0
Licha ya kudai kwamba skendo za ngono sasa basi, staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amekwaa aibu mpya baada ya picha zake kunaswa akiwa na mwanaume mwingine kwa mara nyingine, mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakiwa kwenye Mgahawa wa hoteli iliyotajwa kwa jina la Cape-town Fish Market iliyopo Msasani jijini Dar.

Chanzo cha  habari ambacho kilipenyeza kuwa, katika tukio hilo la hivi karibuni, staa huyo alikuwa hafahamiani na mwanaume huyo, lakini kuna kijana mmoja ambaye mara nyingi anawakuwadia mastaa wa Bongo kwa matajiri, alidaiwa kumtonya Wema kuwa kuna ‘mchati’ anataka kutoka naye.

Kilifunguka kwamba, baada ya Wema kung’atwa sikio juu ya Mkongomani ambaye ana ‘hela chafu’, alidaiwa kuonekana kuchachawa hivyo eti alikubali kupelekwa kwake akajazwe ‘mihela’.

Chanzo hicho kilizidi kumwaga habari za jikoni kuwa baada ya Wema kufika hotelini hapo, alitambulishwa kwa Mkongo huyo ambapo baada ya kusalimiana tu, walikaa pamoja na kuanza ‘kufanya yao’.

Mpashaji huyo alizidi kufunguka kuwa baada ya kukaa na kupata kinywaji cha kutosha, walianza kupiga picha mbalimbali bila kujali kama kuna watu wanaweza kuwapiga picha na baada ya hapo walianza kupigana mabusu yaliyowaacha hoi wapiga chabo a.k.a wavimba macho.

Mpashaji huyo alidai kwamba, baada ya Wema na Mkongo huyo kukutana na kumaliza ‘shida’ zao, kila mtu alichukua hamsini zake huku jamaa huyo ‘akim-block’ Wema kwenye simu.
Ukimwacha Mkongo huyo, huko nyuma Wema aliwahi kuripotiwa kutoka na wanaume kadhaa wakiwemo, TID, Mr Blue, marehemu Steven Kanumba, Yusuf Jumbe Yusuf, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na CK huku wengine zikiwa ni skendo tu na mwenyewe kuzikanusha.


Post a Comment

 
Top