Idadi kubwa ya  Watanzania sasa hivi wako kwenye subira ya kujua ni mgombea gani wa Urais atakaeuwakilisha UKAWA (Umoja wa Katiba ya Wananchi) ambao ni muunganiko wa vyama mbalimbali vya upinzani Tanzania.
 leo namnukuu Tundu Lissu ambaye ni Mwanasheria pia wa CHADEMA aliyeongea haya maneno Geita kanda ya ziwa ‘Tumeshapata
 mgo
mbea Urais wa UKAWA, ameshapatikana na mnamfahamu vizuri sana na 
mnampenda sana na ni mtu anaejulikana dunia nzima kwa msimamo wake, 
hatujamtaja jina najua na nyie mnataka nimtaje….. simtaji ila mnamfahamu
 vizuri sana’
‘Sababu gani simtaji ni kwa 
sababu tunatafuta mgombea mwenza wake, tukimtaja sasa hivi mtatuuliza na
 mwenza? tutawaambia ngoja tukamtafute? tunatafuta mgombea mwenza 
anaeheshimika nchi hii na ni lazima atoke Zanzibar katiba yetu ndivyo 
inavyosema, tukimpata tutaitisha mkutano na Television zote Tanzania 
siku nzima itakua ni siku ya Dr. Slaa !! ahhh nimetoa siri?!!!! hapana 
hapana hapana


Post a Comment