mkubwa yaani we acha tuu, full raha,  muda ukafika kila mtu akaenda kulala, wakati naenda kulala nikiwa nafuraha bila kifani, nilienda kuziwasha zile lap top, nakupekua mizigo yangu, nilizikuta zile video nikazifuta zote , pamoja na picha , nilifungua kile kibahasha nikakuta kuna fedha nyingi sanaa, mpaka nikaogopa, nilikuta shilingi, milioni mbili, duuu. Nikaanza kuogopa"

Itaendelea fuatilia toleo lijalo

Habiba itakuaje mbona fedha nyingi kapewa,

Je abiba alipeleka nini kwa patel 


Sehemu ya 9

Mtunzi Long live josephat

Ilipoishia toleo lililopita,......."habiba anafanikiwa kujiunga chuo na anakutana na memba wake aitwae kemirembe wanaongea mengi ikiwemo kujulishana mazingira ya chuo nakadhalika, habiba anapata hisia tofauti, huku akiwa na hamu yakukutana na member wengine songa nayoooo".....

" si taabu sana kuongea na Kemi, tuliongea vitu vingi sana na baadae aliniambia tutoke kwa ajili ya kwenda kununua chakula niliuliza kuhusu maeneo yakula mule chuoni, alidai kua nje ndipo wanafunzi wengi wanapendelea kwenda kula tofauti na mule ndani nikwamba eti chakula cha mle ndani hakivutii, basii tukawa tunaelekea nje kwenda kula, nilimuuliza sehemu gani wanafunzi huwa wanapendelea kula alinijibu ni kwa pablo huwa wanaenda kuchukua chipsi kisha wanarudi nazo ndani kama take away, Kemirembe alikua anayajua mazingira ya chuo vizuri alisema dada yake alikua anasoma pale hivyo haikumuwia vigumu sana kupajua pale mwalimu nyerere, nilikua nina maswali mengi sana yakumuuliza kemi, la kwanza nilianza na swai la makaburi, nilitamani kujua yale makaburi yana uhusiano gani na chuo maanaake niliyaogopa sana,

....." Eti kemirembe hivi haya makaburi ni ya walimu wa hapa au ni ya viongozi?"..
......." nilimuuliza kemi kwa ustadi kidogo lengo nikujua tuu yale makaburi imekuaje yapo mule chuoni,"..
.....Kemirembe....."  mmh mwenzangu kwa srory nilizo ziskia ni kwamba haya makaburi ni ya wachina sijuiii, inasemekana ndio walikua waanzilishi wa hiki chuo, cha mwalimu nyerere na kwenye zile hosteli ndipo walipokua wanakaa, kwahiyo baada tu yakufariki walizikwa maeneo haya ndio maana mpaka sasa unayaona yapo bado na yapo mpaka sasa kwa ajili ya kuwaheshimu waanzilishi wa hiki chuo,"..

...."kemirembe alitiririka mwenzangu, alinipa kila kitu nilicho hitaji kukijua sasa nikawa nimepata mwanga kidogo juu ya historia ya chuo sio mbaya lakini nilijisifu kwa hilo wakati tukiwa bado tunaelekea kule getini ili tukanunue vyakula tuje navyo nilimuuliza swali jingine kemirembe, nilitaka kujua juu ya masomo na walimu labda ni mwalimu yupi mnoko si unajua tena ili mtu ujipange,"

.......habiba...." ivi kemirembe wewe hujaskia skia juu ya walimu wa hapa pengine yupi ni mnoko au yupi anafanya somo lake liwe gumu, lazma atakuwepo tuu watu kama hawa hawawezi. Kukosa, vip kwa hapa ni yupi?"

...."nilikua nataka story ziende si unajua tena, kibubu bubu, hainogi, na mimi nilikua sina wakuongea nae zaidi ya kemirembe kwaio sikua najinsi ilibidi tuu nimpige maswali, alafu nayeye kujua kidogo historia ya chuo kulinisaidia kufahamu mambo flani, mimi tena habiba, siku yakwanza tuu teyari nataka nijue A, mpaka .Z,  basi kama kawaida mtoto wawatu kemi kwa ufupisho, wa kemirembe alinijibu. sipendi kurefusha jina huwa napenda kufupisha kuweka angalau swaga, siunajua tena, basi ndio hivyo kemi alinijibu lile swali langu kuhusu walimu wa pale"..
..Kemi...." mmh ndugu yangu kwakweli hapo ndio utata mimi sijawahi kusoma hapa lakini kwa story nilizokua napewa na dada yangu, naskia kuna mwalimu anaitwa Kiowi, naskia ni mtata dada unaweza ukakata tamaa yakusoma anamadongo, lakini naskia ukimzoea mnaenda nae vizuri tuu, hana neno mwisho wasiku ni wachache huwa wanafeli somo lake ni mwanaume lakini ni mwalimu mzuri watu wanadai, lakini shoga sikufichi, naskia tetesi za kutakwa na walimu pia zipo yaani inabidi tuwe makini, maana wakikuona umenona tuu  basi mate hayo yanawatoka, ila chuo kipo poa wangu"...

....kemi alinijibu swali langu jingine lakini nikawa natafakari juu ya kutakwa na walimu ,duu sasa hii si balaa tena kweli kila sehemu ina majaribu yake,  baada ya muda kidogo tukawa tumeshatoka nje ya geti la chuo sio mbali sana na kwa muuza chips alikua getini tuu tulitoka nje,
 niliskia mlio wa sms nikaifungua simu yangu ili kuisoma sms ile,  ilikua meseg ya james ,alikua ananijulisha kua nayeye kapata chumba pia pale kizota chumba namba 132, aah sikumjali saana sikutaka ajue kua namimi nimepata hapo kizota, nikaendelea na Kemi wangu , tukaagiza chipsi pale kisha kila mtu akashika mfuko wake safari yakurudi ikaanza, nje kuna madereva boda boda wengi tuu, tulipata pikipiki moja tukawa tunarudi nayo kabla hatujafika mbali kemi aliniambia kua tumesahau maji yakunywa kwahio inabidi nishuke nikayafuate,nilipofika tuu pale getini nikakutana na mvulana mmoja alikua ananisalimia, niliitikia lakini yule kijana akawa anafosi story na mimi, sikumjali lakini aliendelea kunibuguz ndipo nilipoamua kumkashifu yule kijana,"
.....habiba....."  eeh we kaka hujui kama mtu kakataa sitaki nimesema sina muda wakupoteza kipuuzi, naomba uniache nifanye mambo, yangu umenisalimia nimeitikia ,nini tena unataka, aaah watu wengine bwana"......

.....

"Hayo ndio maneno niliyo mtolea yule kijana alibaki kimya hana lakuongea lakini , niliwaza sana yaani siku yakwanza tuu vidume vimeshaanza kunifuata, nilijipa sifa ,lakini ujue bwana sisi wanawake yaani ukiitwa au kusumbuliwa jua kua unalipa mwenzangu, nilijiona nimetisha sana kwa mara yakwanza kigamboni nasumbuliwa, nilijipa credit, zangu lakini yule kijana alikua mzuri kiukweli sema basi tuu naye mlevi yaani  hata kuja kistaarabu yeye  anavamia tuu, potelea mbali wapo wengi, hawa ndio wakina kevi wenyewe hawa, nilijisemea huku nikiwa natafuta duka lilipo, hatimaye nikafanikiwa kupata duka na kununua maji, upesi nikamuwahi kemi, ile nafika getini nikakutana tena nayule kijana safari hii naona alikua kajifunza hakunisemesha, nilijichekea mwenyewe, maskini kaka wawatu kanywea ,na nilivyo mtingisha kajua kua anaongea na mtu mwenye akili na maadili yake kumbe angejua hamna lolote, yeye tuu na kutokujiamini kwake, nilimpita kama sijamuona kisha nikamuwahi kemi, alikua kasimama mbele kidogo, nilipofika tukakwea wote boda boda safari yakurudi chuo ikaanza, mara moja tukawa tupo teyari hostel,wakati naongozana na kemi niliskia sauti ya mtu ananiita"..

......"habiba, habiba habiba",....."alikua ni james naijua sauti yake hivyo sikupata taabu kuitikia , alinifuata mpaka nilipo nilikua karibu kidogo na bweni la muongozo, kemi naye alisimama na mimi, tukawa wote tuna mngoja james, baada ya james kufika tukasalimiana na james na nikamtambulisha kwa kemi kama rafiki yangu, kemi alikaa kidogo kisha akaomba atangulie na vyakula ili nibaki naongea na james kwa uhuru, nilimpa mizigo yangu pia atangulie nayo, basi akatuacha pale chini tukiwa na james, james aliniomba kidogo tusogee karibu kwenye yale makaburi, niliogopa lakini mingefanyaje, ilibidi nijikaze , haoo tukawa tumesogea zikaanza story, bwana baadae zikaja za mapenzi, nikawa nataka kubadili mada lakini nikawa nazidiwa na utashi wa james kwenye mapenzi, tukawa tumefikia hatua mbaya  sasa, "

.....habiba...." Lakini james hapa tutaaa tutaaonwaaa bwaaana, ebu niache kwanza watu wanapita,"..

......"uwiiii james keshaanza mambo yake aaah!!! , alikua keshaanza kunipandisha, kwakweli ilibidi nijitahidi kukataa maana hata yeye kwa miguno niliyokua natoa nikawa nampa moyo wakuendelea , hata ivyo ni muda mrefu tangu nimeipata huduma yake na matatizo pia yalichangia kuikosa huduma ile, basi ningefanyaje unafikiri nikabidi nimuachie kijana wawatu atalii ndani, na nje ya mwili wangi, taratibu kabisa, jicho likawa legevu sana nikawa sina hali tena, jamani nyie acheni tuuu, watu walikua wanapita mbali sana, nilikua nimemlalia james mabegani kama mgonjwa, nikawa nasubiri kutibiwa tuu, duu lakini kilichotokea fahamu zote zikanirudia uteja wa hisia wote ukapotea nilimuona mtu anatoka kwenye makaburi, na alikua anakipensi tuuu, wee niliruka utazani nimepigwa na shoti, james mawazo yake yote alikua anajua nimekolea, ndipo nilipomwambia kua kunamtu, nimemuona anatoka makaburini, alicheka kidogo kisha akaniamabia kua ni jambo la kawaida itakua alienda kuanika nguo zake kwaio kaenda kuzianua, hata yeye eti anadai kesha enda mpaka ndani ya yale makaburi yaliyokua yamewekewa uzio, mmmh nilisita kuendelea nazoezi ilibidi nimuage james kwakweli, nilimuaga haraka kisha nikawa napanda zangu, juu kuelekea kwenye chumba changu, kwenye ngazi nilikutana na paka wawili, weusi, jamani mimi kwa imani za kishirikina ndio mwenyewe ,wacha niogope ile minyau miwili iliondoka nikapanda haraka haraka, wakati matokea kwenye corido baada yakupanda ngazi, nilimuona kijana mmoja ambaye nilikua namfananisha alikua katoka chumba fani ivi alinipa mgongo lakini baada yakuona hageuki nikaamua kuingia ndani kwangu nilikuta kemi keshaanza kula chipsi zake nikajiunga nae na mimi nikatoa zangu nikaenda kunawa, ilinibidi niende bafuni kwanza mwenzenu si mnajua tena nilikua nimeharibika kidogo nikaona ni bora nipitie bafuni kabisa ili ninawe niondoe ma mambo flani, nikabeba kikanga changu ambacho ndani kina nguo zangu za ndani huyoo bafuni,  huko bafuni kwenyewe kukavu yaani hapajatumika muda mrefu nahisi ni kwasababu yalikizo , siunajua tena baada yakufunga tu chuo maeneo yachuo ni nadra kutumika ikiwemo vyoo na mabafu , basi nikawa naoga mlango sikuufunga, maji ya mvua tena, nikawa naoga bwana ila nikashtuka tena kuna mtu nahisi alikua ananichungulia, sasa sijui ni fikra zangu au kweli, ikabidi nitoke nimejishika na kanga yangu mpaka kule nje ile natoka tuu nakutana na yule kaka anakata kona anaishia sikumuona sura niyule yule aliyekua kasimama mlangoni, na nilipata kumbu kumbu alikua ni yule kaka ambaye alikua anataka kunitongoza kule getini,

Itaendelea fuatilia Usiku wa habiba hostel,

Vip ni kweli kuna vitu vya ajabu chuoni kwa habiba


Sehemu ya 10

Mtunzi long live josephat,

Ilipoishia toleo lililopita, "habiba ana fahamishwa na kemi juu ya story za makaburi habiba anapata uelewa kidogo juu ya historia ya chuo baadae wananunua chakula ( take away) wanarudi habiba anakutana na kijana anayejaribu kumtongoza habiba anakua mkali yule kijana anakubali kushindwa, wakati wanarudi wanakutana na james habiba anaongea nae nakisha wanaamia kwenye mahaba, inashindikana james kufanikisha tendo kwa uoga wa habiba,  baadae habiba anaenda hosteli anaingia bafuni anahis kuna mtu anamchungulia wakati huo anakumbuka kua shati alililomuona nalo mtu aliekua akichungulia ni kama la yule kijana alie mkalipia asimtongoze songa nayoo"..

" mmh hii sasa inatisha lohh!!! Mimi hii hali itanishinda siwezi kwakweli, mbona sina amani kabisa,ngoja nimuulize kemi anaweza kuniambia kitu juu ya haya mauza uza wakati najiandaa kwenda kuchukua nguo zangu bafuni, nikakuta jina langu kwenye kioo, lilikua limeandikwa kwa maandishi ya mvuke, hapo sasa nilihisi nina presha ya kushuka, yani ilinibidi nisismke mwili mzima, daa hamu yakuoga ikaishia pale nilirudi upesi baada yakuchukua nguo zangu, sabuni zilikua bado hazijatoka vizuri kichwani, nikaingia haraka chumbani kama nilikua nakimbizwa nakitu cha hatari nje, nilifunga mlango nikaanza kuangaza kemi alipo, kemi hakuwemo kabisa mule ndani nilizidi kujawa na hofu akili yangu ilikua teyari imesha jenga uoga ambao nilihisi unachangiwa na imani za kishirikina, baada ya muda nilihisi mwili wangu woote umekufa ganzi nikawa sina lakufanya, nikabaki naduwaa mule ndani naangaza tuu nisifanye lolote, basi nikashtukia mtu ananigusa mgongoni, mawazo yangu na fikra zangu zilikua bafuni juu ya lile tukio, nilipoguswa nilipiga yowee la uoga kana kwamba nimeona tukio la hatari, sikupata muda wa kugeuka, ila baada ya kupiga yowee nikihisi nimeguswa nakitu cha hatari ndipo nikaamua kugeuka  nikakutana na sura ya Kemirembe, kidogo nilifarijika ila nikiwa nahema kupita kiasi ,nikabaki namkodolea macho kemi nisijue nimwambie nini"

..kemi..." vipi shost, mbona unashangaa kama umeona jini, kulikoni?, na hizi sabuni maskioni na mikononi, kuna nini,?"...
..." kemirembe aliniuliza maswali mfululizo, nakweli yalikua yananihusu sana nikawa natafuta nianze kumjibu lipi, maana hali ilikua mbaya nilitafakari kisha likaja wazo,  mimi tena cha uongo nikampa uongo sikutaka kemi aanze kufikiria kua mimi pengine muoga au nina imani za kishirikina, nilimjibu kiustadi kidogo sikutaka kumuachia ushahidi wala maswali kichwani mwake,"...
.......habiba....." aaah!!! ndugu yanguu ume nishtuajeeee,!! hapa nilikua nimekuja kuchukua taulo langu nikakumbuka na vichupi vyangu baadhi ni vichafu kwaio nikaamua nije kuvichuka nikavifue ili nikija kulala nilale tuu, sasa nilpo kukosa humu nikawa najiuliza utakua wapi kwaio nikashtuka ulipo nigusa sikutegemea"...
...nilimkwepa kwa stahili ile ila mwenzenu mtetemeko nilikua bado ninao sikua naamani kabisa nilikua najichekesha tuu najikaza ila baasi tuu,, niliamua kumtwanga swali ili aache kunidadisi nilibadili mada upesii"

........habiba....." hivi kemi hujamuona mtu anachungulia hapa ,alikua pale karibu na bafu "
....kemi..." hapana sijamuona mtu yeyote nilikua nimeenda kutupa mifuko lakini sijamuona mtu yeyote kupita kwenye corido"..
......." mmmh kemi sasa alikua ananikatisha tamaa sasa yule aliekua anachungulia ni nani kama sio mtu, maana ni muda mchache tuu sasa kemi anasema hajamuona mbona sielewi na yeye alikua nje, au yeye kemi ndio alikua anachunguliaa?, maana huku chuo bwana ushirikina nje nje huwezi jua yupi ni yupi yawezekana ni huyu binti chamsingi kua nae makini tuu, nilikua najisemea mwenyewe lakini nilikua namuhukumu mtu ambaye sina hata uthibitisho kua ndio yeye. Aah basi nikaamua kuzuga tuu pale ndani,nikanyakua vichupi vyangu nikawa naelekea sasa bafuni, uongo mbaya jamani yaani nilikua nataka nimridhishe kemi kua kweli narudi tena bafuni, nilirudi nikawa naenda huku naangalia pembeni nageuka nyuma, yani kama mtu mwenye wasi wasi vilee, nikawa nimekaribia bafuni, kulikua kuna mtu anaoga niliskia maji ya mvua yanamiminika, sikua na uhakika kua kulikua nawatu wawili au lah!!, nilibaki najiuliza baada yakuona kuna nguo  zilizonin'ginizwa juu ya mlango mbele, kulikua kuna suruali, shati, sketi na skin jeans, ni wazi kabisa yalikua ni mavazi ya watu wawili tofauti, ila nilikuja kuamini zaidi, baada yakuskia sauti, sikuiskia sauti yakiume lakini niliskia sauti ya mwanamke alikua, akigugumia juu ya utamu yaani  utamu wa mahaba, niliskia akilia kwa mahaba huku akitaja jaina la mpenzi wake nahisi atakua ndio huyo mwanaume ambaye alienae mule ndani bafunii, basi nikawa natabasamu tuu naumbea nikawa nauleta nijifanya naoga kumbe nafuatilia ya watu, nilijifungia taratibu kwenye bafu la mwisho nikawa nipo kimyaaa!! nakula uhondo kwa kuskia tuu, daa kwakweli walinipandishaaa, wale mafuska, nikatamani niende kwa james, ila sasa sauti zikawa zinazidi, kilicho nifanya nifikirie mara mbili mbili, ni ile sauti ya yule dada sijui ilikuaje , yaani nilikua naskia kama sauti yabatuli vile, sikuelewa kwakweli, ila niliamua kuwaza pengine itakua sauti zimefanana siunajua tena kwenye mahaba sauti za kugugumia utamu nyingi huwa zinafanana, nilijiosha haraka nikajimwagia kisha nikaanza kwenda taratibu chumbani, safari hii sikua na uoga kwakua nilikua nina company mule bafuni japo company yenyewe ilikua yakichoyo, basi nikafungua mlango nikaanza kummwagia umbea kemirembe,"

...habiba..." shogaa!! Nilichokutana nacho huko bafuni huwezi amini yaani nimekuta minguo imetundikwa watu wapo ndani wanafanya mambo yao, kweli hiki chuo shoga yaani nakwambia bafuni kunawatu wanafanya mapenzi, kama huamini nenda sasa ivi utawakuta kama hawaendelei basi wanavaa nguo zao maana ndio natoka huko, ni miguno tuu, we acha tuu"
..."  kemi naye kwa umbea hajambo, huyooo, teyari kaenda kushuhudia, yaani hata hataki kupoteza muda, baada ya dakika mbili namuona anarudi kanuna"..
.....habiba..."  vipi tena shost umemfumania bwanaako nini, mbona ndita zimekunjwa,?"

....."nilimuuliza kemi swali jepesi nijue nini kimemkwaza"...
...kemi...." si bora angekua bwanaangu ningejua namkanya vipi, ila hamna mtu wala dalili ya mtu mule bafuni bafu nililokuta walau kunavimaji ni bafu unalosema ulikua unaoga wewe ila haya mengine ni makavu na hakukua na dalili yakua na mtu au watu"..
..Habiba..." heee basi makubwa shost, maana muda si mrefu nilikua naskia miguno na watu walikua wanaonekana sio wakumaliza mapema walee, mi nimeacha wanaendelea alafu maji pia yalikua yanatiririka nashangaa unavyosema pakavu na wala hamna dalili ya watu kuwepo mulee,"..
...kemi..." basi ndio hivyo shoga hamna mtu labda watakuwa waliondoka punde tuu ulipoondoka"..
..." duu hii kali lakini niliitikia tuu kuondoa maswali mengi eti kemi anasema hamna maji alafu eti hamna dalili ya watu kuwepo wakati nilipokua napita niliskia maji yanatiririka na miguno kibao, hata ivyo niliskia neno badili condom hata dalili ya ganda kutakua hamna basi hii miujiza na mpaka naondoka niliacha mchezo unaendelea na sio wakuisha punde tuu, na nimeongea na kemi hazikupita hata dakika mbili anasema hajaona kutuu, mmh si balaa hili nikawa nJisemea mwenyewe maanake sasa ishakua balaa, mauza uza tuu, muda ulikua umeenda yapata saa nne na nusu, nikaamua kuingia kulala nikakumbuka nimesahau soap dish na sabuni pia , niliona uvivu ila ilinibidi niende kuvichukua tuu siunajua sio nyumbani pale kwaio nikajikaza,nilipo fika nikaongoza moja kwa moja bafu la mwisho nikachukua sabuni yangu, ila kipindi narudi nikakutana na suprize, ilikua lile bafu la pili ambapo nilikua naskia watu wanafnya mapenzi nilikuta boksi la condom alafu kibaya zaidi palikua pameloa sana na nilikuta condom nyingine ambazo zilikua zimetumika, zipo nne, mmh hapo nilishikwa na bumbuwazi, mlango ulikua upo wazi woote, nilipo amua kuingia zaidi, nikakuta, chupi pia nyeupe imesahaulika mule bafuni,  sukutaka kuhoji lakini nilihisi pale kutakua nakitu tuu kanaendelea, basi nikaamua kwenda room kwangu ,kufungua mlango nakuta, kunamtu kalala kwenye kitanda changu nilijua ni kemi lakini kemi nilimuona kwenye kitanda chake,"

Itaendelea fuatilia , vp habiba yapi tena yamemkuta
Ni hapa hapa. Mimaz official blog usikose tena kesho kupata muendezo sehemu ya kumi 11

mawasiliano 0754545194 au
 ni follow instagram mimaz official blog kwa update zaidi

Post a Comment

 
Top