Baada ya kukosa nafasi ndani ya CCM sasa ameanza kuwasha moto ndani ya UKAWA anasema magufuli atasoma number alichokisema lowassa
Waziri
 mkuu wa Zamani Edward  Lowassa  amewaahidi wafuasi wa chama cha 
Demokrasia na Maendeleo Chadema pamoja na wale wa umoja wa katiba ya 
wananchi (UKAWA) ushindi wa kishindo katika uchaguzi mku
u utakaofanyika oktoba 25 mwaka 2015.
Mwanasheria mkuu wa Chadema Tundu Lissu alisema kwamba  ili mgombea ameweze kuwania urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania
 ni lazima awe mwanachama wa chama chochote cha Siasa nchini Tanzania, 
hivyo Lowassa ni mwanachama halali wa Chadema pia amechaguliwa na vikao 
mbalimbali vya kamati kuu ya chama hicho iliyoketi hadi usiku wa manane.
u utakaofanyika oktoba 25 mwaka 2015.
Lowassa
 alisema hayo jana mara baada ya kukabidhiwa fomu ya kugombea urais kwa 
tiketi ya chama cha Demkorasia na Maendeleo ambayo itampa ridhaa ya 
kugombea urais kupitia umoja wa Katiba ya wananchi ukawa unaundwa na 
vyama vinne vya siasa nchini Tanzania ambavyo ni Chadema, NCCR-Mageuzi, 
Cuf na NLD.
Aidha,
 Lowassa aliyekabidhiwa fomu na Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na 
Maendeleo Chadema Freeman Mbowe katika ofisi za Chadema makao makuu 
yaliyopo Kinondoni jijini Dar es salaam jana,alichangiwa kiasi kadhaa 
cha pesa kitakachomsaidia katika yake ya matumaini iliyofufukia Ukawa. 
Katika hafla hiyo  Lowassa aliongozana na Mkewe pamoja na wana familia 
na ndugu wengine mbalimbali.
Uamuzi
 wa Lowassa kugombea Urais ulipokelewa kwa shangwe na umati wa wananchi 
uliohudhuria hafla hiyo makao makuu ya Chadema kinondoni jijini Dar es 
salaam.
Mwanasiasa
 huyo Mkongwe atapambana  na Mgombea kutoka chama cha Mapinduzi Dk.John 
Magufuli katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu utakaokuwa wa aina 
yake  mwaka huu wa 2015.


Post a Comment