0

Waziriwa wa Utamaduni, Vijana na Michezo wa Sudani Kusini Mh. Stephen Lado Onesimo jana aliitembelea timu ya
Malakia FC wakati ikifanya mazoezi kwenye uwanja wa Karume wakati ikijiandaa kwa ajili ya mchezo wake wa leo dhidi ya KCCA ya Uganda mchezo utakaopigwa majira ya saa 8:00 mchana kwenye uwanja wa Taifa ikiwa ni mwendelezo wa mashindano ya Kagame Cup hatua ya makundi.


na nukuu alichosema “Nitakuwepo pia uwanjani kuwashuhudia mkicheza mchezo wenu, nahitaji mjitume kwa ajili ya nchi yetu ya Sudan na endapo mtashinda mchezo wenu, nawaahidi kuwapa zawadi. Nimezungumza na kocha wenu ameniambia tayari mnanafasi ya kucheza robo fainali ya mashindano haya, lakini mimi nahitaji mshinde mchezo huu ili mkacheze robo fainali mkiwa mnaheshimiwa”, alisisitiza. “Nidhamu kwenye mchezo ni kitu muhimu sana, kila mtu anatakiwa awe na nidhamu ya hali ya juu wakati wa mchezo, muelekezane wenyewe kwa wenyewe muwapo uwanjani nani anatakiwa kufanya nini ili kumpunguzia kazi kocha wenu. Mimi nawatakia kila kheri na ninaimani na ninyi na ninamatumaini tutashinda mbele ya KCCA”,  Alisema

Post a Comment

 
Top