0

Wanawake ni viumbe tofauti sana (complex) wao ni walezi kwa asili, waumbaji wa vitu, wasimamizi wazuri na wabunifu sana.

Wanaweza kwa urahisi sana kuelezea kitu kilichopo kwenye akili zao likija suala la deal lolote la biashara kama kununua au kuuza.

Wanaweza sana kwenye mambo ya design na hata mawasiliano. 

Ila likija suala mwanaume hapo ndiyo kuna tofauti.
Wanaume kawaida tunapenda kujua kwamba tumetimiza mahitaji ya wake zetu na itakuwa vizuri sana kama mwanamke atawezesha mwanaume kujua kwamba mahitaji yake kama mwanamke mume anayatimiza.
Kwa hiyo mwanamke ongea nini unahitaji, au nini unapenda kwa maneno au kwa matendo kwani kununa si jawabu au kubaki kimya si jawabu. 

Jawabu ni kuelezana tena kwa upole na upendo jambo lolote unahitaji mwanaume afanye.


Wanaume huhitaji mwanamke anayejua kukubaliana/kuafikiana
Je kama mume wako anapenda kuangalia au kucheza soccer siku za weekend kwa ajili ya kujiliwaza huwezi kuwa naye?

Kuna ubaya gani wewe kushangalia kile mume wako anapenda (hobbies)
Kumbuka maisha ndivyo yalivyo msipofurahi pamoja na kuwa na fun pamoja usitegemee siku mambo yabadilike yenyewe tu kuna kitu unahitaji kufanya sasa ili kesho iwezekane.
Penda kufanya pamoja kile kitu mume wako anakipenda katika maisha inaweza kuwa ni kuimba, jogging, kwenda kutembea sehemu yoyote ili pamoja au matamasha na michezo mbalimbali. 

Kumbuka unaweza kuwa wewe hupendi kwenda naye huko yeye anapenda kwenda, lakini kuna wanawake wanafurahi kuwa naye huko wewe umekataa kwenda na hana njia kwani ni kitu anakipenda na ni sehemu ya maisha yake (kama hatendi dhambi).


Wanaume wanahitaji mwanamke anayejua mambo
Huwezi kutenganisha habari za siasa, michezo, biashara, current news, sayansi na mambo ya kimataifa na mwanaume, hivyo usijiweke nyuma sana unahitaji kuwa mtu wa karibu kupiga naye story za mambo kama hayo, jitahidi na wewe kuwa wamo. 

Inawezekana jioni kabla ya kulala mkawa na glass ya juicemnakunywa wawili huku watoto wamelala, wewe mwanamke kwa ujasiri shusha story za michezo mambo ya Chelsea,Manchester united, Liverpool au hata Yanga na Simba just for fun, au hata habari za mafisadi au hata habari za mfalme Suleiman au Daudi au business ambazo umezitafiti hapo mwanaume atajua nina mke ndani ya nyumba.
Wapo wanawake mume akianza kuongea habari za siasa, michezo au business anaondoka zake na kumwacha naamini wanaume hapo huwa hawafurahii kabisa.
Nakwambia ukijua kuongea na mumeo mambo ambayo wanaume wote wanayapenda utafahamu mambo mengi sana kuhusu ulimwengu, watu na ninyi wenyewe.

Pia unaweza kubadilisha akili katika kufahamu mambo.
Hii huimarisha sana ukaribu na hamasa ya kila mmoja kutaka kusikia kwa mwenzake na matokeo yake ndoa inakuwa tamu maana huo usiku mkimaliza story lazima chumbani kuwake moto.

Mwanaume anahitaji mwanamke ambaye kwa mapenzi ni moto
Huwa kuna kawaida kwamba mwanaume katika jamii zetu za kiafrika ndiyo anakuwa mwamuzi wa mambo mengi kiasi kwamba hata wanawake wenyewe hutambiana kwamba jana mume wangu alinipeleka dinner sehemu.

Je, itakuwaje kama na wewe mwanamke siku ukamwambia mume wako leo pamoja na watoto tunaenda lunch sehemu au dinner sehemu kula, au kula kitimoto na nk pamoja na watoto wenu kwa hela yako au bajeti yako au maamuzi yako.

Wakati huo huo umetinga kiwalo chako cha nguvu (sexy) hadi unamkumbushia zile ezni zenu ambazo zilifanya avutiwe na wewe hadi kukuoa.
Wanaume wanahitaji wanawake wa aina hiyo ambao siku zingine wanafanya vitu romantic au sexy angalau hata kwa mwaka mara moja siyo mwaka mzima hujafanya jambo lolote la kuimarisha mapenzi.
Wanaume wanahitaji mwenzi siyo mtu wa kuishi naye chumba kimoja
Kuagana asubuhi na kuja kukutana jioni bila kuongea chochote mchana mzima ni dalili ya uhusiano usio na afya kabisa. 

Jaribu kufikiri mwenyewe hivi ukiondoka asubuhi unawasiliana na mumeo mara ngapi? 

Siku hizi karibu kila mtu ana simu ya mkononi, unaweza kutuma sms, au kumpigia just to say hi honey! Mbona wakati wachumba sms zilikuwa zinatumwa hadi vidole vikaota sugu, leo kunani?
Hamu na msukumo alionao mmoja kwa mwenzake ni msingi wa kuonesha afya na mahusuano yenye furaha.
Wakati mwingine mahusiano huenda bila mawasiliana ya mara kwa mara lakini hiyo ni sumu kubwa sana kwani inaweza kufikia kipindi hakuna hata kutakana, hamu ya kila mtu kwa mwenzake hupotea na hapo ndipo watu sasa huanza kuishi kama vile watu tofauti walioamua kuishi nyumba moja na chumba kimoja lakini ule moto umetoweka.
Kwa hiyo kama wewe ni mwanamke hakikisha unakuwepo katika mahusiano kwa maana kwamba unahitaji kumtia moyo mumeo, kumuinua pale anapokata tamaa uliza nini kinaendelea asubuhi, mchana, jioni na usiku, pia akifanya kitu kizuri mpe sifa na hongera. 


Jifunze kwa busara na hekima kujua nini kinaendelea katika maisha ya mume wako na pia onesha kwamba unamjali sana (care) na kwa njia hiyo automatically atakupenda zaidi na ndoa yenu itakuwa imara zadi.

Post a Comment

 
Top